Mpaka muda huu sidhani kama kuna ambaye hajajua kinachoendelea huko Mashariki ya kati between Israel and Palestine.
Kwa upande wa Palestine, mapema leo asubuhi wameanzisha peration maalum ijulikanayo kama 'operation Al aqsa' inayojumisha makundi ya wanamgambo wa Hamas na Hesbola yenye lengo la kukomboa maeneo ya Palestina ambayo yanakaliwa kimabavu na Israel, like ukanda wa Gaza.
Katika kujibu mashambulio hayo mabaya zaidi kutokea Israel tangu miongo kadhaa iliyopita, waziri mkuu wa Israel ametangaza rasmi ya kuwa nchi yao ipo vitani na 'operation Iron sword' tayari imesha anza.
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti waisraeli 100 wameshauwawa na wanajeshi w 57 wametekwa, wakati kwa upande wa wapestina, watu wapatao 120 wameuwawa. Inasemekana jumla ya majeruhi imefikia elfu 1000 so far.
Je, ni operesheni ipi itaibuka kidedea?? maana hali inazidi kuwa mbaya kila dakika inapokata.