- Thread starter
- #21
:rain: Maandishi ni alama mojawapo ya lugha inavyowakilishwa. Maneno mengi katika Lugha ya Kiswahili ni yale yaliyosanifiwa enzi hizoooo! kwa sasa tukisema funguwa, onesha, sikiya, panguwa, siyasa.... wenye mtazamo wa sarufi kongwe, tunawaingiza katika mgogoro.
Hivyo fonimu zinazo achwa katika maandishi, huu ni wakati muafaka kuyaandika maneno hayo na yale yafananayo yatendewe haki. Sasa funguweni masikiyo ili msikiye fonimu hizo zinavyo wachwa katika maandiko.
Itachukuwa muda wa kuwabadilisha watumiaji wa abjadi katika kuunda maneno kutokana na vitamkwa. Je, ni siku gani ya usanifishaji mpya ili tujiandaye kuu-o-ndowa utata? Hapa hapatoshi. Ni wakti ni huu kwa wanataaluma na wazuwoni kusemeya haya. Ama sivyo Ndume?
Hapo ndipo penyewe