3D
Kwa nin kuona movie ya 3D inabidi watu wavae miwani? Je Ina maana macho yetu binaamu uwezo wake unaishia kwnye 2D mpaka tuhitaji msaada artificial.
MACHO YA BINADAMU YANAVYOONA
Macho ya binadamu yanaona 3D. Hebu tazama mouse ya kompyuta yako au kitu chochote kilicho mbele yako. Fumba jicho la kulia na kitazame hicho kitu kwa jicho la kushoto bila kuyumbisha shingo. Then kitazame kwa jicho la kulia na fumba la kushoto. Rudia kitendo hiki haraka-haraka...kushoto-kulia kushoto-kulia kushoto-kulia ..haraka haraka bila kugeuza shingo. Utagundua kuwa ukikitazama kwa jicho la kulia kina-appear kuwa kulia zaidi na ukikitazama kwa jicho la kushoto kinaonekana kuwa kushoto zaidi..ni kama vile kinahama-hama position. Ukikitazama kwa macho yote kina-appear kuwa katika position ambayo ni
average ya jicho la kulia na kushoto. Hii inamaana kuwa kila jicho hupeleka picha tofauti kidogo katika ubongo na ubongo hufanya kazi ya kutafsiri average position kwa kutumia taarifa ya positions mbili zinazoletwa na macho mawili.
Chukua simu yako halafu igeuze uitazame upande wake mwembamba (namaanisha
usiitazame upande wake wa mbele wala wa nyuma badala yake tazama upande wa thickness). Ukitazama kwa jicho la kulia pekee utaweza kuona upande wa thickness wote na upande wa mbele kidogo (kama mbele ulipageuzia kulia). Ukitazama kwa jicho la kushoto utauona upande wa thickness wote na upande wa nyuma kidogo (kama nyuma ulipageuzia kushoto). Hii inamaanisha ukitazama kwa macho yote mawili utaona upande wa nyuma kidogo, upande wa thickness wote na upande wa mbele kidogo... hapa ubongo umefanya tena kazi ya kutafuta average.
Hivyo ubongo husaidia kuunda taswira yenye perspective pana zaidi ambayo kimsingi ndiyo 3D yenyewe. Kwa msaada wa views mbalimbali za macho kama nilivyoeleza hapo juu na kwa msaada wa vitu mbalimbali ambavyo huwa vimeambatana na mazingira kama watu, miti, mawe, magari nk ambavyo huwa katika sizes, positions, movements na distances tofauti tofauti tunaweza kuona dunia kwa namna ya kawaida kama unavyoona wewe sasa..yaani 3D. Kilicho mbali unakiona hivyo, kilicho karibu unakiona hivyo. Kilicho nyuma ya kingine unakiona hivyo na unapata picha kiko kwa nyuma kwa umbali gani.
KAMERA YA KAWAIDA NA KAMERA AMBAYO NI STEREOSCOPIC
Kamera ya kawaida iwe ya video au still picture huwa na apecha (tundu la lenzi) moja tu. Kamera za 3D stereoscopy huwa na apecha mbili kama inavyoonekana ktika picha hapa chini:

Kamera hizi hurekodi images za positions mbili tofauti kama macho yanavyofanya. Hebu tazama hapa chini mfano wa picha ile ile kama ilivyoonwa na matundu mawili tofauti ya kamera moja:
Unagundua tofauti yoyote katika hizo picha mbili? Angalia picha ya kulia, miti iliyo mkono wa kushoto wa msichana mkubwa inaonekana kumgusa zaidi kuliko inavyoonekana katika picha ya kushoto. Pia katika picha ya kulia kuna kidude fulani cheusi hewani juu ya kichwa cha msichana mdogo, katika picha ya kushoto kidude hicho kiko zaidi kwa msichana mkubwa nk nk. Hivyo ndivyo camera ya apecha mbili hurekodi (kama ambavyo macho mawili yaonavyo).
Sasa hebu sasa tupate average ya ubongo ya picha hiyo ya wasichana hapo juu hapa ndipo utapoona 3D image (Hata hivyo inahitaji ku-concentrate kidogo akili na kupractice kwa sababu ubongo unakuwa haujatarajia kuona utachokiona):
Ukitazama kawaida hiyo picha utaona ni picha mbili kama unavyoona sasa. Anza kufanya makengeza kidogo kidogo huku ukizidisha makengeza kidogo kidogo...utaanza kuona picha tatu..mbili pembeni na moja imeongezeka katikati...
usizidishe makengeza maana utaanza kuona nne...nataka uone tatu tu. Ukiweza kuona tatu sasa concentrate kwa ile ya katikati... move kichwa chako pole pole mbele na nyuma huku ukiendelea ku-concentrate akili yako katika picha ya katikati... itafikia hatua hiyo picha ya katikati itakuwa very clear na hapo utaona fimbo aliyoishika huyo mdada imesogea mbele na mazingira kama miti na nyumba waliyoipa mgongo iko nyuma sana. Hivyo ndivyo 3D inavyoonekana kwa kuvaa miwani.
SINEMA NA UVAAJI MIWANI.
Kama X-Paster alivyoeleza hapo juu teknolojia ya 3D ni pana na kuna miwani tofauti-tofauti tegemeana na teknolojia husika... kwa kawaida ukitazama sinema iliyokuwa enabled katika 3D usipotumia miwani utaona video iko kama gazeti lililochapishwa vibaya, kama picha ifuatayo inavyoonesha:
Picha hii imekuwa distorted kidogo kwenye colour channels (kama unavyoiona picha....sitazungumzia kiundani). Sasa huwezi kuona 3D ya picha hii kwa kufanya makengeza.. unahitaji miwani ambayo imekuwa designed kusoma hizo colour channels ("colour channels" ni lugha yangu mwenyewe.. nadhani kuna jina sahihi zaidi) na kuupa ubongo illusion ya 3D.
Hii ndiyo sababu ya kuvaa miwani katika sinema za 3D.
Sasa kwanini wasitengeneze TV itayoji-convert yenyewe ili kuondoa ulazima wa miwani kwa kuweka kioo chenye teknolojia ya miwani katika TV yenyewe? .... wameshatengeneza kama alivyosema X-Paster.
Nadhani nimejibu sehemu kubwa ya ulichouliza.
Naomba tu nisisitize kuwa teknolojia hii ni pana sana kama alivyosema X-Paster hivyo maelezo niliyotoa ni sahihi (basing on my knowledge only). Tarajia kusikia mambo mengine tofauti-tofauti tegemeana na teknolojia husika.
All the best.