ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,460
Naongelea maisha ya Boarding school hasa - O'level kati ya mwaka 1985 - 1995. Nitajikita zaidi Kilimanjaro hasa katika shule zifuatazo
Moshi Technical, Kibosho Girls, Weruweru, Masama Girls, Eliboru (Arusha), Umbwe Sec, Kiraeni Girls, Marangu Sec, Old Moshi, Kibohehe Sec, Kolila Sec
Sisi Mafundi wa Moshi Tech tuliambiwa mikono yetu imekomaa, watoto wa weruweru walipenda kucheza na eliboru secondary. Wakati huo madisko yalikuwa ya kishule shule bila kuvaa kisawasawa huwezi ibua mtoto kucheza naye mziki.
Nakumbuka mavazi ya wakati ule yalikuwa na kitanashati kweli kweli Mokasini shoes, Suruali ya mchelemchele na mkanda wake, Shati( Single color) ya mikono mirefu na neck tai au wengine walipiga Suluari za Jeans mawingu-mawingu mashati ya bahama bahama na Raba mtoni- mimi na marafiki zangu tulipenda kuvaa hivi - Nilipenda kupiga Punk glasses kujiweka swa -dakta.
Kama mzazi wako hana ma-peni ilikuwa shughuli- maana hutakuwa na upenyo wa kujihusisha kwenye social activies kama hizi maana kivazi kinakuwa tatizo kwako na kwenye kundi la machekibobu unakuwa humo sababu madisko yalikuwa yanatakiwa michango kwanza then mnakodi Bus linakuja kuwachukua na kuwarudisha.
Kwa wadada walikuwa wanapiga gauni smart ndefu na viatu mokasini za kike hasa rangi Nyeusi au nyeupe.
Kuna shule zilikuwa matawi ya juu kama Kibosho girls - wasichana wanakuja disko wote walikuwa na uwezo wa kupiga mokasini nyeusi gauni zilizoenda shule kisawa sawa, sasa kasheshe kuwaibua kucheza nao disko lazima uthamaminswe kutoka juu hadi chini - kama unalipa hapo ndiyo mtoto anaibuka anacheza na wewe. miziki ya slow (blues kama wengi wanapenda kuiita) ndo ilikuwa utata kupata mtoto wa kucheza naye.
Kulikuwa na wazamiaji wakuu hasa kutoka Kolila sec na Old moshi - hii mijemba ilikuwa inanusa disko hata likiwa wapi then inazamia - walinichekesha tu pale walipopitia maliwato ya kike kuzamia disko kule Kibosho ambalo moshi Tech tulikuwa tumealikwa. - disco likafungwa mlinzi alipigwa kwa sababu ya unoko wake.
Visting days bwana hazikukosa katika haya mashule, tulijitosa siku za weekend kutafuta watu wa kubadilishana nao mawazo wakati huo hakuna simu za kikononi (mobile phones)ilikuwa barua tena kupitia posta hadi mwenzako aipate ajibu then uconfirm visting day ilikuwa shughuli - Sisi wa Moshi Tech tulikuwa na mazoea kwenda Weruweru pale utawakuta watoto wamekaa kusuburi wageni - unafika mzee mkanda nje unajitambulisha kwa dada anayepokea wageni - mgeni anaitwa unalongaa then saa 12 kamili nje ya geti bye shuleni kwenu mwenda kuwatambia wenzako.
Ukiringanisha na sasa watoto wa o'level wanajichangaya sana kwenye madisko ya watu wazima - Sidhani kama wanapata fleva yetu - unajua mtoto wenzio ana nafasi yake. pale ilikuwa kitoto toto lakini hatukeshi.
Pamoja na hayo yote watu walifumua mitihani vilivyo, wakati huo kichwa chako ndiyo tuition - Naona ma Engineer kibao, wanahabari, Wahadhiri, Wanasheria wametoka shule hizi.