Papa afikiria kuruhusu mapadri waoe

Papa afikiria kuruhusu mapadri waoe

Ukipewa andiko la Biblia,tafadhali naomba unitag. Ni mambo waliyojiwekea RC wenyewe,lakini Biblia haina kitu hicho.
Tatizo wanaamini kila wanaloambiwa hawa na viongozi wao. Hao wazungu walijiwekea tu sheria zao huko wakati wanaanzisha hilo.kanisa na wanaujua ukwelo tofauti na hawa wa huku wanaopelekwa pelekwa na ndio maana wameona kuna umuhimu wa kubadilo hii kitu sababu wanajua hata wao hawafanyi dhambi wakibadilo sababu wanajua tangu mwanzo HAKUNA SEHEMU MUNGU ALIKATAA NA NI SHERIA TU ZA KANISA LAO NA NDIO MAANA HATA PAPA KAONA KUNA NAFASI YA KUJADILI.
TATIZO RC KANISA(KATEKISTA) KWANZA THEN BIBLIA.
 
vitu vingine ufaham unatosha,
Mungu muumba karuhusu zaeni mkaijaze dunia, mwanadam aliye na miguu miwili azuie na afikilie kuruhusu?? how come
 
Hakuna jambo ambalo halina faida! Pamoja na kwamba si agizo la kibiblia kuoa au kutooa bali ni utashi wa mtu mwenyewe katika kuitawala tamaa ya mwili! Aliyeweka utaratibu huu alilenga hasa kutengeneza kanisa kama taasisi yaani kumwondolea mtumishi mambo yanayoweza kumpelekea kuwa na tamaa hasa za mali, kwa mfano huwezi mwambia mtu mwenye familia kwamba sadaka hii ni ya Kanisa wakati ana watoto na mke wanaodai matumizi. Pili ili hawa watu waishi pamoja kama ndugu lazima wasiwe na familia au umiliki wa Mali bali ukiruhusu kimoja lazime na kingine ukiruhusu( Mali na familia), ili limesaidia katika kulinda kanisa kwa mihongo mingi sana tangu kuanzishwa kwake. Unaweza fanya utafiti kidogo kuhusu utitiri wa Makanisa ya kileo, sababu kubwa ya mmeguko huu ni kutafuta mali lakini si kulifundisha neno maana hata huko huyo nabii au mchungaji alikotoka wanafundisha neno hilo hilo na haya yanachangiwa na watumishi kuwa na wategemezi ambapo akikaa chini ya Kiongozi flani hawezi ishi katika ukwasi anaotaraji. Hivyo basi ili Papa abadili utaratibu wa utumishi wa mapadre inabidi abadili pia mfumo wa uendeshaji wa kanisa yaani Kanisa lisiwe taasisi bali liendeshwe kama makanisa yakilokole au Lutheran ambapo Padre atakuwa na utaratibu na Mamlaka kamili ya kuendesha Kanisa katika eneo lake kama utashi wake utakavyokuwa. Athari ya hili ni kumeguka kwa Kanisa katika kiwango kisichotegemewa utaanza kusikia kanisa la Padre flani flani.
Lutheran ni TAASISI.
AND WHY NYIE WATU MNAJALI ZAIDI KANISA TAASISI ZAIDI YA BIBLIA NENO LA MUNGU
 
Acha uongo mkuu...unadanganya ili iweje...


Orthodox Church au Eastern Church lilijitenga na Kanisa Katoliki (Western Church)kanre ya 11....Kabla ya hapo Kanisa lilikuwa moja tuu..yaani Katoliki..

Na hiyo ndio schism ya kwanza kabisa ndipo ikafuatiwa na ile ya Martin Luther
Yaani nyie manvyolishwa basi hata kipindi cha Yesu kulikuwa na UKATOLIKI
 
"Enendeni mkaijaze dunia"- andiko liko wazi

Hili suala la kutooa siyo amri ya Mungu, ni sheria tu ya mwanadamu. Watu wanaacha kumsikiliza Mungu wanamsikiliza Paulo, matokeo yake ndiyo haya!
 
Hii itapitishwa, baada ya miaka kadhaa itakuja ya mashoga, kataeni kubalini, dini ni yao wazungu, sisi kupelekeshwa tu, tulio wakristu tunawa admire wenzetu waislamu, wao sheria msumeno, hakuna cha kwenda na wakati wala nini...
 
Yaani nyie manvyolishwa basi hata kipindi cha Yesu kulikuwa na UKATOLIKI
Sio Kulishwa...Kanisa Katoliki limeanzishwa na Yesu Kristo mwenyewe chini cha Mwamba Petro ambaye ni Baba Mtakatifu wa kwanza..


BTW: turudi hapo uliponi-quote...ulitaka kusemaje kuhusu Orthodox Church (Eastern) na Catholic Church(Western)..?
 
Hii itapitishwa, baada ya miaka kadhaa itakuja ya mashoga, kataeni kubalini, dini ni yao wazungu, sisi kupelekeshwa tu, tulio wakristu tunawa admire wenzetu waislamu, wao sheria msumeno, hakuna cha kwenda na wakati wala nini...
Hakuna kitu kama hicho...hizi story za mitandaoni zinaletwa makusudi kupima upepo...

Kubadili doctrine sio kazi Rahisi kama unavyofikiri(Papa hawezi)...Itahitajika kuwe na mitaguso kadhaa....watu wadebate....Canon law lazima zibadilishwe..

Ni ngumu, ni ngumu....haiwezekani...

Na kwaarifa yako Strongness ya Kanisa Katoliki mpaka leo hii(Yani nguvu ile ile toka Yesu alipolianzisha) inatokana na Priest Celibacy...

Ukitaka kuona Kanisa linasambaratika basi ruhusu mapadre kuoa....
 
Hiv kunawatu bado wanaamini katka hii dini ya kisanii?papa amevaa joho la Mungu.

Kwahiyo ataipinga Bible
 
Hiv kunawatu bado wanaamini katka hii dini ya kisanii?papa amevaa joho la Mungu.

Kwahiyo ataipinga Bible
Joho la Mungu lipoje....umeshawahi kuliona..?? Au aliwai kukuonesha...??

Hizi akili hizi..(Kama si za kisabato basi za kiislamu)
 
Siungi mkono kabisa hoja hyo,,,,maan altare n sehem takatifu xo huwez kwenda sehem takatifu huku umezini banaaa
 
Aisee waoe tu ila nawaonea huruma sana wana parokia na makanisa yao.Maana sasa watalisha familia ya padri,wakwe zake na ndugu wengine watajazana pale.
Hahaha hata mimi ntakuwa padri kama wataruhusu kuoa
 
Papa hapa umenikuna fanya fasta.Nimechoka kuishi kinafiki mbele ya mungu.Mimi ni padre lakini nina watoto wa nje moyoni naumia maana naona kama natenda dhambi.Ila ukiamua hivi pia fanya kwa watawa ngoma iwe dro.Nimechoka kuwa mtu wa mapokeo ila imani yangu kwa dhehebu langu iko pale pale.Hakuna mahali pameandikwa mapadre wasioe na ikumbukwe zamani kuna papa alioa nani alikuja badili hili?.
 
Back
Top Bottom