Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

Katika baadhi ya yaliyotekelezwa limo hili la kuifukuza Alex Stewart na kuanzishwa kwa TMAA...soma zaidi hapa...



The government is saving more than Sh11 billion a year after parting company with a controversial foreign gold auditing firm, which was fleecing it.


The Alex Stewart (Assayers) Government Business Corporation (ASAGBC) was being paid Sh16.4 billion every year to audit gold produced in the country while Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA) last year was paid only Sh3.4 billion for the same work. However, the company has projected to spend Sh5 billion this year following extension of its services to more mining sites.

Briefing journalists yesterday, the Chairman of Parliamentary Committee on Mineral and Energy, Mr William Shelukindo, said the government's decision not to extend Alex Stewart contract was commendable. He also said that the local firm which has replaced the foreign company had employed locals.


The TMAA work report of August 2007 to December 2008, showed that ASAGBC had 46 -38 were Tanzanians and only eight were foreigners.
"We were paying a lot of money to the foreign company while the work was done by Tanzanians. They are basically the same people who are doing the work now and we are not doing bad," MR Shelukindo said.


He said TMAA had 53 workers, who were all Tanzanians and it expected to hire 35 more workers this year. He said the Agency also planed to train its staff to improve their skills.


But the committee asked the Agency to rotate its workers frequently. In its audit report, TMAA has exposed a number of shortcomings including mining companies which were acquiring huge loans without the permission from Bank of Tanzania.


The report also revealed discrepancies in salary payments between Tanzanian and expatriates doing the same work for mining companies in the country.

Source: allAfrica.com: Tanzania: Billions Saved in Gold Audit By Local Firm
 
Pia kuna mikataba mingine alishindwa kuvunja kutokana na masharti magumu yaliyotakiwa kutimizwa kama tulivyoona kwenye vyombo vya habari na hasa magazeti.
 
Matumizi mabaya ya ofisi kwa kuvunja sheria makusudi nadhani akijisemea watanifanya nini?

Jamani hamkumsikia siku ile Dodoma? alisema yeye anaweza kuwa dikteta na hakuna cha tume za haki wala nani anayeweza kuuliza. Nadhani sasa anatimiza matakwa yake. Ngoja tuone game litakavyokwenda kati ya mwanajeshi na raia wa kitanzania.
 
Sheria iko wazi, JK hajatenda kosa. Wengi wa JF hawajaisoma na kuielewa ndo maana kuna kupotoshana kwenye posts zetu. Isomeni kwanza ndo mtajua kuwa kazi ya Mhe Tendwa ni rahisi, kutupilia mbali malalamiko hayo.
 
Sheria iko wazi, JK hajatenda kosa. Wengi wa JF hawajaisoma na kuielewa ndo maana kuna kupotoshana kwenye posts zetu. Isomeni kwanza ndo mtajua kuwa kazi ya Mhe Tendwa ni rahisi, kutupilia mbali malalamiko hayo.
We uliyesoma na kuielewa tofauti na sisi weka kifungu unachodhani sisi tunaelewa vibaya tukijadili sawa?
 
Watu bado wanaamini kuwa udikteta ni lazima mtutu utumike. Hiyo ni zamani, huu wa JK ni udikteta mamboleo. Watu bado wanamwamini wakati ana uwongo wa kitoto sana. we unaenda kila mkoa unaahidi na kudanganya watu kwa kuwa tu hawakusoma, hawana uelewa wa mambo wako vijijini vumbi limewaziba macho na umaskini. Hawajiulizi yale aliyoahidi mwaka 2005 kama ametekeleza hata moja!
 
WAGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wenza wao wameendelea kumwaga sera na ahadi zao katika mikutano ya kampeni wakiomba ridhaa kwa Watanzania.

Wakati mgombea wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alikuwa Mbeya, wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alikuwa Dodoma huku mgombea mwenza wa CUF, Juma Duni Haji akiwa Kagera.

Mgombea wa CCM akizungumza juzi katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, aliahidi kuwa kiwanda cha kuzalisha makaa ya mawe cha Kiwira mkoani Mbeya, kitaanza uzalishaji na wafanyakazi watalipwa madai yao, anaripoti Mgaya Kingoba.

Aidha, alisema Serikali ya CCM itawaingiza wakulima wa viazi mbatata katika ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.

Mbali na hayo, wafanyabiashara wa Mbeya wana kila sababu ya kufurahia baada ya kuahidiwa kujengewa soko jipya kama la Mwanjelwa lililojengwa baada ya la awali kuungua moto mwaka 2006.

“Kuna suala la kiwanda cha makaa ya mawe cha Kiwira … kiwanda hiki kilikumbwa na matatizo makubwa yakiwemo ya kisiasa, kiasi cha uzalishaji kusimama,” alisema Kikwete na kuongeza:

“Lakini sasa tumeshatafuta fedha kwa ajili ya kuanza uzalishaji mkubwa wa umeme wa megawati 200, tutawalipa wafanyakazi fedha zao wanazodai na pia tutaongeza wafanyakazi wengine.”

Kiwanda cha Kiwira kilichoko katika wilaya za Kyela na Ileje, kilikumbwa na matatizo mbalimbali yakiwamo ya uwekezaji na kusababisha uzalishaji kusimama na hivyo wafanyakazi kudai mabilioni ya fedha.

Akizungumzia kilimo, mgombea huyo wa CCM alisema Serikali ya chama hicho itaendelea kutoa ruzuku ya pembejeo katika mazao mbalimbali na inafikiria kutoa ruzuku kwa zao la viazi mviringo.

Alisema, hiyo inatokana na maombi ya wakazi wa wilaya za Mkoa huo wa Iringa, kutaka zao hilo liingizwe katika utaratibu huo ambao kwa sasa unahusisha mazao ya chakula hasa mahindi na ya biashara ambayo ni mpunga, korosho, pamba, chai na kahawa.

“Tutaendelea kuongeza ruzuku ya vocha za pembejeo kwa wakulima ambao mwaka huu wamefikia milioni 2.5. Tumeongeza fedha kufikia Sh bilioni 143 mwaka huu.

“Lakini nilipokuwa natoka Rungwe, nilisimama njiani na wakulima wa viazi wakaniomba tuwapatie vocha za ruzuku kama wenzao wengine.
Na hata niliwahi kumwuliza Mama Makinda (Anne) kwa nini Njombe wanatumia mbolea sana, alieleza kuwa wanaitumia pia katika viazi … kwa hiyo tunalichukua hilo na tutafanya utaratibu wa kulipatia ruzuku,” alisema.

Akizungumzia soko jipya la Mwanjelwa, alisema serikali ilikuwa mdhamini kwa Halmashauri ya Jiji la Mbeya katika kupata mkopo wa ujenzi wa soko jipya baada ya awali kuteketea kwa moto mwaka 2006.

Alisema tayari soko jipya limekamilika na litachukua wafanyabiashara 2,000 na kwamba kipaumbele kiwe kwa waliokuwa katika soko lililoteketea.

Aidha, alisema wafanyabiashara 1,500 walioko eneo la SIDO wawe wa kwanza kupewa nafasi katika soko hilo jipya.

Aliitaka Halmashauri ya Jiji kutafuta sehemu nyingine ya kujengwa soko jipya lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 2,000 jijini humo ili kuwapatia nafasi zaidi wafanyabiashara kufanya shughuli zao.
 
Wabunge wanagombea kwa sababu nafasi ziko vacant sasa hii ya rais bado yupo sijui ataacha lini urais ili awe mgombea na yeye.Hii inanichanganya.Ili uwe waziri lazima uwe mbunge sasa mbona bunge halipo lakini mawaziri wapo.Nafikiri katiba mpya inahitajika haraka
 
Jamani mi ni first time hapa napost topic. Kikubwa kilichonitouch ni hizi ahadi anazotoa huyu JK ni nyingi sana kiasi kwamba watu wameanza kutilia mashaka kama zote zitatekelezwa within 5 years. naomba wanajamii tuanze kuzilist hapa chini, na kuzidiscuss kidogo. kwa kuanzia tu
1. Meli kubwa zaidi ziwa victoria
2. Soko jipya la kwa wafanyabiashara mbeya
3.Meli na Kivuko Kipya maeneo ya Itungi Port hadi Matema(Ni Kyela Kama Sikosei)
4.Kufumigate nyumba ZOTE Tanzania katika kupambana na malaria.
5.Vyandarua Million 14
6."Nitatoa billioni 5 kulipia maden ya Nyanza.........."(mnisaidie na hapo wanajamii kuiweka sawa hiyo ahadi)
7.....................
8...........................
9............................
10............................
11................................
12................................
Uwanja ni wenu. karibuni........
 
Umesahau na meli mpya kule Kigoma pia.

kiwanja cha kisasa cha ndege Missenyi na Kigoma wakati ule wa Songwe Mbeya kashindwa kumalizia kazi alizoanza Benja. Ukisikia ya Musa utastaajabu ya farao.


Kila mkoa kuwa na hospitali ya rufaa kama Bugando au Muhimbili
:becky: wakati tuna picha hapa hata kununua vitanda vya vituo vya afya ameshindwa. Naona maumivu ya kichwa uanza pole pole.

attachment.php
 
Umesahau ahadi ya kutoa bajaji 400 kwa ajili ya kusafirisha wajawazito
 
Jamani mi ni first time hapa napost topic. Kikubwa kilichonitouch ni hizi ahadi anazotoa huyu JK ni nyingi sana kiasi kwamba watu wameanza kutilia mashaka kama zote zitatekelezwa within 5 years. naomba wanajamii tuanze kuzilist hapa chini, na kuzidiscuss kidogo. kwa kuanzia tu
1. Meli kubwa zaidi ziwa victoria
2. Soko jipya la kwa wafanyabiashara mbeya
3.Meli na Kivuko Kipya maeneo ya Itungi Port hadi Matema(Ni Kyela Kama Sikosei)
4.Kufumigate nyumba ZOTE Tanzania katika kupambana na malaria.
5.Vyandarua Million 14
6."Nitatoa billioni 5 kulipia maden ya Nyanza.........."(mnisaidie na hapo wanajamii kuiweka sawa hiyo ahadi)
7.....................
8...........................
9............................
10............................
11................................
12................................
Uwanja ni wenu. karibuni........

Uwezo wa serekali kutekeleza ahadi zote hizo upo nakubaliana na kikwete,tatizo kubwa tulilonalo ni utekelezaji wa ahadi za raisi kipindi cha uchaguzi zinachukuliwa kama masihara.kikwete hana tatizo ili watendaji ndio wana matatizo.kubwa la kufanya ni kubadili mfumo mzima wa serekali na yeyote atakeyeingia kwenye system basi ajue yuko kwa maslahi ya taifa zaidi na siyo binafsi kama ilivy sasa.
Upinzani unatakiwa utusaidie sana kuondoa hii gap kubwa iliopo sasa kabla hatujashuhudia ukiukwaji wa amani tanzania.
Vyombo vya habari vinachangia sana kuvunjika kwa hali ya amani ktk nchi,kwa mfano ITV wanataka kujadili issue ambayo iko kwa msajili wa vyama mh Tendwa ni kama kesi iko mahakamani wewe unaanza kuijadili uraiani,ni kukosa hekima,tumwache Tendwa atende yatakayojiri na tukubadiliane yatakayoamuliwa kwa sababu tayari tunajua Tendwa ataamua nini pale,kila mtu anajua maamuzi ya jumatatu ni nini,kwa hiyo siyo kitu cha kushangaza.
Ni mawazo yangu tuu.

 
Natamani ifike siku ya uchaguzi upesi maana natarajia mabadiliko makubwa sana katika nchi yetu. Hii inatokana na ahadi zinazotolewa na watarajiwa .

Naamini tutapata viongozi bora waliotokana na mchakato uliojaa uadilifu thanks to sheria zilizotungwa kuzuia rushwa na pesa chafu katika uchaguzi, ambazo zingeweza kutupatia viongozi wasiokuwa na uchungu kwa nchi yetu. Sipati picha ni vipi safari hii tutasikia mbunge akitamba ati kaingia bungeni kwa pesa yake! Itakuwa maajabu kweli kweli maana hii itakuwa sawa na kujibu " guilty as charged' hata kabla charge sheet haijafikishwa kwa pilato! TAKUKURU nadhani watakuwa macho na masikio kusubiri maungamo kama haya wafanye kweli!


Tunashukuru taasis zetu hasa TAKUKURU kwa kuingilia kati na kuzuia wale wote waliojaribu kutinga kwenye bunge kwa kununua kura hasa za maoni.

Tumeahidiwa mambo makubwa ambayo kama yatatekelezwa basi tunaweza tunapunguziwa kama siyo kuondolewa kabisa shida na matatizo bila kusahau dhiki zetu!

Ahadi za mwaka huu naona zimepitiliza.

Hebu naomba tuorodheshe ahadi hizo ili tuwe na checklist ya kufuatilia maana tuliwahi kuambiwa - MALI BILA DAFTARI HUPOTEA BILA HABARI.

Mgombea wa URAIS kupitia CCM kaahidi:
(BTW - Maisha bora kwa kila mtanzania bado ipo au imeondolewa?)
1. Usafiri wa treni DSM
2. Kupandisha kiwango cha mshahara
3. Meli mpya Ziwa Victoria
4. Huduma bora ya maji
5. Atafanya Kigoma iwe kama Dubai! na kuwajengea uwanja wa ndege

endeleza.............

Mgombea urais kupitia CHADEMA:
1. Kupunguza mishahara ya wabunge
2. Kupunguza mshahara wa Rais kwa asilimia 20
3.

endelezeni .............
 
Asante sana.. angalau tunaweza kufuatilia ahadi za hawa..

MGOMBEA WA CUF

... Elimu Bure kuanzia Chekechekea hadi Chuo Kikuu! (amewapiku CCM na Chadema)
 
Hivi urais unagombewa na CCM, CHADEMA na CUF tu? Nadhani kuna TLP pia.Nani anakumbuka ahadi za mgombea? NCCR nadhani bado wanajipanga watoke vipi.
 
Back
Top Bottom