Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,400
- 4,074
Wadau nawasabahi,
Kama kichwa cha habari kilivyo, nitafurahi sana endapo Waziri wa Mambo ya Ndani Mwenyekiti wa Usalama barabarani Taifa na IGP na Kamishna wa Kikosi cha Usalama barabarani Taifa watalitolea ufafanuzi suala la hawa bodaboda kutokuheshimu Sheria za Usalama barabarani tena kwa makusudi mbele ya Askari wa Usalama barabarani na kusababisha ajali za makusudi ambazo zingeweza kuepukika.
Bodaboda wamekuwa;
1. Hawaheshimi taa za kuongoza vyombo vya usafiri barabarani.
2. Bodaboda wamekuwa wanakatisha popote watakapo hata kama Sheria za Usalama zinakataza.
3. Bodaboda wamekuwa wanabeba abiria zaidi ya 2 tena mbele ya Askari wa Barabarani lakini hawachukuliwi Sheria.
Je, ni kweli bodaboda wapo juu ya Sheria za Usalama Barabarani ndio maana hawachukuliwi hatua? Naamini ingekuwa wanaadhibiwa nadhani hata wingi wa ajali za bodaboda ungepungua kwa kiwango kikubwa lakini ndio kwanza zinaongezeka!
Bodaboda tiini Sheria bila shuruti. Tanzania bila ajali za bodaboda inawezekana.