Ole wako Tanzania, viongozi vijana ni wanafiki haswa Zitto: Posho alisema hivi...

Mleta habari na wewe ni mnafiki, kwa sababu hujatuambia mpaka sasa wewe unasimama upande gani katika suala hili la posho, na lini umewahi kutoa msimamo wako kuhusu posho ili watanzania wote wakujue , mbona zitto, kigwangala na makamba misimamo yao inajulikana kwa kila mtanzania na kwa nini watu wote mnaangalia mtu mmoja tu akiwa anarusha mawe, kama mnaona kuna umuhimu wa kumsaidia kurusha hayo mawe kwa nini msifanye hivyo ila mnasubiri mpaka hayo mawe yanapoanza kumwangukia miguuni ndipo muanze kumlalamikia kuwa tulikuamini utayarusha kumbe yamekushinda
 
Binafsi nilikuwa namwona kama nuru miongoni mwa vijana viongozi wa kisiasa nchini ,ila tangu jana nimesema ntakuwa namsikiliza kwa masikio mawili na kumtizama kwa macho mawili , nitapima kauli zake kwa kina sana .

Ina maana siku zote ulikuwa unamsukiliza Mh. ZITTO kwa sikio moja na kumuangalia kwa jicho moja? Kafie mbali kule M:S:H:E:N:Z:I mkubwa wee! Ubinafsi umewajaa hadi mmewa sahau waTanzania wenzenu.

Nina hakika hata hao walio kuchagua uwawakilishe ni hamnazo kama wewe.
 
Huyu mleta mada ndiye mnafiki na siyo Zitto. Zitto alichozungumza kama ni kweli kasema hivyo anaeleweka kwamba anapinga mbunge kuja Dodoma kufanya kazi za kibunge akiwa tayari amelipwa perdiem yake ya kuishi Dodoma then analipwa tena hela nyingine kwa mfumo wa posho kwa kufanya ile kazi iliyomleta Dodoma in the first place. Hii haileti akilini. Na Zitto yupo sahihi katika hilo. Wanafiki ndio hawataki kumwelewa maana wanangangania posho kwa sababu posho haikatwi kodi. Okay maisha yamepanda...lakini maisha yakipanda kwa mbunge si kinachostahili kuongezwa pale ni perdiem au mshahara? Wao wanangania posho kwa sababu posho haikatwi panga la kodi. Ufisadi wa kitaasisi. Mantiki kuu ya Zitto ni kutafutwa kwa mechamism ya kulipana maslahi yenye sound justification. Posho si mfumo halali wa malipo stahili kwa mtu yeyote yule awe mbunge au mtumishi yeyote yule wa umma. Kila kazi ina ujira wake na kazi ya mbunge ujira wake ni kwenye mshahara kama ilivyo kwa watumishi wengine. Kama wabunge wanastahili hayo maslahi basi yaongezwe kwenye mshahara na hilo litaeleweka hata kwa watu wengine. Implication yake ni kwamba hata scale za mishahara ya watumishi wengine nazo zitapaswa kupanda. Hilo Zitto pia analifahamu na sijaona unafiki wake katika hilo. Mleta mada ndie mnafiki namba moja. Analenga kumwaibisha Zitto kwa mambo ya vikao vyao vya kinafiki walivyojadili kinafiki lakini anayaleta JF. Jinsi ulivyo mbea hata hivyo kuna evidence gani kwamba umemquote Zitto verbatim bila kuspin chochote kwenye matamshi yake?
 
Mtoa mada wewe ndio mnafiki.wewe ni mtetea posho halafu unaongea upupu. Hatudanganyiki kirahisi hivyo.weka jina lako halisi hapa tuwape pole wapiga kura wako kwa kuchemsha.
 
Najaribu kutafakari mantiki ya hoja yako lakini pia natafakari katikati ya mistari miwili, ambcho nimekuwa namsoma Heavy (Zitto) siku zote ni kUKATAA SITTING ALLOWANCE............yamkini hakuna kiswahili sanifu cha hili maana hata ukiita posho ya kiti ni direct translation so aliposema anakataa neno posho labda wewe uliyekua kikaoni umefupisha ...........najaribu kuelewa katika hili......kwamba kwa nini umlipe mbunge posho ya kiti ilihali anatimiza majukumu yake????

all in all yamkini pia ni mchezo wa maneno tu...kwamba si zitto yule tena na huenda ni baada ya kumtia mkwara kwamba akikataa nyongeza ya
mtamuanika.........lakini yote kwa yote mtueleze kinagaubaga enyi wabunge kimsingi wote mna tamaa ya fedha tu ndio maana umeambiwa tujadili hoja si mtu......................wewe unaona ni haki kulipwa kiasi hicho??

(Je ni kweli kwamba kuna mkakati sehemu ya pesa hizo zitarudi gambani? (yaani ikishapanda mtachangishwa 50,000/= kila posho ili kuchangia chama kwa next election?)
 
Mtoa mada wala asiwangaishe maana naamini ni Juma Nkamia mchumia tumbo...nakumbuka akiwa kwenye mjadala BBC alishasema kuwa labda Zitto anapinga posho kwa sababu yeye mwenzake miaka mitano ya ubunge kesha jijenga. Kwa yale maneno yake huyu Mwongozo wa spika as know as Juma Nkamia anataka posho ajenge, afungue biashara ya saloni ili apate mahari pa kupigia umbea kama huu hapa.
 
kwa maelezo ya mleta mada kama kweli ni mbunge basi tuna wabunge wa kipekee,maana ktk kuyajadili maslahi ya wabunge kwa aidha posho au mshahara lazima itambulike kinaongezwa nin na kwa ongezeka la kazi gani ndiyo principle,sasa huyu anayejiita mbunge mbona ni kama haelewi anacho kizungumzia jamani.au wenzangu mmemwelewaje?pia kadri viongozi na wabunge wa chadema wanapotoa neno nimegundua kuna watu wanachanyikiwa na kuvurugika akili kabisa.ukweli ni kwamba mh.zito yupo sahihi na bado kasimamia hoja yake kwa kueleza kuwa lazima kinachoongezwa kiendane na majukum na sio kufikiria hzo cheap politics za mara tumembana mara katuruka.2015 will talk in deep wakuu!
 
Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema “Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho” ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema “Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana”

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.

Kwa hali tuliyofikia ni heri kuwa angalau na wanafiki wengi kama Zito kuliko kuwa na mbunge kama ww unayesubiria kumkosoa Zito, je ww umefanya nn kupinga posho!
 
Usituletee sie mambo ya 'namheshimu zitto na yeye ananiheshimu...' Wewe ni nani? Tunamfahamu zitto lakini hatumfahamu Mwongozowaspika! Hebu jiweke wazi kwanza ndio uje na hizo tunaheshimiana! Ila kumbuka tu kuwa kuna tofauti kati ya mshahara na posho vilevile kati ya nyongeza ya mshahara na nyongeza ya posho.
 
Kwa upande mwingine zeto kama ni ndumila kuwili vile kwa upande wa ccm yumo cdm yumo kupinga posho huku anapokea yumo yani hata simwelewi elewi vile
Siyo lazima kila hoja uchangie hata kama hujafanya utafiti. Ni lini ulisikia au kuona Zitto akikubali ama kupokea posho?
 
Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema “Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho” ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema “Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana”

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.

Wewe ndio zumbukuku kweli, inaonekana hujui hata nini kilikupeleka huko bungeni. Sababu za Zitto kupinga ziko dhahiri kama ifuatavyo:-

a) Ili pawepo na nyongeza ya mishahara ni laziam iwepo justification ya ongezeko hilo kwa ulinganifu na kada zingine za wafanyakzi katika nchi.
b) Mishahara ya wabunge ikiongezwa ni dhahiri kuwa kodi inayokatwa toka mishahara hiyo itapanda hivyo serikali kupata mapato zaidi. Lakini posho kuongezeka serikali haipati chochote ndio maana zitto anapinga nyongeza ya posho kwa kuwa yeye ni mchumi anafahamu hilo.

Sababu ingine ya Zitto kupinga ni "spira; effect" ya ulafi wa wabunge. Ni ukweli usiopingika kuwa madakatari mika nenda rudi wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ya malipo duni lakini wakivumulia kutokana na kuelewa kuwa uchumi wa Tanzania ni mdogo. Lakini ni ukweli usiopingika kitendo cha wabunge walafi kama ninyi ndio chanzo cha mgomo huu wa madkatari kudai nyongeza ya posho na mishahara; kwa maneno mengine ninyi wabunge walafi msiokuwa na hekima wala busara ndio mnahusika na vifo vyote vilivyosababishwa na mgomo huu kwa kujali zaidi maslahi yenu badla ya wabunge kuwa sauti wa watumishi wengine wote. Hii ndio sababu nyingine ya Zitto kupinga alifahamu madai hayo ya nyongeza ya posho yatasababisha hali ya uvunjifu wa amani hapa nchini.
 
Jana nimeisikitikia sana nchi yangu Tanzania, na haswa kwa kuwa na kizazi cha viongozi vijana ambao nilikuwa naona kama wangeliweza kuja kulisaidia hili taifa hapo siku zijazo , lakini nimegundua kuwa kumbe ni wanafiki. Naomba kurudia ni wanafiki.

Hawa ni kijana Zitto Kabwe ambaye kwa kweli ananiheshimu na mimi namheshimu sana kutokana na hoja zake pamoja na kuwa tuko itikadi mbili tofauti.

Jana tukiwa kwenye kikao cha kamati ya wabunge wote kwa ajili ya kupewa briefing na wenzetu walioko serikalini kama ulivyoutamaduni wetu kabla ya kikao cha bunge kuanza ,mjadala mkubwa sana ulikuwa kwenye suala la posho za wabunge.

Zitto , ni mtu ambaye alijipambanua kuwa yeye anapinga ongezeko la posho hizo kwa nguvu zote , baadhi yetu tulimwamini pamoja na ukweli kuwa wengine hatuwezi kusema kutokana na sababu mbalimbali ila leo kaonyesha unafiki wake mbele yetu na hata wabunge wa chama chake walimpinga waziwazi bila hata kujali kuwa ni kiongozi wao na alikuwa ndiye mkuu wa kambi ya Upinzani kwani Mbowe hakuwepo.

Naomba ninukuu kauli yake na kama anamheshimu Mungu na kumwogopa atakubaliana nami na kuwaomba radhi watanzania , alisema “Kimsingi mimi sipingi suala la kuwaongezea wabunge Maslahi yao hata kama nyongeza hiyo ikikubaliwa kufikia kiasi cha shilingi milioni 12 kwa mwezi, ila ninachopinga ni nyongeza hiyo kuitwa posho” ………….

Hayo ndio maneno ya kiongozi huyu na alipomaliza kusema akabanwa na wabunge wengine ambao walimtaka awaombe radhi kwa kuwadhalilisha mbele ya umma , kumbe anakubaliana na kuongezwa kwa masilahi ya wabunge , kibaya zaidi alipobanwa akaomba radhi kwa kusema “Kama kuna mtu ambaye nimemkwaza kwa maneno yangu juu ya suala hili basi ninaomba aniwie radhi sana”

Kauli hii ikanifanya nimuone Zitto kuwa mnafiki kwani alipaswa kusimamia maneno yake na huo ndio uongozi , kuanzia leo nitaanza kumtazama kwa macho mawilimawili.

Kilichoniudhi ni hii tabia ya undumilakuwili, yaani akiwa kwa wananchi anapinga kuongezwa kwa masilahi ya wabunge na yeye anasema kuwa hilo sio sawa kwani maisha yamepanda pia kwa wananchi na watumishi wengine , sasa kusema kuwa hapingi nyongeza ila anapinga jina la hiyo nyongeza ni jambo la ajabu kabisa, kwani inaonyesha hana Principal ya msingi anayoisimamia.

Kwa kifupi na kwa kuwa leo nimeandika kwa mara ya kwanza naomba kuishia hapo, Ahsanteni sana.

Mtoa hoja hii amenistua na kunishangaza kiasi, maana kwa maelezo yake inaonyesha yeye ni Mbunge hila wana itikadi tofauti na Mh.ZITTO kwa mtazamo wangu anamahanisha wapo vyama tofauti maana chama ni ITIKADI na SERA. Lakini kinachonishangaza mbona mbunge wewe ni muoga na mnafiki, mbona ujiweki wazi tukakujua wewe ni nani? unaogopa nini wakati wewe ni mwakilishi wa wananchi? ZITTO yumo humu JF akijiweka wazi kwa jina lake, Dk Kigwangala naye tunae kajiweka wazi bila kificho. Kama unataka tuamini taarifa yako kuhusu UNAFIKI wa ZITTO jiweke wazi ili kama kuna ukweli ZITTO ashindwe kukanusha lakini kama ni uongo akanushe wazi ili wabunge waliomo humu JF watueleze mkweli kati yenu ni nani? Si vyema kutueleza kilichojili kikaoni na kumnyooshea kidole mwenzako halafu usemi wewe ni nani? inawezekana ukawa mwana CDM mwenzake unajidai kuwa mnatofautiana kiitikadi ili asikutambue jiweke wazi ili kusiwe na unafiki.

kifupi tuwekane wazi wewe kama Mh. Mbunge msimamo wako kuhusu posho ni hupi? sio unaeleza ya ZITTO kumbe na wewe ni walewale kuwa jasiri kama Mh. SHIBUDA kaweka wazi msimamo wake japokuwa hupotofauti na chama chake lakini kaamua kuwa wazi ili sisi wananchi tumjue yeye yupo upande gani ktk sakata la posho. Kama ZITTO ni MNAFIKI wewe je? Isije kuwa wewe ni MSALITI kwa watanzania kwa kuunga mkono posho hizo hivyo unatupa taarifa hiyo ili kutuambia mtetezi wenu wa kupinga posho kesha chemsha hivyo tumsulubu(wakati na wewe una usafi wowote na nia njema kwa Watanzania)
 
Zitto ni mnafiki hakuna anachotetea , ila anatafuta hoja za kuugilibu umma wa watanzania ,huku akiwa kwenye vikao ni unafiki mtupu anaendekeza , nimeamua kuweka wazi hapa na kama anabisha aeleze kwenye press yake anayotegemea kuifanya leo nini alisema kwenye kikao.

we umetumwa huna lolote sema wewe unasimamia wapi, umbea tupu mbona hujasema ID yako ya ukweli unafiki mtupu na kumuonea wivu ZITTO kwenye hicho kikao tulikuwemo wote na kwa taarifa yako tunakufahamu umejaribu kutafuta umaarufu kwa nguvu kubwa ila umeangukia pua una hadi tuhuma za kuuza mwili wewe.
 
Back
Top Bottom