Kama unafanya biashara kaa kimya usjibu matusi ya watu, matusi yanakupunguzia credibility.
Kama unajua marketing tafuta namna ya kufanya watu wakuamini, wanakutusi usiwajibu, kaa kimya jibu wenye kuuliza bei na details za biashara.
Ni muhimu sana kua mkimya na kujibu kauli nzuri kwenye bishara ndio maana hata ukipiga simu customer care ya voda,tigo, halotel au airtel hata ukimtukana matusi ya nguoni huyo mtoa huduma bado hatakujibu matusi yako sana sana atakwambia "asante kwa kuchagua vodacom nakutakia mchana mwema"
Kua makini tafuta njia ya kuaminika, kikubwa ni kuaminika tu, ukishaaminika wateja wapo wengi sana humu.kuna wauza bidhaa wenzako walishaaminika humu saivi wanakula ela kiulaini kila mtu anawaamini.
Nakupa mifano kuna member anaitwa abdulwahid anauza Eletronics kama TV kutoka Zenji huyo anauzia watu mizigo hapa hapa jf na watu wanamuamini sana.