Ukijaribu kufuatilia sana diplomasia ya Marekani utapata wazimu, juzi wamedai wamemuua Osama, wanayemwelezea kuwa alikuwa mtu "hatari," leo nasoma kwenye gazeti la Mwananchi kuwa Marekani "inafikiri" kuwa Al-Zawahiri ndiye atakuwa mrithi wa Osama, kwa jinsi walivyomwelezea huyo jamaa ninanukuu Gazeti la Mwananchi
"Zawahiri ndiye aliyekuwa anaongoza Kundi la Al-Qaeda, katika kuishambulia Marekani kwa akitumia silaha nzito za maangamizi.Makachero sita wanaopambana na ugaidi na baadhi ya watu wanaomfahamu Zawahiri, walikiambia Kituo cha Televisheni cha Al Jazeera kuwa kwa miaka mitatu sasa, Zawahiri amekuwa kimya, akiendesha operesheni za chini kwa chini.
"Sasa amekuwa kimya akiendesha operesheni za Mtandao wa Al Qaeda kisayansi na kwa kutumia utalaamu wa hali ya juu," mmoja wa maafisa hao alisema.Mwaka 2008, Zawahiri aliandika kitabu kilichokuwa kinaelezea historia na umahiri wake katika kutumia sila nzito za mabomu aina ya nuclear na mtazamo wenye misingi ya dini wa Mtandao wa Al-Qaeda, kuhusu kuua watu wengi kadiri iwezekanavyo.
Kitabu hicho pia, kinaonyesha jinsi Zawahiri alivyoandaa mpango wa kulipua majengo ya Marekani Septemba 11 mwaka 2001. Hali kadhalika, kinaonyesha namna Zawahiri alivyotekeleza mapango huo akishirikiana na mshirika wake wa karibu bin Laden.
Kwa hili unafikiri ni nini kitakachofuatia??.. ..ni kuanza kumtafuta Al-Zawahiri na kuanza kupiga nchi za watu kwa kisingizio cha kumtafuta, usishangae kama watamuua wakaja na jina jingine la mtu "hatari" na kuendeleza uonevu wao, umepata kitu..........?????