Ombi: Ikulu ipuuze waraka wa Kakobe

Ombi: Ikulu ipuuze waraka wa Kakobe

Kakobe alifanya kosa sana kuliuza kanisa lake akakimbilia marekani,huko amekuta hali ngumu,biashara imekua ngumu wazungu hawadanganyiki,kaamua kurudi kwa style ya,''NITOKE VIPI''.
 
Mpuuzi tu ameshakula pesa za wajinga sasa anataka arejeshe umaarufu wake??amepitwa na wakati ikulu imeshatoa ufafanuzi,amebug step man
Ufafanuzi wa Ikulu ni dhaifu na umeidharirisha Hadhi ya Ikulu.

Ukitaka kujua kuwa kuna udhaifu ni kwamba mda mfupi baada ya kutoa ufafanuzi huo wakawaita tena PCT !!
 
kakobe alifanya kosa sana kuliuza kanisa lake akakimbilia marekani,huko amekuta hali ngumu,biashara imekua ngumu wazungu hawadanganyiki,kaamua kurudi kwa style ya,''nitoke vipi''.
huu uongo ndio uliomugharimu kikwetena tbc.!!!
Wewe huwezi kusema kwamba kakobe ametoroka ati kwa yeye kwenda marekani na kuhubiri injili wakati kikwete anakwenda mara kwa mara huko akikimbia matatizo ya watanzania na wewe huyo huyo hujasema kuwa kikwete katoroka,!! Mawazo finyu kama haya ndo yanawagharimu kuwa domant na kufikiri kuwa watanzania wote wapo hivyo !!
 
Kama PCT walikosea si wangeeleweshwa utaratibu? Hivi kama angeenda mlemavu au shehe au mchungaji binafsi, serikali isingetoa mwongozo wa kufuata? Ingewatupilia mbali? Muda ulikuwepo. Suala la kutupiliwa mbali lisingekuwepo iwapo wangepewa nafasi.Anyway, let's make two in two two's!!
 
Kakobe alifanya kosa sana kuliuza kanisa lake akakimbilia marekani,huko amekuta hali ngumu,biashara imekua ngumu wazungu hawadanganyiki,kaamua kurudi kwa style ya,''NITOKE VIPI''.

HEBU TUPE VIELELEZO!! Alikimbilia Marekeni lini? Aliwaaga watu hivyo au unakurupuka tu? Mimi nafuatilia na hata Mwenge nafika,mtandao wake au website ya huduma yake haijawahi kutoa tamko la kuhamia Marekani. Kakobe si mfanyabiashara! Historia yake na maisha yake ya sasa hujajui. In short alienda Canada, Toronto,June 2012 kuhubiri kwa siku nne na kurudi within two weeks. Ameshaenda nchi nyingi tu baada ya hapo k.v Congo DRC Zambia,nk. Ongea kitu unachoweza kukiprove. Never argue with a fool..
 
WanaJF,

UZEMBE NI WA NANI MPAKA PCT IMEKOSA MWAKILISHI BUNGE LA KATIBA?

Ndugu zangu, hili suala limeshatolewa ufafanuzi na Ikulu na Watanzania wakaridhika maana kabla ya ufafanuzi Watanzania walikuwa wame-panic kuwa PCT imeonewa na kudhurumiwa haki yao ya kushiriki kuandaa katiba.

Ufafanuzi ulisema kwamba, baraza la maaskofu alikufuata maelekezo ya sheria katika kuwasilisha mapendekezo yao ya wawakilishi.

Jambo ambalo PCT walikosea ni kujipendekeza kama watu binafsi badala ya kuwa kwenye makundi kama ambavyo sheria ilielekeza. Hivyo serikali haikuwa na budi bali kupiga majina ya PCT kapuni na kupelekea wapentekosti kukosa mwakilishi.

Hivyo hapa mtajionea kuwa kosa lilikuwa la PCT na sio serikali.

KUANDIKWA KWA WARAKA IKULU:

Baada ya maelezo ya serikali kutolewa, baraza la maaskofu liliridhia kuwa wao ndio hawakufuata maelekezo ya sheria hivyo kukiri kuwa walikosea pia walitoa taarifa kwa umma kuwa wameelewana na serikali kuhusu sakata lao.

Lakini ghafla Watanzania tumeshangazwa na Kakobe ambae amejitokeza na kumuandika mhe. Rais ujumbe uliojaa vitisho na mambo mengi ya kusadikika.

Kusema ukweli hili ni jambo la ajabu, sijui Kakobe kakurupuka au vipi, maana kuhusu Pentekosti kukosa mwakilishi tayari Ikulu imelimaliza na aliyefanya kosa la kukosekana kwa mwakilishi wao kwenye bunge ni hao PCT wenyewe.

Sasa Kakobe tatizo lake hapa ni nini!? Nini ambacho hajakielewa katika ufafanuzi wa kurugenzi ya mawasiliano Ikulu kuhusu hili suala!?

Nitoe angalizo kwa Kakobe: kama Kakobe alitaka arudishe umaarufu wake uliotoweka kupitia huu waraka, basi amepotoka big time.

Watanzania sio wajinga kama ambavyo Kakobe anadhani. Kama Kakobe alifanikiwa kudanganya baadhi ya Watanzania na kuweza kujitajirisha, basi asidhani kama ataweza kutudanganya Watanzania wote.

Wewe jamaa m ji nga sana, una uwezo na uelewakubwa kuliko ikulu?
 
kupuuza ni upuuzi!ikulu yenye akili haiwezi kumpuuza KAKOBE au hata wewe HAMY-D kama una maneno ya maana.NDO maana unaona walikuja haraka kujibu ila hawakupatana namna ya kudanganya ikawa vululu vululu maelezo hayaunganiki!ukiona mkuu anajichanganya sisi wenye akili kidogo tunajua TUMESHASAMEHE.MUNGU ATAINUA HADI MAWE HUMO HUMO MWENYE BUNGE NA KWA KUWA HAMY-D WAONEKANA NDO KWANZA UNAMALIZA SHULE YA KATA BASI CCM ITAANGUKIA PUA MBELE YA USO WAKO MCHANA KWEUPEEE!KAKOBE ANAWEZA AWEPO AU ASIWEPO LAKINI MWELEKEO WA HISTORIA NDIVYO UNAVYOONESHA!YEYE KATOA TU UNABII!
 
Ikulu imepuuza waraka wa Askofu Kakobe hadi leo wanahangaikia katiba mpya
 
Back
Top Bottom