Open Source softwate in advertisment marketplace

....................
...........................Niseme nimepata wivu sana ( sio mbaya hapana) teh teh teh teeeee


Usinionee wivu maana mimi si "mteule wa NEC." lol!! Pamoja Mkuu.

NB. Hoja ya "Uteule wa NEC" nimeitoa katika signature yako.
 
Aah Ah ah ah ah, nimeangalia hii itu kimakengeza nikawa nacheka peke yangu, hata ile yenye color distortion pia inakubali kidogo ila si kama hii ya pili, ila sasa waangaliaji ungewataadharisha wasije kuumia macho... lol!

Wa-China tayari wapo mbali, nadhani wao ndio wa kwanza kutengeneza 3D televisheni zisizo tumia miwani. 3DTV ya inch 42 yenye kutumia teknolojia ya LCD screen, bei yake mpaka sasa ni US dola $20,000.


Haya mkuu nimekusaidia kuongeza makengeza hapa chini:
attachment.php
 
Mkuu, kwanini msianze kujifunza vitu rahisi kama cartoon za 2D mfano wa The Simpson au Tom n Jerry Cartoon? ......................na baada ya jitihada nyingi kazi zao zimekuwa maarufu sana.......... Nahisi hata program zake si ngumu sana kiivyo.


Mkuu X-Paster nitajijibia mwenyewe, wadau wengine watajibu kwa wakati wao. Kwa ufahamu wangu 2D inasumbua sana ku-animate kuliko 3D. Kwa mfano kama umetengeneza umbo la dunia katika 3D ni rahisi zaidi kulizungusha kuliko kufanya hivyo kwenye 2D. Hata kwa objects zingine including binadamu ni vivyo hivyo. Jambo jingine ni kuwa 3D na 2D software zina-handle mambo kwa namna tofauti sana hivyo ni vigumu kuanza kwa 2D (hata kama ni rahisi) kwa makusudio ya kuhamisha knowledge kwenda kwenye 3D. Hata hivyo nikiri tu kuwa kui-master 3D inachukua muda sana kwa sababu inhusisha technicalities kadhaa.

Jambo jingine ni kuwa 3D animation haihusishi katuni tu bali pia vitu vingine kama nilivyoonesha katika clip niliyoanimate mapazia... naamini stages za ku-animate mapazia katika 3D ni chache kuliko 2D kama utajua tricks zake.

Suala jingine ni kuhusu Beauty. 3D inaweza kuachieve realism na hivyo products zake ni attractive kuliko za 2D. Binafsi natumia 3D si kwa malengo ya katuni tu lakini pia hata kwa graphic design.. kiwango ambacho kwa 2D nisingepata quality niitakayo kirahisi. Umaarufu wa katuni za akina Simpson na Tom and Jerry partly umechangiwa na content ya katuni hizo na promo na si beauty... hata hivyo kuanimate Tom and Jerry nahisi ni mziki mnene.

Mwisho ni kuwa sijajipa muda wa kutosha katika 2D hivyo si ajabu nina taarifa zisizo sahihi. Nitafuatilia. Asante kwa link ya Moviestorm.. nitajaribu kuicheki.. inaoneka iko promising.

Asante kwa ushauri.
 
..... ila sasa waangaliaji ungewataadharisha wasije kuumia macho... lol!

Wa-China tayari wapo mbali, nadhani wao ndio wa kwanza kutengeneza 3D televisheni zisizo tumia miwani. 3DTV ya inch 42 yenye kutumia teknolojia ya LCD screen, bei yake mpaka sasa ni US dola $20,000.

Aisee nilisahau kutoa tahadhari maana macho ya mtu yasije yakang'ang'ania kuwa makengeza forever. Ila pia ukifanya makengeza kwa muda mrefu macho yataanza kuuma. Asante kwa kuikuza picha.

Wachina pamoja na kwamba tunawapiga madongo lakini wako mbali sana kiteknolojia. TV ya 3D ya 42'' Samsung (ya kuvaa miwani) nadhani ni something like 3.5 M za ki-Tanzania kama sijasahau. Ila bei haiko tofauti sana na hiyo.
 
Katika ku'animate 2D, inabidi uandae picha 24 kwa kila sekunde, hii namaanisha kuwa, video itaonyesha picha 24 kwa sekunde ndio upate mwonekano wa video footage, ndio kuna software ambazo zinaweza kukadiria picha ifuatayo itakuwa vipi kati ya hizo 24 na kukupa fursa ya kuandaa intermideate photos lakini bado itabidi uzifanyie marekebisho mengi zote zitakazotayarishwa na software.
Kwenye 3D nadhani shughuli ipo kwenye kutayarisha "assets" zitakazotumika kwenye footage yako, kama vile, environment (miti, barabara, mawingu) na pia zipo functionality au software zingine ambazo unaweza kutumia kutengeneza hizo assets, kazi inayobaki ni ku'direct hiyo movie kwa ku'animate assets. Pia, assets hizi zinaweza kutumika tena, na tena hapo kupunguza muda utakaohitajika kutengeneza video yote.
Tukumbuke pia kuwa katika hii fani, kuna expertise tofauti kama vile animator, modeller, director nk ingawaje mtu mmoja anaweza kuwa na expetise zote...
Pia 3D software zinaweza ku'output in 2D mfano "2D in Blender 2.6 – Tutorial"
 
  • Thanks
Reactions: 3D.
Back
Top Bottom