chameli
Senior Member
- Jul 23, 2011
- 132
- 58
Niliwahi kusikia kipindi kimoja kwenye runinga kuhusu historia ya mtume muhamad ya kuwa kipindi chake cha kueneza dini alitafutwa na maadui zake ili auwawe kwa kujiepusha alikimbilia ethiopia wakati huo na ilikuwa nchi inayoongozwa na wakristo,je kama wakristo ni makafiri,mtume alifata nini ethiopia,sidhani kama haya ni maagizo ya mtume bali haya sio maagizo ya mtume bali wanachokifanya sasa ni tofauti na kile alichoagiza mtume,kwa sasa hadi watoto tunawafundisha kuwa wakristo ni makafiri,je tunawalea katika misingi ipi watoto wetu kama sio ya chuki na uuaji.
Nasikia kafiri maana yake ni mtu asiye na dini.watakuwa wanachanganya kama kubeep na kudipu