Hufai kuwa Mbunge kama kweli wewe ni Mbunge. Umeshindwa kuelewa hoja ya Zitto kuhusu utofauti wa posho na maslahi mengine kama mshahara? Zitto amesema hapo hapendi hilo neno posho kwa vile ni la kiujanja ujanja katika ulipaji kama ni malipo ya kiutumishi yawekwe hivyo maana yatakuwa wazi zaidi na yatahusisha vyombo vingi vya umma kujadili hivyo kuongeza uhalali wake sio hayo maposho ya kusinzia yanayojadiliwa gizani.Binafsi nilikuwa namwona kama nuru miongoni mwa vijana viongozi wa kisiasa nchini ,ila tangu jana nimesema ntakuwa namsikiliza kwa masikio mawili na kumtizama kwa macho mawili , nitapima kauli zake kwa kina sana .
Mhe Zitto kajitaja jina na ww jitaje basi maana hakuna mbunge anaitwa Mwongozowaspika,pili mimi nina wasiwasi utakuwa ni mwandishi wa Mtanzania au Jambo leo?Sasa kama alitoka nje na kuwaambia they think small kwa nini walikasirika?Kumbe hizo hela mnazitumia majimboni maana mnalalamika ya kuwa mmekimbia majimboni?Zitto ni mfuasi wa anachokiamini na sio mshabiki kama wewe!Nashukuru umewaeleza wazi kuwav ni kweli jana ulisema kuwa hupingi suala la maslahi zaidi kwa wabunge , ila tatizo ni hayo masilahi kuitwa posho.
kwa hiyo unaeleza nini hapo kuwa ni sisi wabunge tuu ndio maisha yamepanda ?
Mwongozo wa spika,asante kwa taarifa,huo ni mkuki mwingine kwa makamanda wa ukweli.
Mungu tusaidie.
Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.
naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.
Binafsi nilikuwa namwona kama nuru miongoni mwa vijana viongozi wa kisiasa nchini ,ila tangu jana nimesema ntakuwa namsikiliza kwa masikio mawili na kumtizama kwa macho mawili , nitapima kauli zake kwa kina sana .
hii ni sehemu ya gazeti la Mwananchi leo,
JK abariki posho mpya za wabunge
Send to a friend
Monday, 30 January 2012 20:54
0diggsdigg
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGA
Waandishi Wetu, Dodoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku. Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.
Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000. Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.
Katika kikao hicho baadhi ya wabunge wanadaiwa kuwashambulia Zitto, Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Khamis Kigwangwala kwamba wamekuwa mstari wa mbele kupinga posho hizo hadharani. Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye anadaiwa kwamba aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanafuta umaarufu wa kisiasa.
Wanachotafuta ni umaarufu wa kisiasa tu, mimi ninavyojua umaarufu wa kisiasa unakuja kwa kufanya kazi za kibunge za wananchi lakini siyo kupinga posho, chanzo chetu cha habari kilimnukuu Makinda.
Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa anadaiwa kwamba alitumia mafumbo kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza kupinga nyongeza hiyo ya posho. Kauli hiyo inadaiwa kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM. Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa gari, nyumba na analipwa na chama, kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba.
Pia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), anadaiwa kumshambulia Zitto kuwa lazima apinge posho hizo kwa sababu, anapewa fedha na wafadhili kutoka nchi za nje. Shelukindo anasema amefanya ziara nje na kuhakikisha kuna wahisani wanamfadhili Zitto kwa hiyo ana haki ya kupinga posho hizo, chanzo chetu hicho kilimkariri Shelukindo.
Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya mashambulizi hayo, Dk Kigwangwala alisimama kutetea msimamo wake kwamba ongezeko hilo halina mashiko na haliwezi kuelezwa mbele ya umma likaeleweka, lakini alizomewa na wabunge wengi huku wakimtaka kukaa chini.
Hatua hiyo ilisababisha Zitto kusimama na kueleza kuwa tatizo la wabunge kwamba wana fikra finyu, kauli ambayo alitakiwa na wenzake kuwaomba radhi kuwa amewatukana. Zitto ametumia Kiingereza kuwa tatizo la wabunge we think small, Shelukindo na (John) Komba wakaja juu wakitaka kuwaomba radhi kwa kuwatukana, chanzo chetu kilieleza. Zitto anadaiwa kusema wabunge walitakiwa kujenga hoja ya kuongeza fedha za mafuta ya gari wanayolipwa hivi sasa Sh2.5 milioni kwa mwezi, kutokana na kupanda kwa nishati hiyo, lakini siyo posho
Hivi unajua kuwa Mbunge analipwa shilingi milioni 2.5 kwa ajili ya mafuta kwa mwezi na maana yake ni kuwa kila siku anapewa shilingi 83,333 sawa na lita 37.87 kwa bei ya shilingi 2,200 kwa lita , hata siku ambazo tunakaa Dodoma?
Kuna haja gani ya Mbunge wa Viti maalum kupewa hizo fedha wakati hana hata jimbo la kutembelea? Kuna haja gani wabunge wa majimbo ya mjini kupewa hizo fedha kila mwezi? kwanini pasiwe na ratiba kuwa kwa wakati wote wa vikao vya kamati na vile vya bunge hawatalipwa mafuta? Kwanini Zitto anataka kusema kuwa waseme wanahitaji fedha kwa ajili ya mafuta?
Naomba kuishia hapo , ntarejea baadae kidogo.
msimamo wangu upo hapo juu kwani nimesema wengine kutokana na sababu mbalimbali hatuwezi kusema hadharani , ila tunawaunga mkono wenye uwezo wa kusema .
Mimi hata kama hakutakuwa na posho nina uwezo wa kuendelea kuishi kutokana na pension yangu ni nzuri tuu kwa wastani wa maisha ya kitanzania .
ZITTO naomba nikujibu in person.Naomba msiwe distracted na watu. Msimamo upo wazi kabisa. Hakuna posho za vikao (sio tu nyongeza bali mfumo mzima wa posho za vikao twataka ukome. Watu wameamua kutwist nilichosema bungeni jana. Narudia, lazima tupinge posho hizi. Kwa nini wabunge walipwe kwa kukaa kitako? Huyu anayesema mie mnafiki yeye aseme anaunga mkono posho za kukaa au la. Wapiganaji msiwe distracted.