Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?

Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.

Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.

Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.

Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.

Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.

Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
Mama mie nakulavu long taimu kinoma, naomba hii week isiishe tuwe kitu kimoja roni. Nimeamua kuwa mkweli kama unavyotaka natarajia mema toka kwako mpenzi Mzigua90 amini kwamba hutokaa ujute
 
Wanaume mna dhambi nyie acha tu, chuoni nilidate mume wa mtu for a year bila kujua, kuja kujua bila hata aibu analia kabisa eti nisimuache, i was like WTF[emoji134][emoji134][emoji134]

Kuna kipindi napo nusura nidate mume wa mtu, ila nafsi ilisita sana ikabidi nifanye uchungizi kwanza, ilinichukua miezi kama 7 kuja kugundua he is married. Utetezi wake "eti nilijua vile unawachukulia vibaya wanaume waliooa alafu wanaotoka nje ya ndoa zao hivyo usingenikubali na ungenidharau" yaani ndio nikamdharau maradufu.

Akili zao sojui kama ziko sawa na huwa zinawaza nini[emoji134][emoji134][emoji134]
Sasa hivi mambo si fresh lakini?
 
Pole sana jamanii auntie
 
Nimekumbuka mbali sana... hii mbinu ni chafu sana ila inatusaidia kupata totozi mtaani. Yaani unapiga sound mpaka unataja tarehe ya kwenda kwao kujitambulisha next day unapiga mzigo.
Hahahah mambo verse hayo
 
Oopss acha tu mnaongea usiku kucha.....kwake unafika yaani unashangaa
Niliwahi kuwa nae wa hivyo yaani siku nilivyo gundua nilijiuliza maswali mengi kichwani bila majibu mkewe alikuwa nae mda gani maana akitoka job yupo na mimi,weekend yupo na mimi, simu yangu anaipokea bila tatizo.akija kwangu Pete ya ndoa anavua kiazi mbatata yule sitamsahau mwaume mjanja zaidi ya sungura.
 
Haahhaahhaaah eti kiazi mbatata looool
 
Niliwahi kuwa nae wa hivyo yaani siku nilivyo gundua nilijiuliza maswali mengi kichwani bila majibu mkewe alikuwa nae mda gani maana akitoka job yupo na mimi,weekend yupo na mimi, simu yangu anaipokea bila tatizo.akija kwangu Pete ya ndoa anavua kiazi mbatata yule sitamsahau mwaume mjanja zaidi ya sungura.
😂😂😂😂😂
 
Back
Top Bottom