On Star TV: Ipi Misingi ya Amani Tanzania? Sehemu ya 3

Sheria inasema atakayekiuka sheria ya polisi na kufanya mkutano usio na kibali wanatakiwa kufikishwa mahakamani na wakipatikana na kosa wanapigwa faini ya mpaka 50,000.

Je ni wangapi waliofikishwa mahakamani na polisi?

Ni wangapi walipatikana na hatia na kufungwa au kupigwa hiyo faini?

Na kama hawajafikisha mtu mahakamani na wameua kwa visingizio vya kufanya mikutano isiyo na vibali je hawaoni wao ni wa kwanza kutokufuata sheria?
 
(Si ya kusoma)
Mkuu Yahya leo mmechemka sana kutuletea hao makada wa CCM. Mmeshindwa ku balance mjadala wa leo. Mzee Falijara na mwenzio ni wanachama wa CCM, nashauri mjirekebishe

Asante Mkuu
 
Mjadala umepooza hasa dar kwani wazee waliopo wanajaribu kuupinga ukweli.

Kujaribu kutuaminisha kuwa vyama ndivyo vinaharibu/vinavunja amani, kwa kutokutii amri za kipolisi hata kama amri hizo ni kandamizi?

Mfano wa hali iliyotokea hivi karibuni wauumini wa kiislam wameandamana mara mbili bila kibali lakini hawakuvunja hata glass na polisi hawakuingilia na amani ilikuwepo polisi wakiingilia ndo tunaona uvunjifu wa amani.

Polisi/serikali ndi inachangia uvunjifu wa amani kwa kutende kwa upendeleo.
 
Nilipo tune star tv ghafla nimekutana na mzee anakomaa, povu linamtoka, mishipa ya uso na shingo imesimama eti mwanajeshi mstaafu ila sasa anachoongea its non sense utumbo tu.

Hoja mlegezo zisizo na mashiko,hao wazee they beat around the bush, kiukweli kipindi leo kimepwaya
 
Yahya, I'm always in your truck.

Kwa leo hawa wazee siyo: ni bora akina Lissu na Nape wangerudi kujibu hoja zetu na maswali tuliyo uliza kwenye sehemu ya kwanza ya mada hii; kwani wakiwa live studio hawakuweza kuzijibu zote kwa maana ya muda na ukatuahidi kwamba watazijibu kupitia kwenye mitandao yetu kitu ambacho hakikufanyika.

Alafu; Hivi kwanini Polisi siku zote kwenye vitu vya msingi hawajitokezi lakini wakisikia Vyama vya upinzani wanafanya Mikutano yao wanajiweka msitari wa mbele?
 
(si ya kusoma hewani)

James Range,

Uteuzi wa washiriki wako Dar hawajadili mada na hata maswali unayowauliza hawajibu bali wanongea hisia zao tu ambazo ni za kulibeba Jeshi la Polisi.

Waaulize Daudi Mwangosi alivunja amani gani mpaka kauawa kinyama vile?
 
Tanzania tumeipokea demokrasia bila kuweka misingi ya hiyo demorasia ktk kuisimamia amani yetu, ukweli ni kwamba amani itakuwa ni ndoto ikiwa kikundi fulani ktk jamii kinadhani wao ndio pekee wanaopaswa kuwatawala wengine.

Wazee muwe na busara ya kukemea haya na sio kuangalia upande mmoja tu.

Hussein Kamtwanje nikiwa Mtwara Tanzania.
 
mzee anakataa vitu obvious.Mpangilio wa maneno yake ,kwa mtu anayefutilia siasa za nchi na tabia za watu ni wazi alichosema mzee sio siri hata kidogo.
 
Katiba ya nchi inatamka wazi kuwa sheria yoyoyte inayopingana na sheria mama hiyo itakuwa batili. Sasa tunaomba watupe ufafanuzi kuhusu sheria hizi:
1. Katiba inataka yeyote anayetaka kuandamana au kufanya mkutano atoe taarifa polisi saa 48.
2. Sheria ya jeshi la polisi linasema anayetaka kufanya hivyo aombe kibali polisi.

Swali: Ni sheria gani batili hapo,je tuifuate ya katiba au ya jeshila polisi?
Yahya usiposoma huu ujumbe studio ntamuomba Mod wa leo akupige ban angalau ya dakika mbili tu, hili ni swali muhimu kabisa kwa hao wazee kulielezea.
 
Last edited by a moderator:
Mzee Farijala hajajibu swali...Mtu asipotii sheria adhabu yake ni kupigwa risasi? Hawa wazee wanasema tusitaje Chama cha siasa wakati wao kwenye mazungumzo yao wanavilenga vyama vya siasa
 
(Si ya kusoma hewani)

Yahya, kuna mchemsho Dar.

Hawa wazee tukubali tu niwazee wetu na kwa sababu ni wastaafu wameshaingia woga wa maisha ila kwasababu tunawaheshimu tunaomba usiwaite tena, tutafutieni wanaoweza kuendana na changamoto za sasa.
 
Wakuu hii pia ni reflection nzuri kupata uhalisia wa kundi Fulani Lina mtazamo gani kuhusu Amani ya Tanzania. Kwa mliopo field kwenu hii ni sample nzuri. Sikubaliani na wanaolaumu sana selection. Wekeni hoja tuwape wazee challenge.

Tutakuwa na part four ya hii mada

Maxence Melo kafanya kazi nzuri hapo juu. Hii itaandika historia
 
Nimkumbushe Mzee Farijala kuwa hata yeye atazomewa ikiwa maoni yake ndio hayo. Huu sio wakati wa HEWALA BWANA na NDIO MZEE. Tunahoji, tunatafakari na tunachukua hatua.

Policcm ni chanzo cha vurugu. Kama shida ni mikusanyiko, mbona nimetoka kukusanyika KANISANI na hakukuwa na fujo yoyote?

Fikra huru sizitegemei kutoka katika ubongo wa mtu aliyetumikia jeshi kwa miaka kadhaa. Yeye amezoea amri, na haijalishi kama ni ya haki au lah, maadam imetoka kwa AFANDE. Sisi ni wananchi, hatuambiwi kwa amri bali kwa hoja.

Kama wanaamini kuna wenzetu wamestaarabika, basi na ajue ni kwa wenzetu hao hao ambapo polisi hawezi kumshambulia mwandishi kwa mateke na marungu zaidi angemkamata na kumfikisha kwenye sheria.

Kwa akili za jeshini yaweza kuwa sawa, lkn kwa CIVIL RIGHT ni fadhaa kubwa kwa polisi 8 wenye mafunzo ya kijeshi, wakiwa na marungu na bunduki kumshambulia mwandishi m1 mwenye kamera kwa mateke, ngumi na marungu na hatimaye kumuua. Hii ni dalili kuwa mikono inafanya kazi ya ubongo. Endeleeni kutetea udhalimu mpk utakapotokea kwa watu wa familia zenu.

Hata Gaddafi aliweka utawala wa mabavu kwa miaka, lkn wakati ukifika, wananchi huchukua nchi yao.
 
Vijana wetu sasa wana upungufu wa histori ya nchi.

Viongozi wote wa siasa wanataka umaarufu! Hawana roho ya kweli ya kuwakomboa watanzania. Amani ya nchi kwa sasa inatoweka. Fikiri mpaka kwenye misiba siasa zinaingia. Tutapona.
 
Mkuu Yahya leo kidogo mmeteleza,haiwezekani muwaalike studio watu wenye mtazamo mmoja! Majadiliano yao yanakosa mvuto kabisa.
 
Yahya..hawa jamaa uliowaalika kwenye hiki kipindi hawafai.
Na mtangazaji mwenzako wa dar anapwaya hawezi kuwabana hao wazee wakajibu maswali ya msingi waliyoulizwa.
 
Kama viongozi wote wa dini wangekuwa kama hawa waliopo Mwanza, haya matatizo yasingekuwepo.

CCM inaeneza udini na imefanya kuwa mtaji wao, na baadhi ya viongozi wa dini wamejiingiza humo na kushabikia udini.
 
Mjadala umepooza hasa dar kwani wazee waliopo wanajaribu kuupinga ukweli.

Kujaribu kutuaminisha kuwa vyama ndivyo vinaharibu/vinavunja amani, kwa kutokutii amri za kipolisi hata kama amri hizo ni kandamizi?

Mfano wa hali iliyotokea hivi karibuni wauumini wa kiislam wameandamana mara mbili bila kibali lakini hawakuvunja hata glass na polisi hawakuingilia na amani ilikuwepo polisi wakiingilia ndo tunaona uvunjifu wa amani.

Polisi/serikali ndi inachangia uvunjifu wa amani kwa kutende kwa upendeleo.

Duuh, uDC umeshawakosa sasa watafanya nini tena? labda inawezekana baada ya kipindi hiki huenda wakafikiriwa.
 
Back
Top Bottom