Ombi: Ikulu ipuuze waraka wa Kakobe

Ombi: Ikulu ipuuze waraka wa Kakobe

Mtumishi wa Mungu yupi.... Jah, Krishna, Ngai, Budha Y esu Allah, Man-above, Mars Thor, Ra, Mulungu etc... toa upumbavu wako wa mapepo , unadhani kila mtu anaamini unachokiamini wewe. IDIOT:A S confused:
Unauliza MUNGU yupi?.Ukamilifu wao wenye haki utawaongoza, Bali ukaidi wao wenye fitina Utawaangamiza.
[Apotoshaye njia zake atajulikana]
 
Kwanza, rais hana sababu yoyote ya kumuomba msamaha mpentekosto yeyote kwa kuwa rais hatekelezi majukumu yake kumfurahisha mpentekosti bali anafanya mambo kwa mujibu wa sheria.

Pia rais hana sababu ya kumuomba Kakobe msamaha kwa kuwa anamfahamu vizuri kuliko sisi sote hapa kuwa Kakobe ni vuvuzela tu.

Pia, mimi, wewe au yule hatuna sababu ya kumsihi rais apige magoti au afanye ibada. Hilo ni suala ambalo mhe rais analifahamu na analifanya kupitia imani yake ya kiislamu.

Kama unaamini katika haya uliyoyaandika why wasted your time and energy kuanzisha hii thread?

Vuvuzela anahitaji attention ya mtu mwenye integrity kama yako? Why dont you just ignore tu kama alivyofanya Rais na taasisi yake nzima?

I would advice you to just take your time with your other important issues and leave the rest to Kakobe!

Mungu wa Kakobe according to you ni Vuvuzela then what is the mater?

Mm na dhani kuwa gentle tu na uendelee kula maisha na mavuvuzela nao waendelee kupuliza vuvuzela zao!
 
Wewe endelea kutanua bichwa kama hiyo avatar unayoitumia uzani unapata sifa.

Wenye hekima hatusemi kitu juu ya ujumbe wa Kakobe kwa JK kwakuwa amemuhusisha Mungu, basi ni dhahiri kuwa Mungu huyaweza yote na haitaji msaada wa binadamu awaye yote. Kama aliyosema Kakobe ni kweli yametoka Kwa Mungu au nimambo yake binafsi! hilo mimi halinihusu kwani Mungu ndie anayejua ukweli wa yote na Mungu ndie atakaetoa uwamuzi wa mwisho.

Sasa wewe
HAMY-D vimba bichwa humu JF ukizani unapata sifa kwa kutunga hoja za kimaandazi ndo hapo Utakapokutana na Mkono wa Mungu.
 
HAMY-D Kwanza, nikupengeze kwa kuwa mfuatiliaji mzuri wa mambo yanaloligusa au unayohisi yanaliugusa taifa lako. Pili, nikupe pongezi kwa kutumia muda wako kuandika kile ulichokiamini. Pamoja na hayo, maneno yako yanaonyesha ama u- mvivu wa kufanya uchunguzi ama una chuki isiyo na kifani dhidi ya wapentekoste na upentekoste, au una mahaba makubwa na chama chako ama vyote vitatu. Lile la kwanza, nafikiri ndilo linakusumbua zaidi.

Hivi hujui baada ya ufafanuzi wa ikulu, wapentekoste walisemaje? Nadhani hujui. Hata jinsi ikulu ilivyojibu, nasema hujui. Wewe unasema maaskofu walijipendekeza wenyewe, Sasa ngoja nikwambie, ikulu ilisema juhudi za serikali hazikubaini kama walikuwa miongozi mwa watu 118 waliojipendekeza wenyewe. Soma nukuu hiyo hapa chini.

17. Pamoja na kwamba haikutarajiwa kuwa viongozi wa taasisi hii kujipendekeza
wenyewe, na hivyo kuwa miongoni mwa watu 118 waliojipendekeza wenyewe,
juhudi za Serikali zilijielekeza kutafuta endapo kulikuwa na mapendekezo kundi hili.
Hata hivyo, utafutaji haukubaini majina ya viongozi hawa kuwepo katika orodha
hiyo.

Juhudi za serikali hazijabaini kule kunakoitwa kujipendekeza wenyewe, lakini wewe unasema walijipendekeza wenyewe. Lo! maajabu hayaishi duniani, yaani wewe una juhudi sana kuliko serikali unayoitetea.

Eti baraza la maaskofu liliridhia majibu ya serikali. Wewe hujui lolote. Hebu leta ushahidi wa tamko, au link ya gazeti ama ushahidi wowote katika hilo. Kinachofahamika kwa watanznaia ni kwamba Ikulu iliseama haijapokea majina, na baada ya siku 2 wapentekoste walionyesha hadharani saini za maafisa wa ikulu waliopokea majina hayo. Hata humu jamvini saini hiyo iliwekwa hadharani kwa dispatch ya PCT. Hivi mtu binafsi anaweza kujipendekeza kwa nembo, mhuri, dispatch na muhtasari wa taasisi.

Halafu ndugu yangu huo waraka wa Kakobe si alishasema wazi kuwa unaweza KUUPUUZA? hakukulazimisha wewe na Kikwete muuamini, sasa wewe hapo unaweweseka nini? Mwisho nakuomba ukajipange upya, zile sababu zingine ulizoanza kuzitafuta, mara wapentekoste hawafiki milioni 1, mara useme eti Tusichamganye dini na siasa ni za kitoto kwani wale TEC, BAKWATA au CCT si taasisi za dini? Uwezo wako wa kuchambua mambo ni mdogo sana. Nimekudharau na kukupuuza kwa kushabikia ubaguzi unaofanywa na serikali yako.
 
Last edited by a moderator:
Muulize baba yako juu ya huyo huyo Kakobe na siasa za Bongo maana ww bado kinda.Alishawahi kusema "kama Mhe.Mrema asipokuwa Rais,basi Mungu anayemhubiri sio Mungu wa kweli". Je,historia inasema Mrema alishawahi kuwa Rais wa inji hii?!

Kwa nini tusiamini kuwa Kakobe ni TAPELI na mwizi wa fedha za waumini kwa kupitia utumishi wa Mungu fake? Hajasikika siku nyingi,na tayari analijua hilo,leo anataka kulikuza jina lake kwa Utapeli tena wa wazi?! Kama PCT hawakufuata utaratibu wa kuwakilisha katika Bunge la katiba,nini sasa kinachomuwasha Kakobe?!

Lakini pia,kwani katiba ni kwa ajili ya nani na hao waliopo Bungeni sasa hivi,wanamuwakilisha nani?!Kakobe,mvuto umekuisha,sadaka hazitoshi sasa unataka hadi hizo laki 3 kwa siku.Kwanza kanisa lako halilipi hata kodi pamoja na pesa zoote unazokusanya hapo.Is that not a business ur doing??!!

Eleza juu ya ujumbe na si kumshambulia Askofu Kakobe.Ungekuwa na Hekima ungesubiri matokeo ya ujumbe ndiyo ujue ni mawazo ya Askofu Kakobe au ni agizo la MUNGU.Na kama unajiamini na una hakika kwa unachokisema ni vizuri umshawishi Kikwete haukataye huo ujumbe. ili tuone Matokeo yake[Mambo ya MUNGU ni magumu kuaminika kwako kuliko ya Shetani]
 
Hamy-d ndio walewale. Hapo hamtoki mungu yuko kazini.mlimzushia kwamba awetoroka kumbe alikuwa kanisani kwake akimwomba mungu. Sasa imekula kwenu. Subiri ni suala la muda. Pole sana maslahi yako ya meguswa.
 
Hivi Kakobe ndio TB Joshua wa bongo?

Kwamba kila anachosema kitokee?
 
Msiwafanye watanzania wajinga. Kwanini viongozi wanapoapishwa wanatumia vitabu vya dini. Serikali haina dini kwa vipi wakati viongozi wote wana dini zao. Acha pumba zako. Ccm imekwisha.
 
Kwanza, rais hana sababu yoyote ya kumuomba msamaha mpentekosto yeyote kwa kuwa rais hatekelezi majukumu yake kumfurahisha mpentekosti bali anafanya mambo kwa mujibu wa sheria.

Pia rais hana sababu ya kumuomba Kakobe msamaha kwa kuwa anamfahamu vizuri kuliko sisi sote hapa kuwa Kakobe ni vuvuzela tu.

Pia, mimi, wewe au yule hatuna sababu ya kumsihi rais apige magoti au afanye ibada. Hilo ni suala ambalo mhe rais analifahamu na analifanya kupitia imani yake ya kiislamu.
Unatatizo katika Uwelewa wako,Wapi kwenye ule Ujumbe Askofu Kakobe kasema aombwe msamaha na Kikwete au Awaombe msamaha Wapentecoste?.Mihemko ya Kidini ndiyo inayokusumbua.{Kazi yake mwenye haki huelekea Uzimani, Bali Mazao ya wabaya huelekea Dhambini}
 
Ehe Mwenyenzi Mungu, Mungu muumba mbingu na nchi, Mungu Uliyemuumba Kikwete na uliependa ccm iwepo Tanzania kipindi cha Nyerere,Mungu uliye juu ya Mathehebu ya dini zote. Tunanakuomba ujitetee juu ya ujumbe wako ulioupitisha kwa mtumishi wako Kakobe. Mungu tunakuomba usichelewe kufanya jambo kwa ccm kama ulivyosema kupitia mtumishi wako Kakobe ambaye anadhihakiwa sasa. Mungu tunakuomba hasira yako isiwake juu ya Tanzania kwakuwa ni dhahiri kuwa hakuna atakayesalia. Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Chadema, Ameni.
 
No offence, but to me Kakobe is a cone man. Namuona tapeli kama walivyo matapeli wengine.

Kwanza heshima yangu kwake niliipoteza tangu alivyo kimbia ile ishu ya TANESCO. Yani nilikuwa napita nakuta walaghaika wake wakikesha eti kuomba umeme usipite. Yani kuna watu wajinga hapa duniani.

Hivi sasa kote kumewekwa nguzo na mradi wa TANESCO umesonga mbele huku Kakobe akiambulia aibu na kukimbiwa na waumini wake.

Kuwa na heshima acha kutukana watumishi wa mungu, utaumia vibaya sana

Katika waraka wake kuna sehem kagusia sana maCCM wengi kuamini na kutembea katika nguvu cha uchawi... sasa kama na wewe ndio upita hapo

Basi na kusii acha kutukana watumishi wa mungu kwa personala attack utapotea vibaya.
 
wewe ni msemaji wa ikulu? Au ni msemaji wa watanzania gani ambao una wawakilishi hapa ? Ujinga ni kipaji.......ikulu i mjibu kama majibu yapo .....
wewe ni muwakilishi wa kakobe?, au msemaji wa wapentekosti?, mwachie kakobe mwenyewe anayetapeli watu kwa michango ya kidini ndiye aseme.
 
Manake alichokifanya Kakobe ni sawa na kundi la Mashia au Ahmadiya Tanzania nao wapeleke kilio chao kwakukosa mwakilishi bunge la katiba wakati nao wanahaki hiyo. Kwa mantiki hii kila dhehebu la dini likitaka kuwa na muwakilishi bunge la katiba sasa kungekuwa kuna undwa katiba ya dini au katiba ya nchi? Kakobe ni tapeli miongoni mwa matapeli hapa Tanzania, tumsameheni tu.

PCT sio dhehebu kama unavyodhani ni taasisi inayoyaunganisha madhehebu 75. Ufafanuzi wa ikulu unathibitisha kuwa ni kundi ambalo RAIS ASINGEWEZA KUACHA KUTEUA. Soma nukuu ya ikulu hapa chini:

"Kwa kufahamu umuhimu wa makundi mbalimbali ya kidini ikiwa ni pamoja
na Baraza la Maaskofu wa Kipentekoste Tanzania unaoundwa na Maaskofu
Wakuu wa madhehebu ya kipentekoste yapatayo 75, uteuzi wa wajumbe wa
Bunge Maalum la Katiba ulihakikisha kuwa makundi ya kidini
yanawakilishwa ipasavyo"


Ndugu Chamviga, Mjinga akinyamaza, huonekana ana busara. Kajipange upya.
 
Shida mtumishi wa Mungu Kakobe alijua anaongea na watu wanaomjua Mungu, hakujua kama anawaandikia mapagani wasio na hofu na Mungu. Mapigo kwa chama hiki cha zamani hayaepukiki!
 
Masahihisho: Ule si waraka wa KAKOBE bali ni waraka wa Mungu kwenda kwa CCM. Sasa mkiupuuza ni juu yenu kwani hata wakati wa Nuhu wakati akijenga safina watu walimpuuza na kumwita chizi. HAMY-D
 
Last edited by a moderator:
Kama Kakobe angekaa chini na kufikiri kwa uchache tu kuhusu huo ujumbe anao usema umetoka kwa Mungu asinge thubutu kuupeleka Ikulu.

Kwanza napata shaka na Mungu ambae Kakobe amem-refer. Asije akawa Mungu wa kusadikika. Maana Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Yakobo sidhani kama anaongea na matapeli wa kiroho aina ya Kakobe.
Ngoja niongee mambo yaliokuzidi Ufahamu wako na Unijibu,MUNGU alitumia Ujumbe kwa Kinywa cha Punda kwa Balam.YESU akawaambia,watu awa wakinyamaza mawe yatapiga kelele.Lili jepesi kwako MUNGU kumtumia Askofu Kakobe au Punda?. Utomchagulia MUNGU watu wa kuwapa Ujumbe kamwe na utopata hiyo nafasi Milele
 
No offence, but to me Kakobe is a cone man. Namuona tapeli kama walivyo matapeli wengine.

Kwanza heshima yangu kwake niliipoteza tangu alivyo kimbia ile ishu ya TANESCO. Yani nilikuwa napita nakuta walaghaika wake wakikesha eti kuomba umeme usipite. Yani kuna watu wajinga hapa duniani.

Hivi sasa kote kumewekwa nguzo na mradi wa TANESCO umesonga mbele huku Kakobe akiambulia aibu na kukimbiwa na waumini wake.

Nguzo zilipita umeme je?
 
Ehe Mwenyenzi Mungu, Mungu muumba mbingu na nchi, Mungu Uliyemuumba Kikwete na uliependa ccm iwepo Tanzania kipindi cha Nyerere,Mungu uliye juu ya Mathehebu ya dini zote. Tunanakuomba ujitetee juu ya ujumbe wako ulioupitisha kwa mtumishi wako Kakobe. Mungu tunakuomba usichelewe kufanya jambo kwa ccm kama ulivyosema kupitia mtumishi wako Kakobe ambaye anadhihakiwa sasa. Mungu tunakuomba hasira yako isiwake juu ya Tanzania kwakuwa ni dhahiri kuwa hakuna atakayesalia. Mungu Ibariki Tanzania,Mungu ibariki Chadema, Ameni.

Amen and Amen!
 
Ndugu sura mbaya wewe unakaa wapi?mpaka leo umeme ulishindwa kukatiza pale,kuthibitisha hilo nenda Mwenge kaulize.Mwaka Juzi mtu mmoja anaye sadikika kuwa kichaa alipanda mpaka kwenye nyaya hizi lakini hakunaswa,wamekuja Wajapan,Wachina wote wameshindwa.Fanaya utafiti kabla ya kuja kwenye mitandao ya kijamii.Na hii MUNGU alimpandisha kichaa huyo kuthibitisha kuwa maombi ya Wenye haki ni manukato.Wakati wa Biblia Wafalme waliwauliza manabii wa MUNGU,Maraisi wa sasa wanamuuliza nani?kama sikweda mlingotini.Sikushangai maana maajenti wa Ibilisi wako kila sehemu.
 
Rais wetu kikwete usiogope kwenda madhabahuni na kutubu dhambi zako, Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo ni Mungu asiyesema uongo, so kazi ni kwako.
Hivyo hata mkipinga mchana na usiku yeye bado atabaki kuitwa Mungu.
 
Back
Top Bottom