Pacha wangu hataki kuondoka nyumbani

Pacha wangu hataki kuondoka nyumbani

Nasiche

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2019
Posts
291
Reaction score
735
Kichwa cha habari hapo juu cha husika

Mimi ni pacha ke na me. Katika udada wangu kitu sipendi ni kudate mtu ambaye anaishi kwao, Kama niliwahi basi niwakati Nikiwa sekondari Kama sijasahau

Sasa pacha wangu ni mkubwa tu kamaliza Chuo yapata miaka mitano Kama siyo sita imepita akapata kibarua kwenye NG'O alivyopata tu akukaa sana akaenda Kupanga geto Kama miaka miwili hivi sijui ilikuwaje mwaka Jana akarudi home anatoka nyumbani anaenda kazini, vitu vyote akauza friji, TV, kitanda pasi na Kila kitu.

Ukimuuliza anasema alipunguza gharama za maisha Mana mama anamtegemea(kumbuka anakaka zake na dada wengine plus Mimi ) na yeye kulipa kodi anaona Bora akae tu nyumbani. Je, kiuanaume hii Ni sawa mtu wa miaka 30 kukaa kwao?

Wapendwa nisaidieni kumshauri nimemwimbia Sana nimechoka, Kila mtakachonishauri nitamweleza kinaga ubaga Ili angalau abadilike.
 
Pole sana best kiujumla sio sawa kwa kijana wa umri wake kukaa nyumbani mpaka leo, labda kuwe kunasababu maalumu labda wazazi hawapo wote na kunawadogo wanao taka uangalizi wa karibu hapo labda itawezekana.

Naamini yeye anapashwaa kuanzisha mji wake kwaajili ya ustawi wa familia yake atakayo ianzisha.
 
Pole sana best kiujumla sio sawa kwa kijana wa umri wake kukaa nyumbani mpaka leo, labda kuwe kunasababu maalumu labda wazazi hawapo wote na kunawadogo wanao taka uangalizi wa karibu hapo labda itawezekana.
Naamini yy anapashwaa kuanzisha mji wake kwaajili ya ustawi wa familia yake atakayo ianzisha.
Kabisa
 
Muda mwingi tunadhani maisha tunayotaka ndugu zetu wawe nayo ndiyo wayawazao.

Kuna muda unatamani kaka/dada yako awe hivi...lakini haiwezekani nao wana picha ya maisha wayatakayo.
Kweli inaniuma Sana

Pia ana mpenzi wake ambaye ndo wifi yangu ananilalamikia Sana ,hawajaoana Ila ndo hivyo Hana uhuru Naye anavyoniambia Kama ujuavyo home Kuna sheriia lazima awahi kurudi wifi ana mind anaomba nimshauri akapange so hata Mimi Nikiwa na mtu wa hivi siwezi ndo Mana naumia
 
Unajuaje kama ndiyo njia anayotumia kumwacha mchumba!

Kama mimi ningemwacha aishi maisha yake.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom