Papa afikiria kuruhusu mapadri waoe

Mungu ameagiza tuoane na tuzaliane tuijaze Dunia sasa nyinyi wenzetu haya masheria ya ajabu ajabu mliyatoa wapi????
View attachment 623282

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amependekeza kubadili mfumo wa utumishi wa mapadre akisema itakuwa vyema iwapo makasisi hao wakaruhusiwa kuanza kuoa.

Hata hivyo, imefahamika kuwa pengine pendekezo hilo likawaruhusu mapadre wa Brazil pekee kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo. Hivi karibuni Askofu wa Brazil, Kadinali Claudio Hummes alimwomba Papa Francis kufikiria kuondoa sheria inayowakataza makasisi kufunga ndoa.

Ingawa pendekezo hilo la Papa Francis huenda likapunguza tatizo la uhaba wa wanaume wanaojiunga kwenye utumishi huo, lakini linatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waumini wenye msimamo mkali na hata pia kusababisha mgawanyiko ndani ya kanisa.

Ombi hilo linatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha baraza la kanisa kinachotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil.

Kanisa Katoliki linahubiri mafundisho ambayo yanapiga marufuku makasisi wake kufunga ndoa ingawa kumekuwa na baadhi wanaovunja mwiko huo na kuisha maisha ya ndoa. Hata hivyo, wale wanaochukua uamuzi huo hujitenga na kanisa.

Kasisi moja aliyetambulika kwa jina la Paddy O’Kane amenukuliwa na baadhi ya magazeti akielezea uwezekano wa Papa Francis kuchukua uamuzi wa kuwafungulia mapadre kifungo cha kutokua wakati wowote mwezi huu.

“Hivi karibuni nilimsikia Papa anataka kutekeleza ombi alilolipata toka Brazil kama jaribio lake la kwanza,” alisema.

Papa Francis na mtangulizi wake, Benedict XVI wamekuwa wakieleza kuwa suala la makasisi kutoruhusiwa kuoa siyo jambo lisiloweza kubadilika na kwamba jambo hilo linajadilika.

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma history of celibacy in the Catholic church. Utagundua kwamba mapadri na maaskofu na makardinali na mapapa wenyewe walikuwa ni watu wa familia mpaka karibu miaka elfu moja baada ya Kristo. Amri iliyotolewa kuwafungia inaweza kuondolewa kirahisi tu. Biblia inataka askofu na shamasi (yaani padre) wawe ni watu wenye familia- soma 1 Tim 3:1-13.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikutaka kuchangia lakini nimewiwa baada ya kujiuliza maswali kwamba Papa anapendekeza,kwa hiyo jambo hilo liliamuliwa tu kwa matakwa ya kibinadam na siyo SHARTI la MAAGIZO ya Mungu au tuseme andiko la Biblia.

Kwa namna moja inafikirisha sana mambo kama haya ambayo ni utashi wa watu na siyo maagizo ndani ya Biblia.
Mie ndio nashindwa kuelewa biblia hiyo wanatumia lutheran na madhehebu mengine ya kikiristo,kwa nini RC viongozi wa hawaruhusiwi kuoa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waruhusiwe mara ngapi namjua padre mmoja kazaa na nurse watoto watatu na inasemekana anazaidi ya hao kwa wanawake wengi na anawasomesha vizuri kabisa
 
Kwahiyo anayepanga sheria " katika dini ya Mungu ni binaadamu !!!? Aisee .. hizi dini zenu hizi kweli ni Changa la macho hahaha ..khaaa!!!
Yaani mungu ana saidiwa kupangiwa sheria duuh sasa hapo ukamilifu wake uko wapi !!? Endapo kwamba kuna mambo mengine nyeti anashindwa kuyaongoza mpaka asubiri msaada wa kibinaadamu (mimi nilidhani Kwamba swala la makasisi kutokuoa ni amri ya mungu) sasa kama dini ya mungu imekuwa inafanyiwa marekebisho namna hii kama tafiti za kisayansi jamani jamani kuna haja ya sisi kutoweza kuona kwamba hizi dini zina mushkeri " hebu tuonyeshe kujitambua basiii jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu alishatoa option ya kuoa au kutokuoa, Kanisa la R.C wao wakakazia kutokokuoa ili kuweka uniformity na kufanya hii kazi iwe lifetime personal commitment to God but they where wrong lilitakiwa kuwa suala binafsi. Biblia imeweka wazi anayeweza aoe na asiyeweza aache.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
U
View attachment 623282

Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amependekeza kubadili mfumo wa utumishi wa mapadre akisema itakuwa vyema iwapo makasisi hao wakaruhusiwa kuanza kuoa.

Hata hivyo, imefahamika kuwa pengine pendekezo hilo likawaruhusu mapadre wa Brazil pekee kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo. Hivi karibuni Askofu wa Brazil, Kadinali Claudio Hummes alimwomba Papa Francis kufikiria kuondoa sheria inayowakataza makasisi kufunga ndoa.

Ingawa pendekezo hilo la Papa Francis huenda likapunguza tatizo la uhaba wa wanaume wanaojiunga kwenye utumishi huo, lakini linatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waumini wenye msimamo mkali na hata pia kusababisha mgawanyiko ndani ya kanisa.

Ombi hilo linatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha baraza la kanisa kinachotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil.

Kanisa Katoliki linahubiri mafundisho ambayo yanapiga marufuku makasisi wake kufunga ndoa ingawa kumekuwa na baadhi wanaovunja mwiko huo na kuisha maisha ya ndoa. Hata hivyo, wale wanaochukua uamuzi huo hujitenga na kanisa.

Kasisi moja aliyetambulika kwa jina la Paddy O’Kane amenukuliwa na baadhi ya magazeti akielezea uwezekano wa Papa Francis kuchukua uamuzi wa kuwafungulia mapadre kifungo cha kutokua wakati wowote mwezi huu.

“Hivi karibuni nilimsikia Papa anataka kutekeleza ombi alilolipata toka Brazil kama jaribio lake la kwanza,” alisema.

Papa Francis na mtangulizi wake, Benedict XVI wamekuwa wakieleza kuwa suala la makasisi kutoruhusiwa kuoa siyo jambo lisiloweza kubadilika na kwamba jambo hilo linajadilika.

Chanzo: Mwananchi
Unakuta huyo mwumini mwenye msimamomkali anamwenzi sasa huu si uchoyo jamani
 
Hebu muonyeshe kubadilika basi " Mungu kakuumba kwa mfano wake kwa hiyo wewe na Mungu mnafanana? Mungu na yeye huwa ana kunya ..sieti eehhh !!!?
Mwanadamu ana sehemu tatu; roho, nafsi na mwili; ile sehemu iitwayo roho, inafanana sana na Mungu, maana Mungu naye ni roho; tofauti ni kwamba roho ya mwanadamu ina mwanzo, ya Mungu haina mwanzo; Roho ya Mungu inaweza kuumba, ya mwanadamu haiwezi kuumba; na Roho ya Mungu ina nguvu isiyo na kikomo (Almighty) wakati roho ya binadamu ina nguvu yenye ukomo (limited).

Kwa hiyo ni sawa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu.
 
Kweli maana wamewanyima haki yao ya msingi kwa muda mrefu na wale wa zamani wawalipe fidia kwa kuwatendea unyama
Nani aliyewanyima haki?. Kwa taarifa yako huo Utaratibu Kanisa Katoliki halikujitungia lenyewe, Bali Tangu Kristo, wale Wafuasi wake hawa kuwa na wanawake.Hata akina Petro waliokuwa wameoa hapo mwanzo kabla ya kuwa Mitume walilazimika kuwaacha wake zao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom