DOKEZO Ongezeko la Wahamiaji na Usalama wetu: Je, Vyombo vya Ulinzi na Usalama Tanzania vimelala Usingizi wa Pono?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,432
11,100
Wasalaam nyote!

La mgambo likiliia ujue kuna jambo.

Mnisamehe kwa kuanza na utangulizi wa jazba yote ni maumivu ya uzalendo.

Tanzania ni nchi ya ajabu sana kila Jambo lipo kimazoea, nitoe rai na angalizo uhamiaji haramu kupitia mipakani hasa Mipaka na Malawi, Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda ni tishio kubwa sana mikoa ya DSM, Morogoro wilaya za pembezoni, Mtwara, Lindii na Ruvuma wilayani ama pembezoni.

Ni rahisi sana Wanyarwanda na Warundi kujificha kwa kivuli Cha wahaya na waangaza, ni rahisi sana Warundi kujificha kwa kivuli Cha Waha hasa kwa kujibatiza majina ya Hamis, Rajabu, Juma, Rashid kukwepa udadisi wa Uhamiaji (Sina Nia mbaya kabisa na utengamano wetu mapokeo yawe Nia njema). Ni rahisi sana Wamalawi kutumia kivuli cha makabila haya wanyakyusa kwa kiasi, waandali kwa wingi sana, Wanyasa na Wamanda kwa wingi sana,.

Kuhusu Wafipa, Wanyamwanga, na Wanyiha kwa Uhamiaji toka Zambia kwa Mikoa ya Rukwa na Songwe sina uhakika.

Pia tishio sugu la uhamiaji haramu wa wakenya mkoa wa Arusha na Wilaya kama Rombo na hawa ni wengi na vyombo havijali.

Kwa wqganda mpaka wa Mutukula uko porous hasa kivuli cha wahaya kwa waganda wq ukanda wa mpakani na hadi Masaka Uganda, Baganda, Banyoro na Batoro all these felas can click well with Luhaya or Kihaya. Huge task ahead us.

Nawaambia kwa sasa Tanzania iko uchi sana kutoa tahadhari ni uzalendo na mapenzi kwa nchi nawaambia nimejengwa hivyo toka utoto wangu tangu enzi za hofu dhidi ya Makaburu na mchango wa jamii katika kujihami na uvamizi.

Sitarajii mamlaka zifanye kupuuza na si katika dhana na tafsiri mbaya yq ubaguzi nawaambia nchi ni yetu na katika wajibu wa ulinzi na Usalama ubinafsi wa kiinchi na kijamii ni wa lazima sio hiari, hivyo andiko hili na haki ya kimsingi na wajibu wangu wa kikatibu kushiriki katika muktadha huo.

Kisingizio chochote kama cheap labour ya madanguro, ulinzi, nguvu kazi kilimo, Uyaya wa kulea watoto, Mapato ya kupangisha kwa wenye nyumba, Cheap labour kwa wauza maduka, cheap labour kwenye saloon za kike, kujistarehesha kingono isiwe chanzo cha upofu.

Nawasihi ujumbe ukawe mafuta ya baraka ya kufumbua macho na akili zq kiutendaji jumuishi na wajibifu, zenye muitikio wa haraka na mtambuko kwa serikali kwa ujumlq wake hasa Ngazi za mikoa, wilaya, katq, vijiji, vitongojiz mitaa, vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Kampeni maalumu kukemea ya kitaifa na onyo Kali la kitaifa dhidi ya kubweteka huku hatarishi.

Nawasilisha katika Mungu na nchi yetu Tanzania.

Karibu kwa michango, maoni na nyongeza.

I stand to be corrected.

Wadiz
 
Waacheni watu waje kwani shida yako Ni Nini hasa hutaki wageni hi nchi. Ya baba yako , issue za usalama wa Taifa waachie serikali
 
Ni majukumu yetu sote kutoa taarifa za wahakifu na uhalifu. Wahamiaji na wavushaji.
 
Back
Top Bottom