Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Ombi: Unapomtokea Mwanamke Mueleze Ukweli

Hii tabia unamtokea mtu unamdanganya uko single wakati una mke au mahusiano yenye furaha na amani ni UBINAFSI. Wewe utasema unanipenda kwa dhati ndio maana umeamua kunidanganya huwazi nitakavyoumia siku nikiujua ukweli?

Halafu utetezi wenu ni "Ooh bby nilijua nikikuambia ukweli utanikataa". Unaona kukukataa na kuniumiza moyo wangu Bora uniumize ili utimizie lengo lako?
Kwa dhati kabisa ya moyo wangu nawaomba mseme tu ukweli ili mtu ajue anajiingiza kwenye nini Kuliko unidanganye.

Mimi mwenyewe muhanga wa hili jambo na nilikua head over heals kwa huyu mkaka kumbe moyoni mwenzangu anajua kabisa mimi anapita ana mtu wake. Na baada ya kuujua ukweli akaanza kuniambia hana furaha na huyo mwanamke ananipenda mimi. Ila kwa jinsi nilivyompenda nilishindwa kuvumilia nikamwambia tuachane tu siwezi kukushare maan nilimwambia kama huna furaha achana nae uwe na mimi akashindwa. Niliumia mpaka nikaamsha vidonda vya tumbo siku hiyo namshukuru Mungu nimemove.

Rafiki yangu juzi tu kajua mtu aliempenda kwa mara ya kwanza toka apate akili ni mume wa mtu. Na alimdanganya eti hajaoa ana baby mama tu kumbe huyo baby mama ndio mkewe. Na alishamuuliza mwanzo akasema hana mahusiano ana mtoto tu ila yeye na baby mama hawana mahusiano. Mungu alivyo mwema last weekend wamekaa bar kaja mtu anaomba msamaha kwa jamaa kuwa alishindwa kuhudhuria harusi mbele ya rafiki yangu. Rafiki wa jamaa alivyondoka alimuapia rafiki yangu miungu yote kuwa hana mke na ndoa ilishindikana kufungwa halafu kwa sababu ya kijinga sijui kwanini rafiki yangu akamuamini. Sasa nikasikia tena jamaa kaoa nikamwambia rafiki yangu.
Kufupisha tu jamaa ni kweli ameoa na anaesema ni baby mama ndio mkewe nae utetezi wake hakutaka kusema alivyomuona rafiki yangu kwa kuwa aangemkataa ila anampenda.

Mwingine mpaka Pete kavalishwa na mchumba wa mtu na jamaa anaoa week ijayo anamuacha mwenzie na mtoto na aibu ya kupeleka mchumba ambae alikua na mtu mwingine.

Ukijijua huna mpango na mtu mwambie ukweli mtuepushie maumivu makubwa wengine kupenda kwetu kwa bahati tukipenda tunapenda kweli sasa kukaa na kugundua wewe ni side chick kwa bwana wa mtu inauma sana.

Samahanini kwa gazeti ila nimesisitiza na hivyo visa viwili kukazia maombi yangu kwenu. MTUONEE HURUMA na mioyo yetu.
Natamani kutumia mda wangu nawewe sio kwa upendo bali kwa tamaa na mvuto ulionao kwenye macho yangu, nachohitaji ni kuwa wapenzi, kupunguziana hamu na muwasho...ninae ninaempenda kwa sasa naishi nae na nimezaa nae...naomba kwa sasa uwe sex partner wangu na siwezi kuahidi ndoa ila lolote linaweza tokea tukiwa kwenye kipindi hiki, na ikitokea tumependana kwa dhati tutajua tunafanyaje.naomba ulifikirie kwa makini ombi langu..

Kwamba nikisema hivyo unaweza nikubalia[emoji3]
 
Hahaha sindio fahari yenu nyie...unaweza ukaingia bar tu ukaagiza vinywaji ukanywa na ukaondoka bila deni kisa msambwanda tu!

Namwelezaga jamaa..anahis huenda nimetumia hela kuuubwa nikijipa out na watoto 😇😇😇.. kumbe hapo gharama uloingia ni kulipia bembea tu🤗🤗🤗🤗unajirudia zako hom na dompo 2😊😊😊 maisha mubashara kbs..na wanao wanakula kbs..mnafikia kulala🙆🙊
 
😂😂😂😂😂 wewe, sema basi tu
 
Natamani kutumia mda wangu nawewe sio kwa upendo bali kwa tamaa na mvuto ulionao kwenye macho yangu, nachohitaji ni kuwa wapenzi, kupunguziana hamu na muwasho...ninae ninaempenda kwa sasa naishi nae na nimezaa nae...naomba kwa sasa uwe sex partner wangu na siwezi kuahidi ndoa ila lolote linaweza tokea tukiwa kwenye kipindi hiki, na ikitokea tumependana kwa dhati tutajua tunafanyaje.naomba ulifikirie kwa makini ombi langu..

Kwamba nikisema hivyo unaweza nikubalia[emoji3]
Maisha yako yote, subiria jibu la "Asante nashukuru kaka" hapo hata kunawa tu hunawi achilia mbali kula
 
Katika uongo ambao sikuwahi mdanganya mwanamke ni kumwambia kua sina mahusiano wakati nnayo, na nnachofurahi wanawake wa siku hizi hata uwaeleze ukweli kwa 100% bado atakukubali tu
 
Yeah ni rahisi lakini mtu anakupeleka mpaka kwake. Na mahaba kama yoteeee
Umenikumbusha jirani yangu mmoja marioo kakaribishwa tu na demu wake wakawa wanaishi kwa huyo demu, jamaa hana kazi demu ake akienda kazini anaingiza mademu wengine ndani, yaani anaficha kila kitu cha huyo demu wake,
Sasa nkawa najiuliza anawezaje kuficha vyote ilihali chumba ni cha huyo demu?
Hivi nyie wanawake mkifika kwa mwanaume kwa nini msiombe mkague kila mahali ili kujiridhisha?
 
Natamani kutumia mda wangu nawewe sio kwa upendo bali kwa tamaa na mvuto ulionao kwenye macho yangu, nachohitaji ni kuwa wapenzi, kupunguziana hamu na muwasho...ninae ninaempenda kwa sasa naishi nae na nimezaa nae...naomba kwa sasa uwe sex partner wangu na siwezi kuahidi ndoa ila lolote linaweza tokea tukiwa kwenye kipindi hiki, na ikitokea tumependana kwa dhati tutajua tunafanyaje.naomba ulifikirie kwa makini ombi langu..

Kwamba nikisema hivyo unaweza nikubalia[emoji3]
Ndio nakubali
 
Tokea nimeanza kuwaambia ukweli wanawake nimpata single mother mmoja tu tena alikuwa kanizidi umri
 
Hatari sana yani makuzi sana sasa sijui alikuwa anautaka udangaote au umo dewji[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Amna basi tu kuna raha ukiwa unamtia demu asie na njaa af akawa anakupa penzi kama lote
 
Nyie ni wakudanganywa tu ndio tunaenda sawa, kuna mmoja alinipenda mno kumwambia kazi yangu tu akaniacha sijui alishachezewa na hao watu? yani alinihukumu kwa makosa ya wengine
 
Back
Top Bottom