Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Orodha ya ahadi za Kikwete kwa wananchi 2010-2015

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bramo, May 29, 2010.

 1. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #1
  May 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,453
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha


  ---2005 Alikuja na Maisha bora kwa kila Mtanzania,hili halina ubishi lilikuwa ni changa la macho kwa Watanzania,Kama haitoshi akasema anawajua kwa majina wala rushwa,lakini hatuoni hata mmoja aliyemchukulia hatua===hii ni kutaka sifa na popularity.

  ---Juzi amekuja na mpya ya kumpatia kila mwanafunzi Computer ambayo iko connected kwa internet, it's high time now kwa watanzania kuhoji uwezo wa RAIS wetu,ni kwamba anafanya Wa Tanzania ni wapumbavu sana kiasi kwamba hawawezi ku reason kuwa hilo sual haliwezekani???

  Hata kwa wanafunzi tu wa vyuo vikuu hilo suala halitekelezeki leo anatuambia ataanza na shule za msingi,umeme ni tatizo..hivi jk anajua kuwa its only 10% ya wa Tanzania wana access na umeme na 0.05% ya watanzania ndo wanaweza kutuima computer na wana access na internet,hata kwa nchi ambazo zimeendelea kuzidi sisi hilo suala halipo,,yeye anataka kuhadaa Wa Tanzania aili aendelee kubaki madarakani!!!!!me nadhani pia JK na uwezo mdogo sana wa ku reason ndo maana hata hafikirii kuwa suala kama hilo watu wenye akili timamu hawawezi kusadiki,inahitaji mtu mwenye akili za mwenda wazimu kuamini ahadi kama hizo.

  ----WITO WANGU
  Nawaomba wana JF wooote..mu influence watu wenu wa karibu wasimchague JK na CCM yake,watatoa ahadi nyingi sana,watasema watajenga fly over,watasema watajenga majumba angani--->tuwapuuuze na ahadi zao hizo...tuwaulize kati ya zile walizoahidi 2005 ni ngapi wametekeleza mpaka tuwape ajira nyingine kwa miaka mitano!!!!!!

  Watakuja na gia ya kuwa wamejenga DOdoma University,tuwapuuze pia kwa sababbu kwanza ulikuwa ni ukumbi wa bunge wa zamani (chimwaga),halafu huo ni wajibu wake...tuipuuzie kete ya kipuuzi kama hii.
  SAY NO TO CCM-----SAY NO TO JK-----WANYIMENI KURA

  -----------------------------
  [h=2]Miezi 22 kabla ya uchaguzi mkuu:Tujikumbushe ahadi za Kikwete 2010, ngapi zimetekelezwa hadi sasa?[/h]

   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  nimekusoma mwana
   
 3. IsayaMwita

  IsayaMwita JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2010
  Joined: Mar 9, 2008
  Messages: 1,123
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bramo,

  Mbona hutuambii tumchague nani?

  soma hii thread (je Dr. Slaa akitupa jalamba ushindi utakuwepo?)
   
 4. Bramo

  Bramo JF Bronze Member

  #4
  May 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 9,453
  Likes Received: 2,502
  Trophy Points: 280
  Ngoja tusie CHADEMA watamsimamisha nani...ila nawaaasa na CCM na JK wake.
  Sio siri,chadema ndo mbadala wa CMM
   
 5. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
 6. n

  n'golofu Member

  #6
  Jun 3, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimekupata vizuri
   
 7. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Asubuhi nimemsikia Waziri wa Nishati na Madini clouds anajifagilia kuwa umeme utafika katika kila makao makuu ya wilaya Tz nzima (sijui alikuwa anatania..?) Hivi ilani ya uchaguzi si inatakiwa kumalizika kabla ya miaka 5 kwisha? Ama ndo yale ya kupimwa viatu mwaka huu, afu miaka mingine 5 ya kuviagiza, afu mingine mitano ya kuvigawanya... the story has no end!
   
 8. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #8
  Jun 3, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Japan's prime minister, Yukio Hatoyama, today said he would resign just eight months after he took office, after failing to honour election promises to bring sweeping change to domestic policy and fundamentally alter the country's relations with the US.
  The world's second biggest economy faces yet another period of uncertainty after Hatoyama, whose Democratic party won by a landslide last year, became Japan's fourth prime minister in as many years to step down after a year or less in power.
  In a further blow to the Democrats five weeks before upper house elections, Ichiro Ozawa, the architect of last year's election victory, will also step down amid a political funding scandal.
  "Since last year's elections, I tried to change politics so that the people of Japan would be the main characters," Hatoyama said in a nationally televised address to party members.
  Although he has had some success in shifting power from bureaucrats to politicians, Hatoyama conceded that he had failed to win public support for his administration's handling of the economy and, crucially, his recent decision on the fate of a US military base on the southern island of Okinawa.
  "That was mainly because of my failings," he said, his eyes filling with tears. "The public has refused to hear me."
  His fate was in effect sealed by his decision last week to renege on a campaign promise to move a US marine airbase off Okinawa – a move he hoped would demonstrate his determination to end Japan's subservience to Washington's foreign policy.
  In the end, US intransigence and the lack of a viable alternative site forced him to accept a 2006 agreement to move the base from its city centre location to an offshore site on the island's northern coast.
  His change of heart enraged politicians and residents on Okinawa, who accused him of betrayal, and sent his public support ratings below 17%, compared with over 70% when he took office last September.
  Hatoyama, 63, said the importance of maintaining a strong US alliance in the face of a rising China and instability on the Korean peninsula had forced him to cave in to Washington's demands.
  Wallahi, nadhani viongozi wetu watatambua madhara ya ahadi hewa za kampeni, mwenzao kacheki caona umaarufu umeshuku akaogopa kuandikwa vibaya kwenye historia, akaamua kuandikwa vizuri akaachia ngazi. Viongozi wetu wanangoja mpaka wananchi wawafukuze kazi ili wawe negative part of history.
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ziwekeni AHADI ZAKE ZOTE TUZIPE ALAMA ILI HATIMAYE TUPATE MAJIBU YA UHAKIKA YA MATOKEO YAKE ALIYOPATA;

  NAANZA NA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA-AMEPATA D(19)-FAIL;SABABU KILA MMOJA ANA YA KWAKE
   
 10. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #10
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Rais Mkapa aliwahi kusema kitu kikubwa kinachohatarisha usalama wa nchi za Kiafrika ni kuweko kwa vikundi vinavyohodhi madaraka. Kikundi kilichoko madarakani Tanzania sasa ni kile kile ambacho kimetutawala tangu tupate Uhuru miaka 50 iliyopita. Na bado kinang'ang'ania madaraka.

  JK aliwahadaa wana UDSM kwamba ataboresha uenjinia. Kutokana na kushuka kwa uwezo wa kufikiri hapo Kilimani (walimshangilia sana), wasomi wetu hawakutambua kwamba hizo ahadi hazikuwa funded.

  JK aliahidi kukamilisha haraka barabara ya Mtwara hadi Mwanza. Hiyo barabara ingemalizika mwaka 2007 kama JK hangekuwa Rais.

  JK aliahidi kumaliza kabisa shida ya maji Dar es Salaam. Aliahidi kumaliza shida ya umeme Tanzania. Aliahidi kumaliza upungufu wa waalimu. Maneno matupu.

  Thanks to 50 years of misrule by TANU and CCM, Tanzania is now the economic backwater of East Africa. If we elect the same people, we will get the same result.

  It is 100% against our national interest to return CCM to power.
   
 11. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #11
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo slide show inatia uchungu sana, hiyo ni sehemu tu ya mateso wanayopata akina mama wa Tanzania na wananchi wengine kwa ujumla. Inauma sana Serikali inapoyafumbia macho matatizo ya msingi yanayowakabili wananchi wake kwa kisingizio cha ukosefu wa fedha lakini fedha kwa ajili ya safari za nje za rais pamoja na wapambe wake, kununua magari ya kifahari, kutuma mawaziri mikoani kwa safari ambazo hazina tija yote hayo hayakosi fedha za kugharamia. Ni aibu rais wa nchi kutamka hadharani kuwa kila mwanafunzi wa primary school atapatiwa computer ilhal mwanafunzi huyo hana jengo la kujisetiri wakati wa mvua ama jua achilia mbali dawati la kukalia.
   
 12. m

  mpuguso Member

  #12
  Jun 4, 2010
  Joined: Oct 1, 2009
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Za kuambiwa changanya na zako!!!!!!!!! ahahahahaahah, Mbaiwayu hiyoooo.

  Najaribu kufuatilia nicknames za viongozi wetu wastaafu

  mwalimu aliitwa Mchonga meno
  Mzee mwinyi aliitwa Ruksa
  Mkapa aliitwa ukapa
  Mzee Jakaya na guess ataitwa Mbaiwayu!

  ahaha its fun!
   
 13. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #13
  Jun 4, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Ajira millioni moja ziko wapi?
   
 14. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Aliahidi, kwenye bajeti ya 2009 / 2010, kwamba angetumia shilingi trilioni 1.1 kwenye Wizara ya Elimu na Ufundi. Si kweli.

  Aliahidi angeshitaki gazeti moja la Uingereza lililoandika kwamba wakati wa kampeni za 2005, Rostam Aziz alikabidhiwa $20 mil. na Iran kwa ajili ya kampeni za Kikwete. Mbona hajafanya hivyo hadi leo?

   
 15. Rufiji

  Rufiji JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2010
  Joined: Jun 18, 2006
  Messages: 1,710
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
 16. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #16
  Aug 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Hili linanitatiza sana, binafsi nafikiri sio sahihi kabisa kwa mgombea urais kutumia mipango ya serilkali kama ahadi za chama chake.

  Kwa mfano, kusema, ....tumeshaanza kufanya uchambuzi yakinifu wa barabara X na tutaanza kkuijenga mwakani.........this is wrong in my opinion.

  Mnasemaje wakuu??
   
 17. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #17
  Aug 29, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  Tatizo kubwa lipo kwenye katiba yetu, ilikuwa inapasa wakati huu wa kampeni (Mwezi mmoja) 'kipindi cha mpito' nchi iwe chini ya jaji mkuu, ambaye yeye sio mtu wa kugombea kura kama raisi au Spika (Mbunge), sasa hao wote wanaosimamia sheria ni wateule wa Raisi na mpaka sasa Jk anapompa masharti mtu yoyote say TIDO, anampa kama raisi na sio kama Raia Mgombea uraisi,

  wakina Slaa wanachangishana fedha za Kampeni, lakini Jk anatumia fedha za serikali kufanya kampeni zake, wale wanausalama waliokuwa wanamzoazoa pale jangwani siku ya uzindizi wa kampeni walikuwa pale kumlinda raisi na wala sio Mgombea Urais na ni kwa gharama zako wewe mlalahoi,

  kuna mapungufu mengi mno, kiasi watu wanashindwa kutofautisha mambo ya CCM na ya Kiserikali
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  mkuu ndo maana nafikiri ni sahihi kabisa kubadilisha this F* katiba. Slaa is right here. siku 100 za mabadiliko makubwa.

  we need this change.
   
 19. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,365
  Likes Received: 7,001
  Trophy Points: 280
  HAYO MABADILIKO ANAYOYASEMA SLAA WALA HAYAHITAJI FEDHA, KILA MTU AKITIMIZA WAJIBU WAKE IPASAVYO, SIKU 100 (1st Quarter) ya mwaka kila kitu kitakuwa kwenye mstari, ni uwajibikaji tu
   
 20. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #20
  Aug 29, 2010
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,826
  Likes Received: 553
  Trophy Points: 280
  Si hivyo tu hata ile tabia yake ya kutoa maagizo(kama rais) kwenye jukwaa la kampeni kama alivyofanya mkoani kagera kuigawa ranchi kwa wananchi,ni ukiukwaji wa taratibu!
   
Loading...