On Star TV: Ipi Misingi ya Amani Tanzania? Sehemu ya 3

Yahya Mohamed

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
270
317
Salaam wakuu

Katika muendelezo wa mjadala juu ya Amani ya Tanzania, Leo tupo katika sehemu ya Tatu na lengo lilikuwa kuzungumza na Viongozi wa Dini na Jeshi la Polisi.

Viongozi wa Jeshi la Polisi wametoa udhuru na tutajaribu tena JUMAPILI ijayo.

Dar wapo:
Mzee Salum Jazaa - mstaafu JWTZ
Mzee Juma Farijala - Mwananchi Mkazi wa Dar

Mwanza wapo:

Sheikh Hassan Kabeke - m/Kiti JUKUSUTA
Mch.Garlod Deuli - akimwakilisha M/Kiti umoja wa Makanisa Mkoa wa Mza

Karibuni kwa mjadala!

Kwa kumbukumbu:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...r-tv-ipi-misingi-ya-amani-sehemu-ya-pili.html
&
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...ipi-misingi-ya-kuendeleza-amani-tanzania.html
 
Mwambie mzee Farijala kuwa jeshi la polisi lipo linafanya kazi kisiasa na sisi wanachi tunaona na kusikia. Dunia ya sasa si ya zamani na vilevile hakuna kosa kumshangilia mtu au kumzomea katika katiba ya tanzania.
 
Ukweli ni kwamba hao wazee wote hapo wanaongea vitu ambavyo ni ukweli lakini wanaingiza na propaganda nadani yake, kwani wanashindwa kusema ukweli juu ya chanzo cha uvunjifu wa amani Tz ambacho huwa ni serkali (CCM) kulitumia jeshi la polisi kisiasa na ushahidi ni kwamba hata yule RPC Shilogile wa morogoro alitamka wazi kwamba kamwe CHADEMA haitachukua jimbo la Morogoro Mjini akiwa yeye yupo, sasa hapo utaona kabisa ukweli uko wapi.
 
Wachangiaji we mjadala star tv Leo wanapwaya sana. Wamekaa Kuitetea serikali
 
Swali kwa Mstaafu wa JWTZ:

1. Anaposikia amani, nini tafasiri yake?
2. Amekuwa askari na bado ni askari. Kwanini askari hufundishwa kutii amri za wakubwa wao? Nini madhara yake?
3. Wanajeshi ni watu wa kujichukulia sheria mkononi, kosa dogo linalohtaji maelewano, wao hutoa kipigo na mateso makali. Kwa nini iko hivyo? Ndivyo wanavyofundishwa?
4. Natamani ningejua amestaafu na cheo gani, kwani kuna waraka ningetaka kuujua kwake.
 
Ni vizuri sana Yahya umewaalika hao makada wa chama chetu ili watusafishe.

Swali langu kwa Mzee Farijala ni kuwa;

  1. Anaunga mkono nguvu kubwa ya polisi inayotumiwa kudhibiti wanaoandamana?
  2. kwani sheria inasemaje kuhusu mtu anayeandamana hata mara baada ya jeshi la polisi kukataza?
  3. Je, adhabu ya mtu anayeandamana ni kumuua?
  4. je, kulinda amani ya nchi kunakofanywa na jeshi la polisi ni kuua raia ambao hawana silaha yoyote?
Nitafurahi kama ntapata majibu...

Mtego wa Noti!
 
Yahya habari,

(Usisome hii hewani)
Naomba kueleza maoni yangu, Kwa kweli leo kipindi hakina mvuto, kule Dar mmetafuta wananchi ambao wanajulikana msimamo wao, wazee wako biased, wote wawili ni anti-opposition, sioni kama kuna la maana watajadili zaidi ya kulaumu wanasiasa wa upinzani kwamba ndio chanzo cha ukosefu wa amani. Inajulikana wazi kwamba polisi ndio huingilia mikutano ya wapinzani na kuanzisha vurugu, hawa wazee hata kugusia ushiriki wa polisi kwenye uvunjifu wa amani.

Binafsi nasubiri polisi na viongozi wa dini nifuatilie mada.
 
Naomba waulize hao makada wa CCM kuwa maandamano ya kidini ya kiislamu huwa yanapata wapi kibali?

Vipi kuhusu makundi mengine ya kijamii ambayo yanaandamana pasipo kibali ?
 
Katiba ya nchi inatamka wazi kuwa sheria yoyoyte inayopingana na sheria mama hiyo itakuwa batili. Sasa tunaomba watupe ufafanuzi kuhusu sheria hizi:
1. Katiba inataka yeyote anayetaka kuandamana au kufanya mkutano atoe taarifa polisi saa 48.
2. Sheria ya jeshi la polisi linasema anayetaka kufanya hivyo aombe kibali polisi.

Swali: Ni sheria gani batili hapo,je tuifuate ya katiba au ya jeshila polisi?
 
Msingi wa amani Tanzania uko ndani ya katiba yetu kama ilivyosemwa na mwanajeshi mstaafu.

Katiba inatoa haki lakini pia upo wajibu.

Katiba hiyohiyo pia inasema wazi kabisa kuwa mtu unapotekeleza haki yako hairuhusiwi kuingilia haki ya watu wengine.
 
kuna mtu anajifanya kuwa yeye si polisi ila anaongea kwa mitizamo ya polisi.Ningeomba aulizwe kama anjua conventional wisdom..hao polisi hata kama hawatoshi ila kwanini kwa CDM ndio wakosekane?
 
Kaka Yahya waulize,

Hivi wanafahamu kwamba sisi watanzania wa leo tunaelewa sana. Na jeshi la polisi (si JWTZ) linatumika na wanasiasa.

Sisi vijana tunasema hapana kuonewa.
 
Dar wapo
Mzee Salum Jazaa - mstaafu JWTZ
Mzee Juma Farijala - Mwananchi Mkazi wa Dar

Karibuni kwa mjadala

Yahya, hawa walioko studio ya Dar wanapaswa kuelewa hii sio dunia ya kale. Hizi si siku zile walipoingia jeshini wakiamini ni fadhila. Tanzania ya leo ina watu makini wenye kulichambua jambo.

Hakuna mtu aliyezaliwa mkorofi. Ukorofi huja pale mtu anapoona haki yake ya msingi inakiukwa. Mimi sioni mantiki ya wao kuwa wasemaji wa uzuri wa polisi ambao watu wengine hawauoni. Sisi si watoto wadogo au majuha wa kusimuliwa tunachokiona. Naomba niwape mfano mmoja wa namna jeshi linavyotumika kisiasa na kuwa chanzo cha fujo:

Miezi fulani hapa nyuma kulikuwa na mashindano ya mpira wa miguu hapa DAR, sikumbuki ya nini lkn yalihusisha timu za taifa mbalimbali za hapa Afrika. Moja kati ya washiriki walikuwa ni KENYA. Wakati mashindano haya yakiendelea, WANAHARAKATI waliazimia kufanya MAANDAMANO YA AMANI kupinga jambo fulani (kama sikosei ni issue ya madaktari).

Jeshi la polisi lilikataza maandamano yale, likidai kuwa tupo kwenye tishio la Al Shabab. Kwa ubabe na nguvu yale maandamano hayakufanyika, kigezo AL SHABAB. Wakti huo huo, ndani ya Uwanja wa Taifa, watu takribani 65,000 walikuwamo wakiiangalia timu ya KENYA ikicheza mpira.

Swali langu kwa Salum Jazaa na Juma Farijala; Kwa akili tu ya kawaida, na kwa kuzingatia ugomvi wa Kenya na Al Shaabab, wapi palikuwa most likely to be attacked by Al Shabab, kwenye maandamano ya Watanzania au Timu ya Taifa ya Kenya ambao wana ugomvi nao?

Waelewe tuna akili zetu na tunafikiri. Hakuna nidhamu inayofundishwa kwa uonevu na kunyang'anya haki.
 
Kauli mbalimbali za wanasiasa ndio kichocheo kikubwa cha vijana wa sasa kutotii sheria za nchi. Wanasiasa wanapoanza kuvunja sheria unatarajia nini?

Wao ndio wamepitisha halafu wanakuja kwa wananchi kusema sheria ni mbovu. Niseme tu kuwa hapa kinachofanyika ni kuwahadaa wananchi ili kupata umaarufu tu. Sheria zikifuatwa sidhani kama amani itatokea.
 
Yahya,

(Si ya kusoma hewani)
Mjadala huu kwa majuma mawili yaliyopita ulikuwa mzuri ila Leo umekua hovyo sababu ya kuleta watu wenye ITIKADI moja "makada" so hakuna Mawazo ya changamoto ni one sided debate..... Kutokana na mazungumzo hayo Nina maswali kazaa kwa Hao wazee

(waweza kusoma)
Je, hatua ya Jeshi la polisi kuingilia haki ya kikatiba ya Watanzania ya kutoa maoni, kuandamana, na kupata habari ni sawa?
Je, ni Sheria gani inayowaruhusu polisi kutoa kibali CHA maandamano?
Je, wameshafatilia sehemu zote ambazo mauwaji yametokea nani alikuwa CHANZO?
Na je, kama wanasiasa ni CHANZO kama wanavyotaka kutuaminisha kwanini sehemu ambazo polisi hawa kujiingiza Kumekuwa na Amani?
Je, wanajua kuwa polisi wanatumia Sheria ya kikoloni?

NB. HAO WAZEE WAKAE WAKIJUA KIZAZI CHA DOT.COM TINAJUA MBIVU NA MBICHI NA SEHEMU AMBAYO HAKI YETU ITAKIUKWA TUTAFIGHT KUIPATA HAIJALISHI WATAWEKA PROPAGANDA HATA HIZI STRUGGLE SASA NI SABABU TUNAJUA WAJIBU NA HAKI ZETU "ni bora vita inayotafuta haki kuliko Amani inayopumbaza"

 
Ipi misingi ya amani Tanzania?

Misingi ya amani ni katika uwazi na ukweli jambo ambalo limekua adimu sana katika serikali na uongozi wa sasa.

Na kinachoitia amani ya tanzania majaribuni ni siasa uchwara za waliopo madarakani na wanao taka kuingia madarakani.

Polisi wanatumika kisiasa, na watendaji ambao sio wana siasa nao wanatekwa na wanasiasa. Kwa kweli ni jambo baya sana kwa siasa kuingila kila mahali...

Ikiwezekana kuitenganisha siasa na mambo mengine kama dini na utendaji.
 
kauli mbalimbali za wanasiasa ndio kichocheo kikubwa cha vijana wa sasa kuto tii sheria za nchi. Wanasiasa wanapoanza kuvunja sheria unatarajia nini. Wao ndio wamepitisha halafu wanakuja kwa wananchi kusema sheria ni mbovu. Niseme tu kuwa hapa kinachofanyika ni kuwahadaa wananchi ili kupata umaarufu tu. Sheria zikifuatwa sidhani kama amani itatokea.

wewe chunga kauli zako,usifikiri ni enzi za chama kushika hatamu
 
Mzee Farijara na huyo mzee mwenzio naomba mtufahamishe, Polisi kazi zao ni kukamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani, iweje waanze kujitwalia sheria mikononi na kuwaadhibu watuhumiwa?

Kote walikoua watu, watu hao hawakuwa na silaha yoyote mikononi mwao, kwanini polisi waliwaua badala ya kuwakamata na kuwafikisha mahakamani?
 
Asalaam Aleykum kaka Yahya,

Awali ya yote naomba nijenge hoja yangu kuwa AMANI ktk nchi yetu ya Tanzania imejengeka ktk misingi ya HAKI na USAWA kwa wote...

SWALI kwa wazee wangu walioko DAR...

Je HAKI kwa Wananchi wote ipo kwa sasa?

USAWA ktk mgawanyo wa pato la taifa UPO? Je ni kweli kuwa mwanasiasa aliependekeza kujitenga kwa jimbo lake kutokana na kubaguliwa anakera saana kuliko MAFISADI wanaoendelea kuitafuna nchi hii bila huruma?

Bilioni zilizowekwa Uswiss hao wazee haiwakeri?

Je ni kweli kuwa inakera sana kwa waziri mkuu kuzomewa kwa kuwaambia vijana warudi vijijini walikokimbia hali ngumu ya maisha ilihali wao wanatembelea mashangingi yenye viyoyozi na kushindwa kuwanunulia hata mikasi ktk hospitali zetu?

Kwa Mtazamo wangu AMANI ya NCHI yetu inatoweka kutokana na kuongezeka kwa GAP kati ya WANANCHI MAFUKARA na WATAWALA WACHACHE WENYE UTAJIRI unaotokana na UKUWADI wa RASILIMALI zetu...

Muda si mwingi wananchi hawatawaangalia na kuwashangilia hawa watawala kwa kuendesha magari mazuri, kamwe hatutajali suti zao za hariri wakati wamewatelekeza ktk kila nja za kijamii...
 
Back
Top Bottom