@3D
nimepata interest na mambo ya graphics miezi michache ya nyuma. Najaribu jaribu kujifunza lakini duh si mchezo kila fani ina wenyewe. Vipi Adobe Premiere Pro? ina fit vipi kweye hizo
Kingine nilikuwa ninapenda nitengeneze animation ya lile shairi la sungura na sizitaki mbichi hizi.( Nadhani unalijua)
Je utakubali kutoa dasara za hatua na taratibu kwa lugha nyepesi ninazotakiwa takiwa kufuata kufanikisha just simple animation ya ya hili shairi
ADOBE PREMIERE PRO
Adobe Premiere Pro, Sony Vegas Pro, Final Cut Pro, Avid ni professional editing software ambazo kwa kawaida hutumika kuedit (kukata vipande, kuvipanga, kuboresha rangi na mwanga etc) wa video ambazo zimerekodiwa location ama kutengenezwa na programu zingine kama za 3D etc.
Ukienda location kushoot video (sinema, muziki, tangazo) huwa kuna vipande visivyohitajika au vilivyorekodiwa vibaya ambazo itabidi viondolewe... hapo ndipo Premiere na wenzake huingia. Katika video za muziki, ukiwa location inabidi uu-play wimbo husika na msanii huigiza kuuimba lakini location huwa kuna kelele za upepo, magari, watu, ndege etc hivyo ukirudi kwenye kompyuta inabidi uoanishe flow ya uigizaji wa msanii kutokana na wimbo uliopigwa location na wimbo halisi wa kwenye CD ambapo baadaye sauti ya location huondolewa. Hapo ndipo Premiere na wenzake hutakiwa.
Program za 3D animation na nyingine za
compositing kama Adobe AfterEffects, Apple Shake, The Foundry Nuke, Autodesk Combustion etc hutumika kutengeneza vipande vifupi ambavyo huchanganywa na vipande virefu vya video ama sinema kwa kutumia Premiere na wenzake. Program nyingine za editing ambazo si high end ni kama Pinnacle Studio, Ulead Video Studio, Cyberlink PowerDirector, Adobe Premiere Elements, Windows Movie Maker etc. Hizi programs ambazo si high end huwa na templates kibao (Pinnacle Studio huwa na transitions zinazotumika sana katika video za harusi - usipoziweka watu watadhani hujui editing!) ambazo beginners huvutiwa nazo. Hata hivyo for simple editing, software za category ya Pinnacle Studio zinafanya vizuri tu.
VIJANA WENGI WANAOTENGENEZA VIDEO ZA MUZIKI (NAZUNGUMZIA TZ) HUTUMIA SANA ADOBE PREMIERE NA SONY VEGAS. AFTER EFFECTS INATUMIKA KIDOGO JAPO NI MORE POWERFUL NA IKO EQUIPPED KUFANYA EFFECTS AMBAZO NI MORE ADVANCED - INAHITAJI MUDA ZAIDI KUJIFUNZA KULIKO PROGRAMS ZA EDITING KAMA PREMIERE.
SIZITAKI MBICHI HIZI
Sijaelewa vizuri aina ya darasa nalotakiwa kulitoa. Kwa harakaharaka naomba niseme mapema "Sizitaki mbichi hizi"! Well, kutengeneza katuni pamoja na viumbe hai wengine huitwa character modelling/animation. Hadi dakika hii naandika hapa sijaweza kufanya character animation pamoja na kujaribu mara kadhaa. Hata hivyo najua what it takes to model and animate a character, japo kwa vitendo majaribio yangu hayajafanikiwa. Achilia mbali kuhuisha (animating) hata kuumba tu (modelling) ya character bado sijaweza, my wish however
"By December 2012 I must be able to model and animate a character."
Shairi za Sungura sizitaki mbichi hizi nalifahamu. Kwa majibu ya jumla ni kuwa ni lazima uandae sketches ambazo zitakuwa zinaambatana na hatua mbalimbali za shairi hilo. Sketches hizi humsaidia mhuishaji kujua poses, movements na views mbalimbali bila ulazima wa wewe kumsimamia au kumuelekeza kila hatua. Sketches hizi huitwa
Storyboard. Hivyo hatua ya kwanza ni storyboard then modelling and animation. Mwisho ni compositing (After Effects, Shake, Nuke etc) kama kuweka sauti na effects zingine kama upepo, radi, mvua etc. Baadhi ya software za 3D kama Blender na Maya zina uwezo fulani wa kufanya compositing.
Ila kama concern yako ni kutengeneza wewe mwenyewe.... naomba niongee lugha rahisi (kama ulivyosema)
ni lazima ujifunze basics za 3D na uchague software moja ya 3D among several (I would recommend Cinema 4D as I personally consider it easy to learn) but 3ds Max may be a good option too because it has so many tutorials on the web probably more than any other 3D software (Kotinkarwak may recommend Blender 3D) ili ujifunze hiyo. Generally, it is impossible kuanza directly kuanimate SUNGURA ikiwa hujui software husika ya 3D inafanyaje kazi kwa ujumla wake. Kumbuka mnyama kama sungura ana macho, ana masikio ambayo hucheza separately na mwili (itabidi ujue kumodel na kuanimate masikio), ana miguu, ana nywele ana mkia (ambao nao hutikisika separately). Vitu kama nywele tu huhitaji kujifunza specifically kwa kuwa kuna vitu kadhaa vya ku-consider. Usipojifunza haya utajikuta unatengeza kituko... mwenyewe utadhani umetengeneza sungura lakini watakuja watoto wa jirani halafu watakwambia "Umetengeza puto zuri"!
Kwa ujumla ni vigumu (almost impossible) kumwambia mtu ambaye hana idea na 3D generally na specifically software fulani eg Cinema 4D "Ili kutengeza masikio extrude polygons mara tatu then select the lowest edge then bevel it halafu the whole model ifanye iwe child ya hypernub (meshsooth)".
YOU'LL FIRST NEED TO GO THROUGH THE BASICS.
Othwerwise, 3D is generally interesting. Whether it is difficult or not..depends much on the level you want to attain na pia personal skills. Lakini pia bidii ya kutosha na kutokata tamaa husaidia. Start with simple things like modelling mobile phones, remote controls, chairs, tvs, bottles etc then go for more complex things like animals, humans and etc.
EXTRA
Nilinunua kitabu cha Adili na Nduguze cha Shaaban Robert kwa nia ya kukitengenezea sinema.. sijakata tamaa lakini kuna mambo kadhaa katika hadithi hiyo ambayo hadi sasa sijayaweza. Mfano kuna wakati Adili alinyakuliwa na tai mkubwa toka baharini alikotupwa na nduguze... kasheshe ni kumtengeneza huyo tai halafu kumfanya aonekane kambeba Adili (aliyezimia) juu juu huku akipiga mabawa naturally kama ndege arukavyo kwa kiwango kitachofanya watazamaji (including wewe Mtazamaji) wastaajabu wakidhani ni kweli na si "katuni tu." Mambo bado aisee. But one day yes kwa sababu
"Nazitaka mbivu hizi"!
Naamini nimejibu suala/swali lako.