WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI
ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako
UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani
Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?
Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?
Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia...