Leak
JF-Expert Member
- Feb 22, 2012
- 52,206
- 42,068
Hadi mwezi July Barabara ya Kimara-Kibaha ilikuwa imefika karibu asilimia 98 na ukiangalia kwa macho ni barabara ambayo ilikuwa imalizike mwezi wa nane kabisa kama walivyokuwa wamepanga maana kwa kuangalia ni kipande kidogo cha kiluvya -kibaha upande mmoja ndiyo ilikuwa haijawekewa tabaka la mwisho la lami.
Lakini cha kushangaza barabara hii toka mwezi wa saba mwishoni imesimama na ni wazi kabisa thamani ya mradi huu itazidi kuongezeka na itapelekea serikali kupata hasara zaidi na itatakiwa kulipa zaidi mkandarasi.
Wengi wanajiuliza maswali mengi inakuwaje pamoja na matozo yote kwanini barabara hii kwa kipande ambacho hakifiki kilomita moja serikali imeshindwa kukimalizia haraka?
Serikali inatengeneza mwanya wa kupiga hela kwa kusimamisha miradi halafu kuiiibua baadae wakati thamani yake ikiwa juu zaidi.
Nini kimeifanya serikali kusitisha mradi huu uliokuwa umefika mwisho kabisa?
Kuna shida gani pamoja na matozo?