On Star TV: Ipi Misingi ya Amani Tanzania? Sehemu ya 3

Jeshi la polisi wasingeweza kutokea kutokana na mada yenyewe ilivyo ingawa naamini saa hizi watakuwa wanafuatilia kwa makini sana. Wanaelewa kwa sasa wao watakuwa ni watuhumiwa wakubwa kwa yanayotokea sasa.

Nashauri jeshi la polisi lijisafishe kwa kutekeleza jukumu lake la kikatiba la Kusimamia Ulinzi wa wananchi na mali zao na sio wao kuwa mstari wa mbele kudhuru wananchi.
 
Kuna mama anatapika katika simu, anadai viogozi wa jeshi ndio wanajua sana...

CCM imeharibu sana akili zetu. Imagine mtu wa nje anatutazama na kutusikiliza. Mama analilia amani asiyoijua?
 
Wageni wetu wa leo wamejikitikita katika kutetea chama fulani na kuponda chama fulani, hata kama hawataji jina la chama au jina fulani akili ya kawaida inatutosha kung'amua mawazo yao, na naweza kusema bila kumung'unya maneno kwamba viongozi wa namna hii ndo wanao hatarisha amani.

Lazima tujue chanzo cha yote haya ni umasikini uliokithiri ndani ya jamii yetu na serikali kupitia chama tawala wameshindwa kutuondoa hapa na hawako tayari kukubali kwamba wameshindwa.

Watu tuwe tayari kuambiana yale tusiyopenda kuyasikia ndiyo njia pekeee ya kulikomboa taifa hili kinyume na hapo machafuko hayaepukiki.
 
Kumzomea au kumshangilia Kiongozi yote ni feedback. Anayezomewa anapaswa kujirekebisha pale alipokosea.

Polisi wamejifunza nini kutokana na maandamano ya Waislamu?

Star Tv tumewaambia; hao wazee hakuna kitu angalia sasa huyo anaitaja ITV kupitia Star Tv... Hiyo haikubaliki hata kidogo
 
Huyo mama aliyeongea ni kama waziri/mbunge fulani hivi, ingawa sijamfahamu naendelea kufanya uchunguzi kujua ni nani.
 
kuna mama antapika katik simu,andai aviogozi wajeshi ndio wanajua sana..ccm imaharibu sana akili zetu.Imagine mtu wa nje anatutazama na kutusikiliza.

Acha kupotosha... nyie ndio wale washabiki wakutia sumu katika akili za wakurupukaji na bendera fuata upepo bila kuuliza. Umemsikiliza, wafanyie haki Watanzania ambao hawajabahatika kusikiliza wajue kasema nini!

Kaongea ya msingi na namuungua mkono kwa kiasi fulani, ingawa kaegemea mno upande mmoja.
 
hu hu..mzee farijala kajumlisha ITV ktk list ya wabinafsi...at least katuambia kuwa ndiyo TV worth it.
 
Wewe mama wa Morogoro, hata vyama vya kisiasa vipo kisheria na vina hadhi, hivyo navyo viheshimiwe na viachwe vifanye kazi zao kwa mujibu wa kikatiba.

Yaani huyu mzee mwanajeshi mstaafu, ni mchemfu, sasa hapo ITV imeingiaje? Mr. Yahya uwe unaleta wazee wenye akili timamu!
 
Mzee Farjala kaniacha hoi, kachanganyikiwa kabisa na kaanza kuirushia ITV matusi.

Naona Yahya anaweka hali sawa kwa kuiomba ITV radhi kwa huyo mzee kupotoka.... mzee anazeeka vibaya kwa kweli.
 
Wanaposema kutii sheria ya nchi, wakati sheria hizohizo kwa makundi mengine sheria zinatumika na kwa wengine hazitumiki, hapo ndo tutaonana wabaya! Haki haki haki ndo mpango mzima!
 
Back
Top Bottom