Kamati ya Bunge yaishauri Serikali kuanzisha Barabara za kulipia tozo

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,982
49,650
Kamatia ya Bunge ya Miundombinu imeishauri Serikali kuona umuhimu wa kuanzisha na kujenga Barabara za Kulipia Tozo Ili kuweza kuongeza mapato.

Kamatia imetaka Barabara ya Kimara Hadi Kibaha ndio iwe ya kwanza kuingizwa kwenye mfumo huo.

My Take: Safi sana Kamatia,ifike mahala tuepukane na mifumo ya kijima inachelewesha maendelea sana.

=============

SERIKALI YASHAURIWA UMUHIMU WA KUANZISHA BARABARA ZA KULIPIA TOZO

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu yaishauri Serikali kupitia Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuanza na mfumo wa barabara zenye tozo katika mradi wa ujenzi wa barabara njia nane kutoka Kimara Jijini Dar es Salaam hadi Kibaha mkoa wa Pwani ili kuweza kuongeza mapato.

Ushauri huo umetolewa wakati Kamati hiyo ilipofanya ziara kutembelea mradi wa barabara wa njia nane ambapo waliongozana na viongozi na watumishi kutoka Wakala wa barabara Tanzania (TANROADS) kuona maendeleo ya mradi huo ulipofikia pamoja na kuona changamoto zilizopo.

Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kuduma ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Selemani Kakoso amesema duniani kote, barabara nyingi zinajengwa kwa mfumo kama wetu ambao ulishaanza muda mrefu na sheria inatukataza huwezi kuwa na barabara ya tozo kama huna njia nyingine mbadala.

Aidha amesema katika mradi wa barabara kunatakiwa pia kuimarishwa kwa mifumo ya mifereji kwaajili ya majitaka kwani mvua zinaponyesha maji yanashindwa kwenda kwenye maeneo husika na kuleta kero kwa watumiaji wa barabara.

Pamoja na hayo Kamati hiyo imeridhishwa na miundombinu inayojengwa katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuipongeza Wizara kwa usmamizi mzuri ambao wanaufanya kupitia TANROADS kujenga miundombinu ya barabara nchini.

"Tumeiona dhamira ya Serikali kupunguza msongamano ambao wanaamini utarahisisha shughuli nzima kwenye sekta ya uchukuzi". Amesema Mhe.Kakoso.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi mhandisi Godfrey Kasekenya amesema kumekuwa na ongezeko la gharama kubwa kwenye ujenzi wa miundombinu kutoka kwenye gharama ya mwanzo mpaka mradi unapokaribia kuisha gharama zinaongezeka kutokana na usanifu wa ujenzi wa miundombinu mipya.

Nae Mtendaji Mkuu wa TANROADS Mhandisi Rogatus Mativila amesema mradi huo uliogharimu shilingi za kitanzania bilioni 218 umejengwa na Mkandarasi mzawa kutoka kampuni ya ESTIM CONSTRUCTION umefikia asilimia 98 na unatarajia kukamilika mwezi ujao.

Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
 
Duuh hii nchi mbona inaongozwa na watu wajinga sana? Yaani wao hawaoni kuna vitu vya muhimu sana hawajafanya wanang'ang'ania tozo tu kila siku?
 
Labda zile Lane mbili za mwendokasi ndio wazofanye za kulipia, otherwise watakuwa wamebugi sana. Morogoro road ndio lango la jiji, unailipisha vipi barabara nzima wakati watu wote(wenye nazo na wasio nazo) wanahitaji kupita hapo?
 
Best option wangeongeza hata sh 10 kwenye Lita ya petrol/diesel na hiyo pesa iende kwenye mfuko maalum wa bara bara . Shida iliyopo kwa serikali ya Tanzania ni kutoheshimu matumizi ya fedha za kwenye mifuko husika, Rais akitoa amri ya kutaka pesa toka mfuko fulani basi zitatolewa tu.
 
Sio kwamba wewe ndio Mjinga? Unajua modality ya concept ya toll roads? Acha kuropoka hovyo wewe mbumbumbu.
Mnabuni miradi yenu ya kijinga jinga ili muendelee kuumiza wananchi? eti kamati ya bunge yan mmejazana vichwa panzi tupu kwenye hiyo mnaita kamati ya bunge, taifa linanuka umasikini kwa sababu linaendeshwa na nyinyi wehu yan huko serikalini mmejazana wezi hamnazo mnashindwa kutatua matatizo miaka nenda rudi alafu leo mnaibuka na idea za ki.fala kuendelea kuumiza raia.
 
Labda zile Lane mbili za mwendokasi ndio wazofanye za kulipia, otherwise watakuwa wamebugi sana. Morogoro road ndio lango la jiji, unailipisha vipi barabara nzima wakati watu wote(wenye nazo na wasio nazo) wanahitaji kupita hapo?
Kuna Barabara 8 lane za kulipia zitatengwa na za nyie maskini zitakuwepo.
 
pmbavu ccm wewe, mnabuni miradi yenu ya kijinga jinga ili muendelee kuumiza wananchi? eti kamati ya bunge yan mmejazana vichwa panzi tupu kwenye hiyo mnaita kamati ya bunge, taifa linanuka umasikini kwa sababu linaendeshwa na nyinyi wehu yan huko serikalini mmejazana wezi hamnazo mnashindwa kutatua matatizo miaka nenda rudi alafu leo mnaibuka na idea za ki.fala kuendelea kuumiza raia.
Duu nyumbu mbona una makasiriko? Toll roads is all over the world Sasa wewe ni mshamba hujui kitu Tulia uletewe maendelea kenge wewe.
 
Back
Top Bottom