Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?

Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.

Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.

Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.

Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.

Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.

Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
Na nyie muwe mnatongoza wanaume mnaowapenda.
Hiyo ya kudanganywa huwatokea sana wasichana wanaojifanya wanaringa na kujisikia. Kuna mmoja miaka ya zamani alijua nitamuoa yeye nikapindua matokeo.
 
Umeandika kwa hisia sana pole mpenzi ......


Naunga mkono hoja habari za kuwekana na matarajio makubwa mwisho wa siku yanakuja kutokea haya kwa kweli sio poa ....yameshawahi kunikuta haya tena mtu anakwambia oooh watoto hawa mamayao alitaka kunichoma kisu nikaponea chupuchupu akapelekwa police ushahidi alitoa mwanangu huyu kwahiyo mama yao sipo nae pamoja.....mtu najitutumua kuwapenda watoto nawaweka dp huko Sijui vikorombwezo gani siku ya siku nakuja kujua jamaa ana mke tena mwanamke alikamata namba zangu akanipigia kanichimba mkwara wa nguvu


Me huwaga mpole tu kwenye kesi za ndoa za watu nikamwomba msamaha yule dada yakaisha ...lile punguwani nikalipiga stop kunitafuta kwa namna yoyote.....


Kwakweli wanaume muwe wawazi mnapotuficha vitu kama hivi mnatutengenezea mazingira ya kufakufa ....wake zenu wengine ni vichaa anakuiba namba anamtafuta huyo uliyemfanya mchepuko anaenda kumfanyia kitu kibaya .....

Kuweni na huruma tu ....halafu nyinyi mmeoa huku nje mnatafuta nini mbuzi wa kafara nyinyi mnataka nini hukuuuuuu aaaaagggggrrrrr[emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35] [emoji35]
Pole best huyo bazazi usikubali kuludi kwake shwaini wahedi
 
Suala la kuambiana ukweli kwenye mapenzi kwa zama hizi tusahau kama unataka ukose unacho taka sema ukweli kwamba baby me nina mtu ila nimetokea kukupenda au baby mie kiukweli kitandani huwa napiga nusu bao nivumilie usiniache nakupenda utaishia kuwaita shemeji wadada wazur
Hahaha ndio hivyo ukweli ni mzuri sana ila hauko practical kabisa hasa kwa hawa dada zetu. Yani kuna mazingiria flani usipoyatengeneza tu ukaya present kwake hawezi kukubalia hata kwa kujilazimisha.
 
Wanaume mna dhambi nyie acha tu, chuoni nilidate mume wa mtu for a year bila kujua, kuja kujua bila hata aibu analia kabisa eti nisimuache, i was like WTF[emoji134][emoji134][emoji134]

Kuna kipindi napo nusura nidate mume wa mtu, ila nafsi ilisita sana ikabidi nifanye uchungizi kwanza, ilinichukua miezi kama 7 kuja kugundua he is married. Utetezi wake "eti nilijua vile unawachukulia vibaya wanaume waliooa alafu wanaotoka nje ya ndoa zao hivyo usingenikubali na ungenidharau" yaani ndio nikamdharau maradufu.

Akili zao sojui kama ziko sawa na huwa zinawaza nini[emoji134][emoji134][emoji134]
 
Wanaume mna dhambi nyie acha tu, chuoni nilidate mume wa mtu for a year bila kujua, kuja kujua bila hata aibu analia kabisa eti nisimuache, i was like WTF[emoji134][emoji134][emoji134]

Kuna kipindi napo nusura nidate mume wa mtu, ila nafsi ilisita sana ikabidi nifanye uchungizi kwanza, ilinichukua miezi kama 7 kuja kugundua he is married. Utetezi wake "eti nilijua vile unawachukulia vibaya wanaume waliooa alafu wanaotoka nje ya ndoa zao hivyo usingenikubali na ungenidharau" yaani ndio nikamdharau maradufu.

Akili zao sojui kama ziko sawa na huwa zinawaza nini[emoji134][emoji134][emoji134]
Zipo sawa kabisa wewe una wasiwasi tu!
 
Back
Top Bottom