Oneni utata jamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Oneni utata jamani?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by ndume, Jan 13, 2011.

 1. n

  ndume Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Baraza la kiswahili lilitumi vigezo vipi kuita majina yafuatayo kama ifuatavyo:
  mnyama mbwa badala ya kuita m'mbwa.
  Mbu badala ya kuita m'mbu.
  Nge badala ya kuita n'nge. Vilevile hata neno nje badala ya kuita n'nje.
  Naomba msaada kuhusu hizi ni kwa nini waliita hivi?
   
 2. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  acha tusubiri wataalam wakuje kumwaga elimu.

  lakini kwanini na wewe unaitwa ndume na sio n'ndume?
   
 3. n

  ndume Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwani wewe ujui maana ya ndume,wewe mbona unaitwa klorokwini
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Kiswahili kuandika na kutamka ni tofauti kama kilivyo kiIngereza. Ukitaka kutatuwa tatizo la kuandika na kutamka tumia herufi za kiarabu. Kiarabu kina vitamshi vinavyofanya kila neno ulisome kama linavyotamkwa hata kama ndio mara ya kwanza kulisoma hilo neno.

  Kumbuka kuwa historically kiswahili kilikuwa kinaandikwa kwa herufi za kiarabu na si za kilatini kama tufanyavyo sasa. Kuna baadhi ya wazee wa kiSwahili mpaka leo hutumiana baruwa za kiswahili kwa maandishi ya kiarabu.
   
 5. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  Khaaaaaaa.......mbona unalinganisha visivyo vya aina moja...??? Hayo maneno aliyoyaulizia yeye yanavyoandikwa na yanavyotamkwa ni tofauti kama ilivyo kwa maneno ya kiingereza
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,420
  Likes Received: 3,768
  Trophy Points: 280
  We unakoelekea......mnh haya........
   
 7. n

  ndume Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  sikiliza wewe kwani mimi nimekwambia mimi naitwa n'ndume? Mimi bwana naitwa Ndume bwana swala zima naomba majibu kwa sababu neno linavyoandikwa sivyo linavyotamkika.
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hapa tatizo ni kuwa maneno uliyoyataja na mengine kama hayo (ndio=ndiyo, kukua=kukuwa, ingia=ingiya, n.k), yako vilevile kama yalivyoandikwa kwa mara ya kwanza katika karne ya 19 na Johnson, na bado mpaka leo wataalamu wetu hawakufikiria ama kuyabadilisha au kutoa maelezo ya kuridhisha kwa nini yabakie hivyo.

  Nafikiri kwa kiasi kikubwa mambo mengi yamerekebishwa katika kamusi la kiswahili lililotolewa na Baraza la Kiswahili Zanzibar mwaka jana, lakini sina hakika kama maneno yote yenye utata yametatuliwa.
   
 9. Mwenzetu

  Mwenzetu JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 500
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Jamani acheni siasa mpeni Ndume majibu na kama hamna basi muwe wazi.Ndume nami nasubiri jibu,ila hata miye sijui baraza la kiswahili lilitumia kigezo gani
   
 10. n

  ndume Member

  #10
  Jan 18, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  mimi naona kama unanipigia hadithi sababu unakuwa unageuza mada hayo unayosema mimi sikuyauliza kwa kuwa yapo maneno mengine kama
  Mfano:1.Amenionesha ili neno linatokana na kitenzi Ona.
  2.Amenionyesha ili linatokana na kitenzi Onya.

  Kwa kumalizia watu wengi hutumia maneno hayo kwa kuyachanganya kwa kuzani kuwa yana ujumbe mmoja, kumbe yana jumbe mbili tofauti.

  Sasa mimi naomba majibu utata upo palepale ni kigezo kipi walichokitumia mpaka maneno hayo yawe tofauti jinsi ya kutamkika na kuandikika.
   
 11. Zing

  Zing JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 1,780
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  mhhhh eti kiswahili kinaandikwa kwa kilatini. soma history ya kitu kwanza. hizi herufi tunazoumia ni za kirumi au kiroma.

  hukuwiii kusema hata 1,2,3,4,5 ,6 ni kilatini

  ukitaka kujua kilatini original gonga hapa Latin Alphabet
   
 12. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Nakubaliana na wewe cku mmoja ililetwa barua ya Posa kijengoni kwetu lkn barua hiyo iliandikwa kwa kiarabu cha kiswahili,aisee nilipata tabu mpaka kuja kugundua kumbe hiki ni kiswahili ila kimeandikwa kwa herufi za kiarabu,mimi nilifikiri kilichoandikwa mule ni kiarabu ili niwatafsirie kwa kiswahili,basi ukawa ni mteremko tu nikawasomea posa yao na jamaa akaja kuchukua jike lake.
   
 13. sheri

  sheri Member

  #13
  Feb 3, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sautu za hayo maneno zipo katika matamshi na si maandishi............katika linguistic kuna process inaitwa ASSIMILATION dio iliyotu mika kuficha hizo sauti katika maandishi...
   
 14. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #14
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hapo kwenye bold ndo uwingi wa ujumbe?
   
 15. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #15
  Feb 4, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hizi namba tunazo zitumia asili yake si kilatini, namba zina asili ya herufi za Kiarabu na Kihindi.


  Source:


  Arabic numerals

  Eastern Arabic numerals

  Indian numerals
   
 16. m

  mjasiria JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 3,790
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sio uwingi ni wingi
   
 17. b

  bakarikazinja Senior Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 9, 2009
  Messages: 179
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kaka swali lako limejikita sana kwenye ngeli za majina hasa katika misimamo yote miwili ule wa kisasa na wakimapokeo na yote hiyo inatoka kutokana na upatanishp wa kisarufi
   
 18. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,130
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  kweli jf imevamiwa siku hiz haya mambo gani tenaaa hiv umepitia sekondari kweli wewe au mtaala ulikuta wameubadirisha
   
 19. b

  bwanafundi Member

  #19
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  hapa nakubaliana na wewe
   
 20. nkyandwale

  nkyandwale Member

  #20
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  :rain: Maandishi ni alama mojawapo ya lugha inavyowakilishwa. Maneno mengi katika Lugha ya Kiswahili ni yale yaliyosanifiwa enzi hizoooo! kwa sasa tukisema funguwa, onesha, sikiya, panguwa, siyasa.... wenye mtazamo wa sarufi kongwe, tunawaingiza katika mgogoro.
  Hivyo fonimu zinazo achwa katika maandishi, huu ni wakati muafaka kuyaandika maneno hayo na yale yafananayo yatendewe haki. Sasa funguweni masikiyo ili msikiye fonimu hizo zinavyo wachwa katika maandiko.
  Itachukuwa muda wa kuwabadilisha watumiaji wa abjadi katika kuunda maneno kutokana na vitamkwa. Je, ni siku gani ya usanifishaji mpya ili tujiandaye kuu-o-ndowa utata? Hapa hapatoshi. Ni wakti ni huu kwa wanataaluma na wazuwoni kusemeya haya. Ama sivyo Ndume? :director:
   
Loading...