Pamoja na tozo kila kona, Serikali imesitisha mradi wa Barabara ya Kimara-Kibaha?

Watanzania wanataka maendeleo. Kama kuna wanaofikiria kuoiga deals waangalie mara mbili mbili. Ipo siku watadaiwa tu
 
Hadi mwezi July Barabara ya Kimara-Kibaha ilikuwa imefika karibu asilimia 98 na ukiangalia kwa macho ni barabara ambayo ilikuwa imalizike mwezi wa nane kabisa kama walivyokuwa wamepanga maana kwa kuangalia ni kipande kidogo cha kiluvya -kibaha upande mmoja ndiyo ilikuwa haijawekewa tabaka la mwisho la lami.

Lakini cha kushangaza barabara hii toka mwezi wa saba mwishoni imesimama na ni wazi kabisa thamani ya mradi huu itazidi kuongezeka na itapelekea serikali kupata hasara zaidi na itatakiwa kulipa zaidi mkandarasi.

Wengi wanajiuliza maswali mengi inakuwaje pamoja na matozo yote kwanini barabara hii kwa kipande ambacho hakifiki kilomita moja serikali imeshindwa kukimalizia haraka?

Serikali inatengeneza mwanya wa kupiga hela kwa kusimamisha miradi halafu kuiiibua baadae wakati thamani yake ikiwa juu zaidi.

Nini kimeifanya serikali kusitisha mradi huu uliokuwa umefika mwisho kabisa?

Kuna shida gani pamoja na matozo?
Tunamalizia utalii kwanza mpaka tuyakue maeneo yote mazuri mazuri. Bado serengeti.
 
Hii barabara walaanza 2018/2019 na mpaka leo haijakamilika. Ni kipande kidogo sana.

Kati ya tatizo ambalo linaigharimu nchi hii pesa nyingi ni hizi kazi zisizoisha, miradi isiyokamilika, kazi za kujirudia rudia.
 
Tatizo kubwa sana hilo,na je serikali umetoa ufafanuzi ucheleweshaji huo??
 
Kuna ile ya makongo juu mwaka wa tano sasa hakieleweki kinachofanyika hapo.....na ina chini ya kilometa mbili.....hii tozonia wee acha tu!
 
Ukiona barabara au mradi wa ujenzi umesimama ujue ni tatizo la muda mrefu mara nyingi huwa ni kutokulipa mkandarasi au kushindwa kwa makandarasi kufanya alichotakiwa kufanya (termination by Employer). Je mkandarasi ameondoka site? Au unataarifa za ndani zinakuhakikishia kusimama kwa mradi? tuwe waangalifu kuandika taarifa zisizo na uhakika.
Kipande cha SGR cha Dar-Moro tuliambiwa kingekamilika na kuanza kazi mwishoni mwa 2019, leo hii 2021 hakuna kinachoeleweka......watu wakiongea mnaleta utetezi usio na kichwa wala miguu...
 
Wanaupiga mwingi ndugu, ndio kwaanza wanarekodi sinema huko mikoani, nchi hii ina matatizo makubwa sana
 
Maeneo yasije kuwekwa sokoni tu yakaibuka yale ya loliondo.......maana kwa jinsi ninavyomjua beberu anaijua ngorongoro na serengeti mara mia zaidi ya masai na mang'ati wanaokaa pale, hivyo huna haja ya kumtangazia....
 
Back
Top Bottom