On Star TV: Ipi Misingi ya Amani Tanzania? Sehemu ya 3

Yule msela wa Dar aongeze ukali kidogo,,,anayesupport maasi ya CCM hana rafiki,,,

Chanel ten + Star tv + ITV+ Mlimani TV + EATV + BBC + DW + VOA + DTV+ ATN vs TBC = ????

TBC sasa hivi haina tofauti na vijarida viawandikavyo akina Diamond na Sepetu, au kipande cha gazeti ambacho wavuta tumbaku hutumia, au hata vipande ambavyo watu wa vijijini hutumia badala ya toilet paper.

Mlimani TV hawana coverage kubwa na bado CCM wanaweza ingiza mikono.

EATV watawamaliza TBC kwa ze comedy+musics .

ATN mpira na upande wa pili CCM hawawezi wapeleka wazee wa dar kwani si unajua wale jamaa wana vivua vile vikofia.ITV kile kipindi cha dkk 45 si interactive na kimekaa sana kama vile mtangazaji kakaribishwa nyumbani kwa mshiriki, Ila akisimama Masako magamba hutamani nchi ipasuke,utadhani wameingia ktk interview wakitokea disco.

Hao akina BBC + wengine ndio kabisa hawafagilii CCM tangu enzi, wanahitaji nchi kwa umuhimu wake kwa hii kanda na inabidi fanya kazi na ccm kwa convenience tuu.

CCM na polisi wamejenga perfect environment habari zao mbaya kwa upande wa raia ziripotiwe vivuri sana wakati zao za kupiga zikiandikwa bila mvuto au kupewa kakurasa kadogo sana kam zi kufichwa ndani.
 
Yahya umeonyesha busara na weledi wa hali ya juu kuiomba msamaha ITV.

James Range alipswa kumzuia yule Mzee kutaja chombo kingine cha habari kupitia chombo cha habari.

Hongera sana Yahya Mohamed kwa jinsi unavyoendesha mijadala Star TV

Yahya Mohamed ni hazina Star TV lakini ni hazina kwa mustakbali wa Taifa letu hasa kuwa mtangazaji wa kwanza kurusha maswali ya wana JF hewani! Akifikisha umri wa akina Jenerali Ulimwengu atakuwa ni zaidi ya mtangazaji!
 
jenista muhagama,ana kilango,beatrice shelukindo,sofia simba hawa mmoja wapo alikuwa ndiye aliyejiita zahra wa morogoro.
hawa pamoja na mamlaka waliyonayo kwenye chama chao bado wanaficha majina na kusaport uozo.
kweli ccm hakuna kiongozi kule.
 
Kauli mbalimbali za wanasiasa ndio kichocheo kikubwa cha vijana wa sasa kutotii sheria za nchi. Wanasiasa wanapoanza kuvunja sheria unatarajia nini?

Wao ndio wamepitisha halafu wanakuja kwa wananchi kusema sheria ni mbovu. Niseme tu kuwa hapa kinachofanyika ni kuwahadaa wananchi ili kupata umaarufu tu. Sheria zikifuatwa sidhani kama amani itatokea.

kauli za maisha bora yakawa bora maisha nazo zimechangia sana
 
Yahya Mohamed ni hazina Star TV lakini ni hazina kwa mustakbali wa Taifa letu hasa kuwa mtangazaji wa kwanza kurusha maswali ya wana JF hewani! Akifikisha umri wa akina Jenerali Ulimwengu atakuwa ni zaidi ya mtangazaji!

Yahya hawa wazee wanaweza kuhatarisha amani ya nchi kwa kauli zao, Eti ITV....Hapo kweli unategemea kupata busara kweli? Tunazungumzia misingi ya amani ITV wamekujaje hapo, Next time changanyeni watu wa umri tofauti, hicho kizazi cha wazee kama hao hakina jipya, kiko nyuma miaka 47 iliyopita enzi hizo akiongea kiongozi hata kama ni pumba watu walipiga makofi, sio leo, ukichemka watu watasema tu
 
...hao wazee akili zao zimeisha kuwa used...hakuna la maana waliloonge zaidi ya blabla tu...juma pili ijayo tuleteeni wazee kutoka mikoa mingine tupate maoni tofauti...
 
Hata mimi niliistukia ile sauti ya Mama aliyejiita ni Zahara kutoka Moro na hakika aliwaunga mkono wale wababa wa Dar hadi kichefuchefu. Kiukweli nimeifananisha ile sauti na yule Mh. Jenista wa Peramiho.

Huyu mama anataka kutuambia polisi kuua ni sawa? maana anasema Wamechokoza nyuki, kwanza ni kina nani wamechokoza nyuki? ni wananchi au waandishi wa habari, na hilo jeshi la polisi liko kwa kuwalinda kina nani?, ni maswali ambayo kila mtu anaweza kujiuliza, Tanzania tuna watu akili zao ni afadhali watoto wa chekechea, yaani mtu anaongea utafikiri anatumia fikra za wapi ha inachosa sana sijui tutabadilika lini, safari naiona ndefu sana
 
"Wazee wa Dar" leo wame-reflect aina ya wazee wa Dar waliompokea Mwalimu miaka ileeeee ya kupigania Uhuru kama inavyosimuliwa katika Makala za Mohamed Said. Ha ha ha ha ha.

"Wazee wa Dar" leo wame-reflect aina ya watu wa Dar katika harakati mbali mbali za kisiasa nchini mwetu katika kumkomboa mwananchi wa kawaida.

Hakika, "Wazee wa Dar" leo wame-reflect mawazo ya watu Dar; aina ya watu wa Dar ambao Rais wetu hupenda sana kuongea na Taifa kupitia kwao anapotaka kuzungumzia masuala MAZITO ya kitaifa.

Hao ndio wazee wa Dar; mahali panapoaminika pameendelea zaidi, pana wajanja zaidi, na watu wake wameelimika zaidi kuliko sehemu nyingine yoyote ya nchi yetu.

Hiyo ndio Dar ambayo nilidhani wazee wake wana busara kumbe ni kwa sababu hawapati nafasi za kuongea kwenye media otherwise hamna kitu. Kweli Dar ni nouma.

Hicho kizazi kina matatizo sana, unajua wao wameshiba kwa hiyo wanaona mambo yaendelee hivihivi, wanasahau kuwa kundi kubwa linaishi maisha ya taabu, halafu wanajifanya wanaijua amani sana, watu kama hawa hawapaswi kupewa nafasi yoyote ya kuongea kwani hawana hata chembe ya busara, wamenibore sana
 
Nimekuta kipindi kinamalizikia ila maoni yangu siku nyingine hawa wadau wapewe mada siku mbili kabla ili wajiandae pia wapewe DO and DON'T unapokuwa hewani LIVE maana kuna mgeni mmoja kiukweli alinekera sana pale alipokitaja kituo kingine cha tv bila sababu na hii ikanionyesha hana uvumilivu hata kidogo pindi anapotofautiana na watu (kwa mfano wa mzee huyo inaweza ndio ikawa vivid example ya CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA AMANI kwa viongozi kutosikiliza kilio cha wananchi na kuwa mbogo pindi wanapokuwa na maono tofauti)
 
Mkuu in short unapendekeza kuwe na ile kitu inaitwa rehearsal kama kwa graduands siku moja kabla hawajapokea shahada zao! Linaweza kuwa wazo zuri lakini tatizo ninaloliona MAGAMBA hayafundishiki ndugu yangu.

Wamefunikwa mno na UNAFIKI na UONGO; ndilo tatizo lao kuu. Magamba wako tayari kuita kinyesi keki badala ya jina lake halisi na hii inawagharimu sana.

Siku zote ukweli kutoka moyoni hauhitaji rehearsal ya aina yoyote kwani hujishuhudia wenyewe bila nguvu zozote za ziada.
 
Hata mimi niliistukia ile sauti ya Mama aliyejiita ni Zahara kutoka Moro na hakika aliwaunga mkono wale wababa wa Dar hadi kichefuchefu. Kiukweli nimeifananisha ile sauti na yule Mh. Jenista wa Peramiho.

Ile sauti ya mama Shelukindo, nilivyosikia tu anaongea nikakumbuka mjadala wa Jairo. Tone na spidi ile ile, Mhagama anaongea pole pole kiasi.

I stand to be corrected.
 
Mkuu in short unapendekeza kuwe na ile kitu inaitwa rehearsal kama kwa graduands siku moja kabla hawajapokea shahada zao! Linaweza kuwa wazo zuri lakini tatizo ninaloliona MAGAMBA hayafundishiki ndugu yangu.

Wamefunikwa mno na UNAFIKI na UONGO; ndilo tatizo lao kuu. Magamba wako tayari kuita kinyesi keki badala ya jina lake halisi na hii inawagharimu sana.

Siku zote ukweli kutoka moyoni hauhitaji rehearsal ya aina yoyote kwani hujishuhudia wenyewe bila nguvu zozote za ziada.

Kweli KUTOKA MOYONI HAUHITAJI REHEARSAL maana una flow tu nondo lakini kwa design waliotuletea leo walihitaji rehersal maana mtu mzima ana panic na kufanya conclusion kabisa kwamba waangalie TV flani ndio huwa ina mawazo kama watu wa mitandao wakati huku kwenye mitandao ndio chimbuko la hoja hata kama zikiwa kinyume na matakwa ya wengine au viongozi. Hii inanikumbusha siku mjomba Mkutugenzi wa Michezo ndugu Leonard Thadeo alivyo-panic kisa hoja za yule mdau wa riadha Bidabudai
 
Nimekuta kipindi kinamalizikia ila maoni yangu siku nyingine hawa wadau wapewe mada siku mbili kabla ili wajiandae pia wapewe DO and DON'T unapokuwa hewani LIVE maana kuna mgeni mmoja kiukweli alinekera sana pale alipokitaja kituo kingine cha tv bila sababu na hii ikanionyesha hana uvumilivu hata kidogo pindi anapotofautiana na watu (kwa mfano wa mzee huyo inaweza ndio ikawa vivid example ya CHANZO CHA KUPOROMOKA KWA AMANI kwa viongozi kutosikiliza kilio cha wananchi na kuwa mbogo pindi wanapokuwa na maono tofauti)

Mkuu upo sahihi..ila kiti maalumu CCM ni chukizo la taifa.Ni aibu taja mama zetu kama kti maalumu.Huwa wataanza vizuri ila baada ya sekunde chache watafall back to their equilibrium, tena watapaza sauti, kwa kukosea mheshimiwa speaker/mtangazaji naomba uniache nimaliziekuwapasha,pia watajisahau kwa kinga ya chama na kujikuta wakiseme na kujipendekeza hovyo kwa polisi na viongozi wao.KWa ujum wanajirahisi sana. Msimamzizi wa kipindi aki moderate wataichukia kama ITV.wao haki ina definition tofauti sana,wao matusi ni relative, wao chochote tofauti na ccm ni adui kwao na kwa taifa.
 
Star TV kuna haja ya kujipanga upya msaidie kuweka mawazo ya watanzania pamoja kama mlivyofanya katika Mfululizo huu. Hii itasaidia kufikisha ndoto za Muda mrefu za Mh. Mbowe za kuwa na mjadala wa Kitaifa kujadili mustakbali wa Taifa hili.

Hatuhitaji rasilimali kubwa sana, Nyenzo kama akina Yahya Mohamed na wanahabari wengine wenye upeo mkubwa wa mambo, uzalendo na uthubutu wa kufanya mambo mnaweza kuwaunganisha watanzania.

ADIOS
 
Back
Top Bottom