Pamoja na suala la Katiba Mpya, Halmashauri ya CCM ilipaswa kujadili hujuma dhidi ya mradi wa JNHP, bei za mbolea na mafuta ili waliohusika wakamatwe

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,086
6,568
Ninashangaa sana kusikia eti katiba mpya imekuwa ina umuhimu sasa hivi wakati kuna kikosi kazi kilisema mpaka mama akishinda uchaguzi wa 2025 ndio mchakato uanze.

Sio mbaya maana sasa ni hitaji la kitaifa na mchakato uanze mapema, lakini kwa nini CCM wabadili gea?

Mbona masuala ya msingi kama hujuma dhidi ya mradi wa JNHP, kupanda bei mafuta na mbolea hayajadiliwa na ilihali yanaleta dhahama kwa wananchi.

Huu mradi wa JNHP ni muhimu sana kwa maisha ya wananchi. Mbolea imekuwa ni kikwazo maana nchi jirani ni bei rahisi tofauti na hapa nchini. Mafuta nayo ni songombingo maana kuna namna za watu humo kama inavyosadikika. Kwa nini hawayajadili haya?
 
Hivi kuna kitu muhimu Kwa nchi yoyote kuzidi Katiba? Au mwenzetu unasombwa na akili za kina Mkama wanàosema watu hawali Katiba? Na kama hawali Katiba ndo wanakula mabwawa Sasa?
 
Hivi kuna kitu muhimu Kwa nchi yoyote kuzidi Katiba? Au mwenzetu unasombwa na akili za kina Mkama wanàosema watu hawali Katiba? Na kama hawali Katiba ndo wanakula mabwawa Sasa?
Tumia akili, kama huna akili azima za wengine
 
Bei ya mbolea ni muhimu hatua stahiki zikachukuliwa.

Wananchi wanashindwa kulima kutokana na bei ya Mbolea kuwa juu.

CCM originally ni chama cha wakulima na wafanyakazi hivyo kujali mustakabali wa wakulima ni sahihi.
 
Hoja lazima ianzie chadema (think tank) ndo CCM izinduke. Hata hilo la bwawa lazima lianzishwe na chadema la sivyo huko kwingine ni bendera fuata upepo. Ulitaka historia angalia chanzo cha elimu bure na sasa katiba mpya.
 
Nasikia vikwazo vya chakula na mbolea vimeondolewa Urusi. Why wasiende kuchukua mbolea kule na ni bei rahisi mno, yani mbolea bongo bei kubwa mno wakati Urusi bei ya kutupa inasikitisha sana! Ingesaidia sana mana Uchumi wetu unategemea sana kilimo, siku hiz watu hawalimi sana kisa mbolea imepanda. Aliyeturoga waAfrica alaaniwe!
 
CCM huwa inaendeshwa na Chadema. Ukitakaka ccm waanze kujadili bei za bidhaa na bwawa la Nyerere subiri chadema waanze kujadili kwanza .

Si unaona suala la katiba mpya?
 
Nasikia vikwazo vya chakula na mbolea vimeondolewa Urusi. Why wasiende kuchukua mbolea kule na ni bei rahisi mno, yani mbolea bongo bei kubwa mno wakati Urusi bei ya kutupa inasikitisha sana! Ingesaidia sana mana Uchumi wetu unategemea sana kilimo, siku hiz watu hawalimi sana kisa mbolea imepanda. Aliyeturoga waAfrica alaaniwe!
Umaskini mbaya mkuu, ukifanya biashara na Urusi unawekewa vikwazo, misaada na mikopo ndio basi tena,
Utapata mbolea na mafuta, utakosa mikopo na misaada ya kibajeti,

Tuna raslimali tumeshindwa kuzitumia vizuri sasa huu ugumu wa maisha watu wataamka na kujiuliza tumefikaje hapa,

Shida zitawaunganisha watu na kuacha kushabikia ujinga wa vyama vya siasa,

Mwisho wote waliotufikisha ktk hali hiyo watajulikana na hatua stahiki zitachikuliwa hata kama itapita miaka mingi,
 
Back
Top Bottom