Pamoja na mishahara ya sasa ilivyo bado walimu waliishi maisha mazuri zamani kuliko sasa

Hofu-less

JF-Expert Member
May 19, 2014
524
1,044
Kwa bahati babu, bibi, baba na mama yangu wote walikuwa ni walimu, na mimi mwenyewe nikafuata nyayo kwa miaka 10 kabla sijakimbia nilichoona kipindi kile cha zamani.

1. Makazi/Nyumba za walimu zilikuwepo, walimu walikaa kwenye maeneo ya shule na hata kama hakukuwa na nyumba basi kijiji au serikali ya mtaa ilihakikisha walimu wanapata sehemu ya kujihifadhi bila kulipa! Sasa hivi mwalimu atajua yeye akae wapi, suala moja tu anatakiwa afike kazini kwa wakati, na mshahara wake huo ndiyo alipe Kodi!

2. Posho ya kufundishia hii iliwekuwepo enzi za Mwinyi na ilisaidia sana!

3. Mshahara walimu walilipwa dirishani/mkononi na hivyo kuepuka Kodi na Tozo,
kwasasa sina haja ya kuelezea kinachoendelea.

4. Kupewa kipaumbele na heshima, zamani walimu waliheshimiwa. Kazi kama hizi za sensa, uchaguzi n.k walimu walipewa kipaumbele kwanza lakini sasa hivi ndivyo sivyo, ubabe ubabe.

Kwa sasa mshahara wa mwalimu huo huo alipe Kodi, huo huo alipe nauli, huo huo anunue chakula, hata kama akilipwa milioni mbili hawezi kutoboa.

Ndiyo maana wabunge wana mishahara lakini wana posho, na posho za mafuta! Serikali ingeweza kuanza na suala la nyumba za walimu kwanza kwa Tozo hizi. Ndani ya miaka miwili tu walimu wanaweza kuondoka na kero ya nyumba za kupanga.
 
Wajiongeze wafanye Kazi za ziada vijijini kufanikiwa ni rahisi
 
Back
Top Bottom