Ole wako Tanzania, viongozi vijana ni wanafiki haswa Zitto: Posho alisema hivi...

Yes, acheni siasa chafu za kusafishana nyie wote mnaojifanya wanaharakati uchwara wanasiasa midomo bila kichwa, zitto AMERAMBA MKENGE katika hili, amejikwaa mh. Ni binadamu.

Ameacha maslah ya watanzania maskin sana, ameunga mkono maslah ya wabunge ambao ni well off, iitwe ni posho au isiitwe, badala yake ikaunganishwa kwenye mishahara ni the same tu haimsaidii maisha ya mwanatanganyika wa nyasa au ngudu. . Jaman Nyeusi ibaki kuwa nyeusi, vivyo hivyo kwa rangi bluu.. Bro ameenda chaka
 
Nimelazimika kurejea baada ya kuona kuna watu wanapotosha hoja yangu,

Hivi Shibuda si alisema posho iwe milioni kumi na mbili kama Zitto wakamtishia kumwondoa hata ubunge?
Shibuda alisema isiitwe posho bali ujira wa Mwiha , si alishitakiw kwenye kamati kuu ya chama chao?

Sasa tofauti ya Zitto na Shibuda iko wapi hapo? ukisimamia jambo hakikisha unalisimamia mpaka mwisho na sio kuyumba yumba kwani huo ndio unafiki.
 
Binafsi nilikuwa namwona kama nuru miongoni mwa vijana viongozi wa kisiasa nchini ,ila tangu jana nimesema ntakuwa namsikiliza kwa masikio mawili na kumtizama kwa macho mawili , nitapima kauli zake kwa kina sana .

Wewe unayejiita Mwongozo wa Spika hivi nani kakudangaya kuingia humu? Kwanza bado hujakomaa kwa majadiliano ya humu jamvini unataka kuleta ujanja wako wa MAGAMBA! Waulize kwanza akina Wasila na Anne Makinda a.k.a Bi. kiroboto wakupe semina elekezi ya namna ya kuwasilisha mada! Tena ukome kuleta umbea wa kwenye mistari ya TAARAB!
Bahati yako sheria zinanibana ningekutusi wewe!!!! *******yako!
 
Nimelazimika kurejea baada ya kuona kuna watu wanapotosha hoja yangu,

Hivi Shibuda si alisema posho iwe milioni kumi na mbili kama Zitto wakamtishia kumwondoa hata ubunge?
Shibuda alisema isiitwe posho bali ujira wa Mwiha , si alishitakiw kwenye kamati kuu ya chama chao?

Sasa tofauti ya Zitto na Shibuda iko wapi hapo? ukisimamia jambo hakikisha unalisimamia mpaka mwisho na sio kuyumba yumba kwani huo ndio unafiki.

Sasa naona unatafuta wakucameroon! Haya weka picha yako watu watathmini mpiko!
 
Zitto ni shujaa,ametimiza wajibu wake,wewe ndio mnafiki usiolijua ulitendalo..
 
upupu mtupu!

Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema “Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho” ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema “Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana”

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.
 
hapa hoja si mleta mada kupinga posho, hoja ni unafiki wa zitto.
Kwann kwenye media na kwenye majukwaa aipinge halafu akiwa na wenzake aikubari?
Anakuwa kama simba kwenye ngozi ya kondoo

Ehee, kakubali wapi hebu tujuze. lakini utoe majibu baada ya kusoma maelezo yangu kwenye post no. 29 na kuelewa incentives anazozungumzia Zitto
 
Kimsingi sijaelewa umeeleza nini. Mimi si mfuasi wa Zito lakini nameelewa tangu mwanzo Zitto ambacho hataki. Ni kwamba posho ni fedha ambayo inatolewa kwa baadhi tu ya watu fulani tu.

Hii ina maana kwamba allowance haina Kodi na kwa sababu hiyo inafanya taifa lipoteze fedha nyingi sana ambayo ingelipiwa kodi. Pia mwalimu wa kawaida anawezaje kunufaika na posho? Daktari wa kawaida atanufaikaje na posho?

Huu ndiyo hasa msingi wa hoja ya Zito. Kwa nini msiongeze mishahara na badala yake mnaongeza posho? Unajua posho ikiongezwa haiathiri watu wote katika nchi. Lakini ukiongeza mishahara ya wabunge ni wazi kwamba jambo hili litaathiri taifa zima.

Ndugu yangu nikweleze watu tu. Wewe ndiyo mnafiki, usiyelewa kitu chochote. Yaani kwa mda wote huu hujaelewa hoja ya Zito mimi nadhani unashida kubwa kama mbunge sijui unawakilisha nini.
 
Achana ne huyu jamaa, nimemwambia ni boga kabisa, nia yake ni sisi watu wazima na nanihii zetu tumjadili Zitto badala ya kujadili Uhalali wa SITTING allowance, na uhalali wa Ongezeko la SITTING ALLOWANCES kwa wabunge.

Wanaelewa sana, sema hawa ni wagonjwa wa "Zittophobiasis"
 
We mleta mada unapomkandia Zitto wewe unamchango gani. Maana Zitto ni mnafiki wewe usie mnafiki unalisaidiaje taifa. Kwanza kuuchuna ndani ya kikao afu unakuja huku unatoa habari za vikao wakati ukiwa umeficha ID yako ni majungu.
 
Nimelazimika kurejea baada ya kuona kuna watu wanapotosha hoja yangu,

Hivi Shibuda si alisema posho iwe milioni kumi na mbili kama Zitto wakamtishia kumwondoa hata ubunge?
Shibuda alisema isiitwe posho bali ujira wa Mwiha , si alishitakiw kwenye kamati kuu ya chama chao?

Sasa tofauti ya Zitto na Shibuda iko wapi hapo? ukisimamia jambo hakikisha unalisimamia mpaka mwisho na sio kuyumba yumba kwani huo ndio unafiki.
Kwani wewe binafsi msimamo wako nini? bona unapenda sana kuwa mfuasi
 
Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.
 
..ukisimamia jambo hakikisha unalisimamia mpaka mwisho na sio kuyumba yumba kwani huo ndio unafiki.
Mbona msimamo wake unaeleweka tu....na kubwa zaidi ameacha kuchukua kile anachokikataa! Labda kama unasema ameanza kuchukua posho tena hapo nitakuelewa.
 
Hivi unajua kuwa Mbunge analipwa shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya mafuta kwa mwezi na maana yake ni kuwa kila siku anapewa shilingi 83,333 sawa na lita 37.87 kwa bei ya shilingi 2,200 kwa lita , hata siku ambazo tunakaa Dodoma?

Kuna haja gani ya Mbunge wa Viti maalum kupewa hizo fedha wakati hana hata jimbo la kutembelea? Kuna haja gani wabunge wa majimbo ya mjini kupewa hizo fedha kila mwezi? kwanini pasiwe na ratiba kuwa kwa wakati wote wa vikao vya kamati na vile vya bunge hawatalipwa mafuta? Kwanini Zitto anataka kusema kuwa waseme wanahitaji fedha kwa ajili ya mafuta?

Naomba kuishia hapo , ntarejea baadae kidogo.

mamaaaaaa....hizo za mafuta mbona zimepita take home yangu mara nyingi sana???nina degree,maji marefu darasa la nne..at the end of their term,a tax free gratuity to the tune of 40+million!!!!!bado mmejiongezea miposho ya kukaa kitako ambayo inakaribiana sana na kamshahara kangu..give me machete and i'll take it to the bush muthaf**k*z
 
Niliandika hii habari nikiwa sijui lolote na kumbe ni kweli utafikiri nilikuwepo. Nilisema Mbunge wa Sikonge ni kasheshe....

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa anadaiwa kwamba alitumia mafumbo kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza kupinga nyongeza hiyo ya posho. Kauli hiyo inadaiwa kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM. "Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa gari, nyumba na analipwa na chama," kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba.
Nina wasiwasi atakuwa Mbunge wangu.

Inabidi afuate mstari wa ndugu yake Kigwangala....
 
Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.


Nashukuru umewaeleza wazi kuwa ni kweli jana ulisema kuwa hupingi suala la maslahi zaidi kwa wabunge , ila tatizo ni hayo masilahi kuitwa posho.

kwa hiyo unaeleza nini hapo kuwa ni sisi wabunge tuu ndio maisha yamepanda ?
 
When you decide to be a looser, don't involve others.
kama wewe umejikatia tamaa, tulia tu,
kama umeajiriwa, basi fanya kazi, ngoja upate mshahara mwisho wa mwezi na ukalipe bills,
kama hautatosha, kakope kwa duka la Mangi.

Nijikatie tamaa jambo gani? Tehe
 
Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.

mkuu Zito,mbona umewadanganya vijana kuwa utapeleka hoja binafsi ya tatizo la ajira kwa vijana kwenye bunge liloanza jana??na hili unalizungumziaje ikiwa wapambanaji vijana walikuwa wanaisubiria kwa hamu hoja iyo.
 
Back
Top Bottom