Ole wako Tanzania, viongozi vijana ni wanafiki haswa Zitto: Posho alisema hivi... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ole wako Tanzania, viongozi vijana ni wanafiki haswa Zitto: Posho alisema hivi...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mwongozowaspika, Jan 31, 2012.

 1. m

  mwongozowaspika Member

  #1
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

  Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

  Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

  Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

  Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema "Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho" ………….

  Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema "Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana"

  Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

  Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

  Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.
   
 2. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  una matatizo ww.hujui kuwa ukija na hoja ya kuongeza mshahara utabanwa kwa style nyongine.inajulikana mishahara ni midogo bt watu wanataka posho kubwa.
   
 3. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  wewee ni mbunge? huoni kama hata wewe una jukumu la kupinga kwa nafasi yako kwani zitto alizaliwa kukuonesha kila mwelekeo na kama uligundua hoja ya zitto awali ilikuwa sahihi mbona hukutoka hadharani kumuunga ili asikate tamaaa weka pia sababu kwa nini huwezi wewe kupinga hadharani? lakini pia kumbuka zitto si msaafu wa vijana nchi hii wala siye QURAN AU BIBLIA kuna vijana wengi bado tunawangazia macho
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Huyu mbunge feki hata sijui wajimbo gani, wewe unategemea zitto atetee nchi na wewe umshangilie tu pembeni hv wewe ni wale wakupewa nini?
   
 5. m

  mwongozowaspika Member

  #5
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo kuna watu mnashambulia bila kujua mantiki ya hoja yangu, soma gazeti la Mwananchi la leo utaona kifungu walichomnukuu Zitto akisema kuwa tatizo wabunge they think small...... hapo hapo anasema kuwa walipaswa kujenga hoja kuwa nishati ya mafuta imepanda bei na hivyo ndio iwe sababu ya kueleza umma kuhusiana na nyongeza ya posho .......hapo unaweza kuona namaanisha kitu gani.
   
 6. m

  mwongozowaspika Member

  #6
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zitto ni mnafiki hakuna anachotetea , ila anatafuta hoja za kuugilibu umma wa watanzania ,huku akiwa kwenye vikao ni unafiki mtupu anaendekeza , nimeamua kuweka wazi hapa na kama anabisha aeleze kwenye press yake anayotegemea kuifanya leo nini alisema kwenye kikao.
   
 7. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Zitto amewadanganya vijana kuhusu ahadi ya kupeleka hoja binafsi ya tatizo la ajira kwa vijana..kwa hili nitaendelea kumweka kwenye list ya wanasiasa wanaotumia matatizo ya vijana kama ngazi ya kuelekea anapotaka.
   
 8. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kaka zitto haaminiki kama zamani sawa hapo tunakuunga wewe je umefanya nini? bora yake anavibrate
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nina wasiwasi atakuwa Mbunge wangu.

  Inabidi afuate mstari wa ndugu yake Kigwangala....
   
 10. Mamzalendo

  Mamzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jan 31, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,664
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Kwa maneno yake hayo kwa kweli ni mnafiki,tena anacheza na akili za watz,lakini mi naamini ipo siku mapinduzi yatatokea katika nchi hii,
   
 11. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mbunge umesema tumekusikia na sasa acha watu wafuatilie na ukweli utajulikana .Lakini na wewe je uko kufanya nini? Unaitaka posho ? Au kwa kuwa uko CCM huwezi kusema hapana unaogopa kuitwa nakuulizwa ?Sasa kama wewe unashindwa kusema kwa nini Zitto ? Mbona wewe hufanyi kama Zitto uudanganye umma then mkiwa ndani uwe namwelekeo tofauti ?
   
 12. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Jadilini hoja yake acheni kumjadili yeye.
  Ni kweli kwamba ZITTO ndio aliishikia hii hoja bango kabla haijafika bungeni na baada
  ya kufika bungeni, Mimi binafsi kama Mwananchi na mlipa kodi mzuri niliishaweka msimamo
  wangu hapa kwamba hizo posho kwa wabunge ziachwe ziongezeke na wakati wote
  nilikuwa napata shida sana kumuelewa zitto alikuwa anaelekea wapi na msimamo wake
  wa kupinga posho kiasi cha kukataa hata kusign dafutari la mahudhurio kwenye vikao
  vya bunge ili kukwepa posho

  Sasa, kama ni kweli kwamba ZITTO katoa kauli za namna hiyo basi anastahili kuitwa
  "Kijana Mnafiki of our time"
   
 13. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  wewe nawe ni mnafiki kama huyo unayemtuhumu,kwani yeye ni bosi wako?msimamo wako ni upi?au wewe ni mzee?
   
 14. n

  nongwa fadhili New Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala la posho ci jambo dogo kama tunavyodhania ndo mana hata pm wakati anajibu hii hoja alisema kabisa kwamba wataliendea taratibu kuona ni jinsi gani zinaweza kupunguzwa....sasa tatizo tunaleta ushabiki mbele bila ya kufafanua ukubwa wa posho na wapi zikatwe....unafiki sio zitto peke yake wapo wengi tu kwenye suala hili la posho...kuanzia wenyeviti wote wa vyama..makatibu...hata wanachama.angalia migogoro...ya CUF,NCCR,TLP...posho ni moja chanzo cha migogoro..MTAZAMO TU HUO
   
 15. m

  mwongozowaspika Member

  #15
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]
  hii ni sehemu ya gazeti la Mwananchi leo,


  JK abariki posho mpya za wabunge

  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Monday, 30 January 2012 20:54 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0diggsdigg  [​IMG] Rais Jakaya Mrisho Kikwete

  KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGA


  Waandishi Wetu, Dodoma

  WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku. Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.


  Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.


  Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000. Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.


  Katika kikao hicho baadhi ya wabunge wanadaiwa kuwashambulia Zitto, Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Khamis Kigwangwala kwamba wamekuwa mstari wa mbele kupinga posho hizo hadharani. Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye anadaiwa kwamba aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanafuta umaarufu wa kisiasa.  "Wanachotafuta ni umaarufu wa kisiasa tu, mimi ninavyojua umaarufu wa kisiasa unakuja kwa kufanya kazi za kibunge za wananchi lakini siyo kupinga posho," chanzo chetu cha habari kilimnukuu Makinda.  Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa anadaiwa kwamba alitumia mafumbo kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza kupinga nyongeza hiyo ya posho. Kauli hiyo inadaiwa kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM. "Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa gari, nyumba na analipwa na chama," kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba.  Pia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), anadaiwa kumshambulia Zitto kuwa lazima apinge posho hizo kwa sababu, anapewa fedha na wafadhili kutoka nchi za nje. "Shelukindo anasema amefanya ziara nje na kuhakikisha kuna wahisani wanamfadhili Zitto kwa hiyo ana haki ya kupinga posho hizo," chanzo chetu hicho kilimkariri Shelukindo.


  Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya mashambulizi hayo, Dk Kigwangwala alisimama kutetea msimamo wake kwamba ongezeko hilo halina ‘mashiko' na haliwezi kuelezwa mbele ya umma likaeleweka, lakini alizomewa na wabunge wengi huku wakimtaka kukaa chini.  Hatua hiyo ilisababisha Zitto kusimama na kueleza kuwa tatizo la wabunge kwamba wana fikra finyu, kauli ambayo alitakiwa na wenzake kuwaomba radhi kuwa amewatukana. "Zitto ametumia Kiingereza kuwa tatizo la wabunge ‘we think small', Shelukindo na (John) Komba wakaja juu wakitaka kuwaomba radhi kwa kuwatukana," chanzo chetu kilieleza. Zitto anadaiwa kusema wabunge walitakiwa kujenga hoja ya kuongeza fedha za mafuta ya gari wanayolipwa hivi sasa Sh2.5 milioni kwa mwezi, kutokana na kupanda kwa nishati hiyo, lakini siyo posho

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 16. m

  mwongozowaspika Member

  #16
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuhusu umri nimejieleza hapo juu kuwa naonea huruma taifa langu kwani wale vijana niliowafikiria kumbe hawafai kuachiwa nchi maana ni wanafiki
   
 17. USTAADHI

  USTAADHI JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2012
  Joined: May 10, 2011
  Messages: 1,518
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  kwani zitto ndiye kijana wa vijana?
   
 18. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mbunge wa aina gani wewe!!! unatia aubu kutuletea huu upuuzi ili tumjadili mtu badala ya hoja!!!
   
 19. m

  mwongozowaspika Member

  #19
  Jan 31, 2012
  Joined: Jan 30, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Binafsi nilikuwa namwona kama nuru miongoni mwa vijana viongozi wa kisiasa nchini ,ila tangu jana nimesema ntakuwa namsikiliza kwa masikio mawili na kumtizama kwa macho mawili , nitapima kauli zake kwa kina sana .
   
 20. K

  Konya JF-Expert Member

  #20
  Jan 31, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Sidhani kama huyo zito sasa awe ndo sportlight ya watz hasa vijana kwa kila atakalolisimamia,naamini kabisa watz wa leo ni wafuatiliaji wazuri tu wa mambo mnayoyafanya na ww ukiwa mmoja wao kama kweli na ww ni mbunge,unachotaka kutuaminisha ni kipi?labda ni kumchongea huyo zito,ingekuwa bora ukatupa msimamo wako,au na ww ndo walewale mnaoongozwa na maslahi ya chama zaidi au kisa habari zako hazikuandikwa na mwananchi..ningependa kama utatueleza msimamo wako khs posho
   
Loading...