Padri Kitima: Unafiki na kusifia kila jambo ili kupata vyeo kutaliua Taifa

Unafiki unaanza kwao
Akija wa kuwashikisha adsbu wanafunga midomo
Waendelee kuhubiri ya Mungu haya ya unafiki ni kila sehemu yapo na akija mbabe wanaufyata tena
Viongozi wa dini wanastahili kusimama katika, kukemea uovu wote, kutetea haki za wanaodhulumiwa. Wanatakiwa kuyafanya yote bila woga. Huo ni wajibu wao wa kiimani.

Kazi kubwa ya Padre ni kuendeleza kazi aliyoianzisha Kristo: Kristo ni:

Ni kiongozi mkuu
Ni mwalimu
Ni kuhani
Ni mpatanishi
Ni mtetezi
Ni mlinzi
Ni sadaka
Ni mwokozi

Katika haya, Padre hutakiwa kusimama imara bila kuyumba.
 
Padri yupo sahihi...lakini kwa nini hakutuyasikia haya kipindi cha JPM,ilifika hatua hadi anapewa mic kanisani ahutubie.....huku wakina Pengo wakimtaka Makonda awe raisi wa awamu ya Sita.
Ni kweli Padri Kitima yupo sahihi,"Unafiki wa kisiasa unaondelea miongoni mwa watanzania,utaliangamiza taifa"

..hawakumgusa Jpm kwasababu ya kuogopa kupotezwa au kuuwawa.

..Ssh akitaka kuheshimiwa sawa na mtangulizi wake aanze kwa kumlipua mwanaharakati mmoja. Wengine wote watakaa kimya.
 
Yeye na Kanisa lake pia ni Wanafiki. Wakati wa Mwendazake ambaye ndiye mwanzilishi wa hii tabia hawakudiliki kusema kitu. Sana sana walimsifia.

Kwenye hili siliungi mkono Kanisa.

Ukweli unabaki ukweli! Kama huliungi kanisa mkono ni sawa umetumia haki yako ya msingi!

Wakati wa mwendazake, wako viongozi wa kanisa waliendelea kukemea serikali akiwemo Bagonza, Niwemugizi, Kitima, Emmaus Mwamakula na wengine! Wako vile vile waliotishwa na vishindo vile wakafyata mkia, na wako wanafiki pia!

Suala la Kusifia sifia liko pia ndani ya viongozi wa kanisa, haliko serikalini tu! Kwa hiyo statement ya Fr. Kitima inakata pande zote.
 
Viongozi wa dini wanastahili kusimama katika, kukemea uovu wote, kutetea haki za wanaodhulumiwa. Wanatakiwa kuyafanya yote bila woga. Huo ni wajibu wao wa kiimani.

Kazi kubwa ya Padre ni kuendeleza kazi aliyoianzisha Kristo: Kristo ni:

Ni kiongozi mkuu
Ni mwalimu
Ni kuhani
Ni mpatanishi
Ni mtetezi
Ni mlinzi
Ni sadaka
Ni mwokozi

Katika haya, Padre hutakiwa kusimama imara bila kuyumba.
Well said
Na wasimamie haki kila wakati na wakemee dhulma kila wakati tena kwa kumsontea mtu kidole awe police, mbunge, waziri na hata watu wa kawaida na hata kama kuna Gazeti linapotosha au kuegamia upande mmoja basi wakemee

Huo ni wajibu wao ila wengi hawakumbuki wajibu wao aidha ni tamaa za Dunia au woga
 
Naona masheh wameamua Rasmi kupambana na warumi!!!

Vuguvugu lilianza pale masheh walipoamua kuwaaachia masheh waliotuhumiwa kwa ugaidi!!

Juzi mmoja kasema wazi Kuwa mapadri zaidi ya hamsini wameuawa Lakini VYOMBO vya habari havitangazi!

Leo kuna kesi kadhaa za ulawiti!!

Samiah mama YANGU nakuonya !!!Acha kupambana na Hawa WATU!we Tulia coz waliyemuamini akapewa kutawala aliharibu Sana!wanamaumivu walipoteza utawala pale mtu wao alipo itwa na MUNGU!Wana uchungu Sana!!!

Wakiamua huwezi washinda can masheh BADO hawajatengeneza Taasisi imara ya kutawala Dunia kama wao!!

"Rasimu ya Warioba irudi mezani SASA iwe katiba mpya"
Kama umesahau, huyu kitima wakati magufuli akiwa madarakani alisema uchaguzi wa term yake ya pili ulikuwa ni uchafuzi si uchaguzi timamu
 
..Kitima akisisitiza haki sawa kwa vyama vyote wakati wa utawala wa Jpm.

Kwa sasa maadili ya kiimani yametoweka kwa dini zote.

Wakristu na waislam wote hawana tena huo utumishi wa kiimani.

Kila siku utasikia padre kawabaka waumini wake na kesho utasikia shehe kawarawiti wanachuo wake.
Wakumbuke hata Yuda Ishariote licha ya kuteuliwa ya YESU mwenyewe, alienda kinyume na maadili kwa kushawishiwa na mwovu.
 
..hawakumgusa Jpm kwasababu ya kuogopa kupotezwa au kuuwawa.

..Maza akitaka kuheshimiwa sawa na mtangulizi wake aanze kwa kumlipua mwanaharakati mmoja. Wengine wote watakaa kimya.

" Katibu mkuu wa Balaza la maskofu Tanzania (TEC) amemuonya Rais Magufuli na CCM kwa namna wanavyoviminya vyama vingine vya siasa, na kuwataka watu wasikae kimya watoke na wakemee haya matendo yanayoligawa Taifa." Video naoma mods waliitoa.

Link nyingine

Unafiki umeanza kwa viongozi wa dini hao ndio wanafiki namba 1 wakati wa nyakati ngumu nao waligeuka bebdera kufuata upepo sasahivi nao wanainua mabega kujifanya wanakemea unafiki wakati wao ndio waliobeba bendera ya unafiki aache upuuzi asijifanye hayo anayaona leo yeye aendelee kukusanya sadaka na waendelee kuzitumia tu
 
Padri yupo sahihi...lakini kwa nini hakutuyasikia haya kipindi cha JPM,ilifika hatua hadi anapewa mic kanisani ahutubie.....huku wakina Pengo wakimtaka Makonda awe raisi wa awamu ya Sita.
Ni kweli Padri Kitima yupo sahihi,"Unafiki wa kisiasa unaondelea miongoni mwa watanzania,utaliangamiza taifa"
Yaani kitima kimechelewa mnooo,

Kwanini kipindi hiki,tena kipindi kile ndo kusifu kulipamba moto.Sisi watu wa Jf tulishakemea sana.Labda tumshauri apitie nyuzi zetu humu ili ajifunze kwetu!!
 
Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.
Na.kuhusu huyu unasemaje?
 
Ukweli unabaki ukweli! Kama huliungi kanisa mkono ni sawa umetumia haki yako ya msingi!

Wakati wa mwendazake, wako viongozi wa kanisa waliendelea kukemea serikali akiwemo Bagonza, Niwemugizi, Kitima, Emmaus Mwamakula na wengine! Wako vile vile waliotishwa na vishindo vile wakafyata mkia, na wako wanafiki pia!

Suala la Kusifia sifia liko pia ndani ya viongozi wa kanisa, haliko serikalini tu! Kwa hiyo statement ya Fr. Kitima inakata pande zote.
Nipe mfano wa Kanisa Katoliki.
 
Mimi Ni mkristo lkn hii trend ya akiingia rais Muislam then RC na madhehebu mengine ya kikristo kujifanya yanamuwashia Moto sio fair.Enzi za JPM walitulia kimya na ujinga wote ule aliokua anafanya.

Pamoja na yote niliyosema lkn ujumbe wa Kitima Ni Valid.
Nakazia mkuu,,,,nashukuru umeliona hilo
 
Back
Top Bottom