Yaani Mbeba Maono, umekaa katika computer yako na kudhani unatoa maono, kwa JF na jamii kwa ujumla kwa kuzungumzia suala kuwakandia Ze Comedy, wewe sasa ndiyo stage kwa leo. Kam walivyosema wenzangu huko nyuma kwamba inaonyesha wewe ni MBABE SANA. Na ninadhani hata jina lako ulikosea kuandika ulidhamiria kuandika MBABE WA MAONO. Mbele yako pale sebuleni watoto wako hawaongei kwa sauti bali kwa kunong'ona unadhani ni kwanini? Ubabe wako. Sasa nakuamuru, "Ondoka Ubabe wako Umekuponza....."
Naunga mkono kabisa! Sidhani kama kila tendo linachekesha.
Hawa wanaweza kuwa wanachekesha kwa kundi fulani na isiwe kwa kundi jingine.
Tutawaita wasanii waliofanikiwa kama watachekesha majority. Isiwe kila upuuzi udhaniwe kwamba unachekesha, eti ni comedy.
Binadamu hataki kuona utu wake ukidhalilishwa na ndiyo maana kama uko fit ki-akili usingependa kuona sex yako ikidhalilishwa.
Siyo Dume zima lionyeshwe kama jike au jike lionyweshwe kama dume, halafu useme ndiyo maana ya comedy. Comedy to who?
Hawa watu wana challenge maana sasa hivi nionavyo mimi, they are overdoing. so called comedy is turning to be stupidity.
Mwanzo ulikuwa mzuri na ukielimisha na kurekebisha jamii juu ya matukio yanayotokea. Lakini hiii ya sasa! NO! NO!
jamani, mmenisema sana, hii inaonyesha ni watu wa aina gani tulionao tz. kazi kwelikweli. lakini ukweli uko palepale. jana niliona kipindi fulani cha star tv, kinaonyeshwa kuanzia saa tatu kamimi usiku kila alhamisi, ni komedi yao na wao, wenyewe wanaita FUTUNI. naomba jaribuni kuangalia hiyo, halafu museme. wale jamaa waliigiza namna ya ushirikina ulivyofanywa kule bungeni hivi majuzi, lakini the way walivyo express, wanachekesha na wanaonekana wameenda shule, kwa ufupi jamaa wana onyesha kutoa ujumbe kisomi, kiustaarabu na hakuna hata doubt. mimi nina kazi zangu, wala msiseme kuwa nimetumwa na hao jamaa. ninyi wenyewe angalieni ile halafu mjaji wenyewe namna kina joti wanavyotakiwa kufanya. jamaa wanavaa vizuri, wanaongea maneno yasiyo ya udhalilishaji, yasiyo ya kitoto wala utumbo, ila wanachekesha na kufurahisha. na nina hofu kuwa, wale jamaa wanaweza wakawapiku kina joti kwa mda si mrefu. amini msiamini mtaona wenyewe kwa macho yenu. kwaherini.
You shall serve the hands that feed you. Kama wame nunuliwa na Manji hiyo siyo siri loyalty yao itakua kwa nani. Usishangae kwa wao kutumika. Unafikiri Manji kawa mwagia mamilioni kwa ajili ana wapenda sana? Alikua na nia na madhumuni ya kuwa chukua. Akisha watumia ata watupa tu na wanaweza kurudi kumlilia Mengi. Japo kuna sehemu nataka kuku rekebisha.Mengi hakuwa hudumia hawa watu personally, walikuwa waajiriwa kama walivyo waajiriwa wengine. Sidhani kama walikua na mahusiano binafsi na Mengi. Hapa ni kwamba kituo cha Mengi ndiyo kili watoa ila siyo kuwa Mengi aliwa chukua chini ya mabawa yake na kuwalea. With that said I still fon't think they should have disrespected Mengi the way they did.
sasa kama kituo cha mengi ndo kiliwatoa, si mengi mwenyewe? unafikiri hakimuumi mengi? have you ever been betrayed in your life? umemsaidia mtu au niseme kampuni yako imemsaidia mtu alafu anakuja kukugeuka, hata kama hautaki chochote toka kwake, inauma sana because you fee betrayed. hao watoto walitoka kupitia vyombo vya habari vya mengi. hata kama si hivyo, basi wangeondoka wafanye kazi sehemu ingine kama mengi hawalipi vizuri.
ninachosapoti mimi, ni kwanini wanawatetea mafisadi? kwanini wanatumiwa kama instruments na mafisadi kupinga wapigania maslahi ya watz? ni kweli, watatumiwa, likitokea kundi lingine lenye mvuto zaidi yao, kina manji watalinunua hilo wao watatupwa kama hawajawahi kujulikana. remember, upandacho ndicho utakachovuna. ukipanda betrayal utavuna betrayal. kwa macho yenu mtaona kuna siku hawa orijino comedy watalia na kusaga meno.