Papa afikiria kuruhusu mapadri waoe

Papa afikiria kuruhusu mapadri waoe

Nitajie hayo yanayotarajiwa kubadilika...???

Nyinyi watu hamjui mfumo wa Kanisa.....mnachojua ni Propaganda.....

Mkuu;
Mbona huna nia njema?? Kulitetea kanisa katoliki sio kwa namna hiyo. Tusaidie tiririka hapa huo mfumo na jinsi haiwezekani. Tuliaminisha na Papa Pius X, kuwa Galileo Galilei ameenda motoni milele kwa kusema kuwa dunia ni mviringo. Si unakumbuka kuwa ni Papa Yohane Paulo II, ndiye aliyemfungua Galileo na sasa yupo mbinguni?
Je, haiwezekanihuyu Papa Francis naye akateleza ulimi hadi aje Papa mwingine amfungue?
 
Kweli wewe ni jiwe. Ni kipi sio cha kweli hapo mkuu??
Mkuu Kanisa Katoliki sio kijiwe cha kahawa..!!hiyo taarifa sio ndg kama unavyofkr...!!!

Mtoa mada anasema source Mwananchi..!! Sasa najiuliza hbr nyeti kama hiyo iweje itangazwe chombo kidogo kama Mwananchi peke yake..???au mtoa mada taarifa kaipika chumbani kwake alafu akawamezesha Mwananchi...???

Kwa nijuavyo Kanisa Katoliki(VATICAN) ni Dunia..!!kunapokuwa na taarifa tetanishi kama hii sio chombo kdg kama Mwananchi tuu,ungesikia CNN,BBC,DW,nk.

Pengine cjaweza kuzipata huko vyombo vya hbr vya kimataifa hebu niletee au niambie Mwananchi wamezipata wapi...????sio kwamba nawazarau Mwananchi bali kwa unyeti wa VATICAN na HBR YENYEWE...!

Karibu mkuu...
 
Je, wajua kuwa kuna kikundi kinaitwa American Fathers?? Unajua hawa wameoa?
Daaah!!! Hakuna mapdre anayesema anaushirika na Kanisa Katoliki eti akaruhusiwa kuoa...Hakuna....

Papa Benedict alifanya Kitu kimoja kwa Kanisa la Anglican...(Anglican Ordinarate)...Maana Katoliki na Anglikan hatuna tofauti za Kiliturujua aliruhusu Waanglican waonataka Kurudi Catholic (communion with Pope) warejee catholic bila ya wao kubadili utaratibu wao wa Married Priest na liturujia yenye vionjo vya kianglican....ndiposa ikaitwa Anglo-catholic(Anglican Ordinarate)

Tofauti na hapo hakuna, hakuna , hakuna....tuache uzushi...

Ingekuwa ni kweli sasa hivi dunia ingepamba moto kwa habari hii..si BBC, si Aljazeera, si CNN...kote ingekuwa ni habari ya dunia
 
Hapana, mawazo ya kuoa yamekuwapo from time immemorial! Ndio maana kuwa walutheri, waprotestant walio amua kuoa wakajitenga. Na hawa watajitenga waoe lakini si kuwa ndani ya utumishi wa daraja la upadre na wake!
Msichanganye, kuna mapadre waliioa lakini hao walikuwa wa anglican huko ulaya, walipobariki ushoga wakaamua kutoka na kuja Roma na familia zao na wakakubalika maana walikuwa wamejitoa kumtumikia Mungu. Walikubaliwa na hali zao. Ukitaka mfano nitakupa inbox

Nashukuru kuwa kuna watu wenye ufaham zaidi humu JF. Naomba unisaidie kumpa mifano hiyo Otorong'ong'o.
 
Mkuu;
Mbona huna nia njema?? Kulitetea kanisa katoliki sio kwa namna hiyo. Tusaidie tiririka hapa huo mfumo na jinsi haiwezekani. Tuliaminisha na Papa Pius X, kuwa Galileo Galilei ameenda motoni milele kwa kusema kuwa dunia ni mviringo. Si unakumbuka kuwa ni Papa Yohane Paulo II, ndiye aliyemfungua Galileo na sasa yupo mbinguni?
Je, haiwezekanihuyu Papa Francis naye akateleza ulimi hadi aje Papa mwingine amfungue?
Ndio shida yako..

Atleast ungejua maana ya Doctrine na Dogma au tofauti zake....Halafu ungejua list of all doctrines na dogma za Catholic Church hapo ungejua ugumu uliopo....

Halafu ungekuja kufahamu tu kidogo Canon Laws(Mother of Secular and Religious law)ungejua ugumu..

Celibacy ni doctrine...
 
Hapana, mawazo ya kuoa yamekuwapo from time immemorial! Ndio maana kuwa walutheri, waprotestant walio amua kuoa wakajitenga. Na hawa watajitenga waoe lakini si kuwa ndani ya utumishi wa daraja la upadre na wake!
Msichanganye, kuna mapadre waliioa lakini hao walikuwa wa anglican huko ulaya, walipobariki ushoga wakaamua kutoka na kuja Roma na familia zao na wakakubalika maana walikuwa wamejitoa kumtumikia Mungu. Walikubaliwa na hali zao. Ukitaka mfano nitakupa inbox
Thanks..nimemueleza..

Inaitwa Anglican Ordinarate
 
Nashukuru kuwa kuna watu wenye ufaham zaidi humu JF. Naomba unisaidie kumpa mifano hiyo Otorong'ong'o.
Mifano...mifano anayotaka kukupa ni ya Married Priest wa Anglican walirudi Catholic na Baadhi ya Makanisa ya Mashariki..(Syrian Catholic na Chaldean) ambao wana Communion with Pope ila wameruhusiwa ku-retain utamaduni wao wa Married Priest

Tizama hii
Screenshot_20171104-111252.png
 
Nashukuru kuwa kuna watu wenye ufaham zaidi humu JF. Naomba unisaidie kumpa mifano hiyo Otorong'ong'o.
Nitampa, kuna padre yuko mkoa fulani alikuwa na famila yake pale, mke na watoto. Ndio tukapewa utambulisho huo, maana tulipigwa na butwaa padre kuoa!
 
Daaah!!! Hakuna mapdre anayesema anaushirika na Kanisa Katoliki eti akaruhusiwa kuoa...Hakuna....

Papa Benedict alifanya Kitu kimoja kwa Kanisa la Anglican...(Anglican Ordinarate)...Maana Katoliki na Anglikan hatuna tofauti za Kiliturujua aliruhusu Waanglican waonataka Kurudi Catholic (communion with Pope) warejee catholic bila ya wao kubadili utaratibu wao wa Married Priest na liturujia yenye vionjo vya kianglican....ndiposa ikaitwa Anglo-catholic(Anglican Ordinarate)

Tofauti na hapo hakuna, hakuna , hakuna....tuache uzushi...

Ingekuwa ni kweli sasa hivi dunia ingepamba moto kwa habari hii..si BBC, si Aljazeera, si CNN...kote ingekuwa ni habari ya dunia
Mkuu Otorong'ong'o kuna post yako ilinivunja mbavu 2 mpaka nikalazwa referral hospital kwa matibabu...!!!ngoja niitafute niilete humu.

Alfajiri ya leo kuna mmoja nimeamka nae anajiita Charles177 dk za mwisho nikaambulia matusi,sasa nimemuonesha uongo wake ametokomea kusikojulikana...

Ngoja nitafute ile post yako maana nimeona kama ina ukweli ndani yake....
 
Never on Earth, japo celibacy ktk kanisa sio "funzo imani" bali ni moja kati ya "mashauri makuu ya injili" haliwezi kubadilika kwani ndilo shauli pekee linalomfanya kuhani mkatoliki kuwa "another Christ"..... kuna desturi na mapokeo madogo mno ndani ya kanisa ambayo huenda yasingehitaji hata sinodi ya maaskofu kuyajadili lkn imeshindikana kuyabadili, sembuse hili kubwa namna hii....mashauli mengine ni " utii" na "ufukara", vipi haya nayo hayataanza kuhojiwa kuwa " yanawakandamiza? Kama tutakuwa hai tutaona, I know my church.....
 
Natural selection..haijawai kumuacha mtu salama
 
Ndio maana mkuu nikasema; Najua kuwa wewe ni mkatoliki mzuri tuu. Haya unayajua ila nadhani hii fununu ilitokea kwake pia baada ya kutembelea Amerika ya kusini. Je, wajua kuwa kuna kikundi kinaitwa American Fathers?? Unajua hawa wameoa?
Hakuna Kaasisi mwenye ushirika na Kanisa Katoliki anaweza kuoa akiwa ndani ya Kanisa...

Huu ni uongo wa hali ya juu...!!!
 
Nitampa, kuna padre yuko mkoa fulani alikuwa na famila yake pale, mke na watoto. Ndio tukapewa utambulisho huo, maana tulipigwa na butwaa padre kuoa!
Hilo unalolisema binafsi siwezi kulipinga au kulikubali...!!!

Maana kama Padri ameamua kumiliki familia kwa siri kinyume na Sheria za Kanisa,Ushauri wangu kwako hebu matafute Askofu au kiongozi yeyote wa Kanisa alafu umshirikishe ila uwe na ushahidi wa kutosha sio Guessing maana Kanisa Katoliki limepitia misukosuko mingi sana toka kuanzishwa kwake na Yesu Kristo mwenyewe.
 
Hujaelewa, sikiliza. Huyu alikuwa Padre wa anglican UK, walipobariki ushoga akasema siwezi kutumikia kanisa lililobariki ushoga. akaomba kwa Pope aje atumikie Mungu kama padre katika kanisa katoliki. walikubalika kuwa mapadre kama walivyo, kwa kigezo hicho tu. ndiyo akaamua kuja Tanzania kufanya uinjilisti.
 
Hiyo mbona ndio naisikia tena na sidhani kama kutakuwa na ukweli ndani yake...!!!

Kwa misingi ya Kanisa Takatifu Katoliki la Mitume utoke kwenye kanisa la Anglican kama Padre alafu uje Katoliki upewe nafasi ileile uliyotoka nayo Anglican....!!!!!

Otorong'ong'o hebu nisaidie hili huyu jamaa naona wameamua kutidanganya kama EGW alivyowadanganya..
 
Sasa wewe kumbe mbishi tu! Nina haja gani kuja hapa kusema uongo. alikuwa padre wetu parokiani, unabisha tu! si vema kuwataja watu humu, ningelikutajia uende utamkuta anatumikia wakatoliki
 
Sasa wewe kumbe mbishi tu! Nina haja gani kuja hapa kusema uongo. alikuwa padre wetu parokiani, unabisha tu!
Akitokea Anglican kama Padre alafu aje Katoliki ape Upadre aliokuwa nao Anglican...???

Mmh me ndio naisikia Leo..

Ngoja Otorong'ong'o amalizie lunch akujibu me ngoja nimalizie kazi nikajiandae kwenda ibada ya siku ya Dominica.
 
Back
Top Bottom