OLD SCHOOL DAYS - Mko wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OLD SCHOOL DAYS - Mko wapi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by ELNIN0, Apr 29, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Naongelea maisha ya Boarding school hasa - O'level kati ya mwaka 1985 - 1995. Nitajikita zaidi Kilimanjaro hasa katika shule zifuatazo
  Moshi Technical, Kibosho Girls, Weruweru, Masama Girls, Eliboru (Arusha), Umbwe Sec, Kiraeni Girls, Marangu Sec, Old Moshi, Kibohehe Sec, Kolila Sec

  Sisi Mafundi wa Moshi Tech tuliambiwa mikono yetu imekomaa, watoto wa weruweru walipenda kucheza na eliboru secondary. Wakati huo madisko yalikuwa ya kishule shule bila kuvaa kisawasawa huwezi ibua mtoto kucheza naye mziki.

  Nakumbuka mavazi ya wakati ule yalikuwa na kitanashati kweli kweli Mokasini shoes, Suruali ya mchelemchele na mkanda wake, Shati( Single color) ya mikono mirefu na neck tai au wengine walipiga Suluari za Jeans mawingu-mawingu mashati ya bahama bahama na Raba mtoni- mimi na marafiki zangu tulipenda kuvaa hivi - Nilipenda kupiga Punk glasses kujiweka swa -dakta.

  Kama mzazi wako hana ma-peni ilikuwa shughuli- maana hutakuwa na upenyo wa kujihusisha kwenye social activies kama hizi maana kivazi kinakuwa tatizo kwako na kwenye kundi la machekibobu unakuwa humo sababu madisko yalikuwa yanatakiwa michango kwanza then mnakodi Bus linakuja kuwachukua na kuwarudisha.

  Kwa wadada walikuwa wanapiga gauni smart ndefu na viatu mokasini za kike hasa rangi Nyeusi au nyeupe.

  Kuna shule zilikuwa matawi ya juu kama Kibosho girls - wasichana wanakuja disko wote walikuwa na uwezo wa kupiga mokasini nyeusi gauni zilizoenda shule kisawa sawa, sasa kasheshe kuwaibua kucheza nao disko lazima uthamaminswe kutoka juu hadi chini - kama unalipa hapo ndiyo mtoto anaibuka anacheza na wewe. miziki ya slow (blues kama wengi wanapenda kuiita) ndo ilikuwa utata kupata mtoto wa kucheza naye.

  Kulikuwa na wazamiaji wakuu hasa kutoka Kolila sec na Old moshi - hii mijemba ilikuwa inanusa disko hata likiwa wapi then inazamia - walinichekesha tu pale walipopitia maliwato ya kike kuzamia disko kule Kibosho ambalo moshi Tech tulikuwa tumealikwa. - disco likafungwa mlinzi alipigwa kwa sababu ya unoko wake.

  Visting days bwana hazikukosa katika haya mashule, tulijitosa siku za weekend kutafuta watu wa kubadilishana nao mawazo wakati huo hakuna simu za kikononi (mobile phones)ilikuwa barua tena kupitia posta hadi mwenzako aipate ajibu then uconfirm visting day ilikuwa shughuli - Sisi wa Moshi Tech tulikuwa na mazoea kwenda Weruweru pale utawakuta watoto wamekaa kusuburi wageni - unafika mzee mkanda nje unajitambulisha kwa dada anayepokea wageni - mgeni anaitwa unalongaa then saa 12 kamili nje ya geti bye shuleni kwenu mwenda kuwatambia wenzako.

  Ukiringanisha na sasa watoto wa o'level wanajichangaya sana kwenye madisko ya watu wazima - Sidhani kama wanapata fleva yetu - unajua mtoto wenzio ana nafasi yake. pale ilikuwa kitoto toto lakini hatukeshi.

  Pamoja na hayo yote watu walifumua mitihani vilivyo, wakati huo kichwa chako ndiyo tuition - Naona ma Engineer kibao, wanahabari, Wahadhiri, Wanasheria wametoka shule hizi.
   
 2. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 499
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  umenikumbusha mbali......Weruweru disco ilikuwa inachezwa na taa kibao, kwenye disco walikuwa wanaingia kwa madarasa ua mabweni hakuna kuchanga. Walikuwa wanavaa uniform za shule kwenye disco isipokuwa graduation tu. Na disco ilikuwa mwisho saa 4........
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Du! umenikumbusha mbali sana.
   
 4. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Mie nilikuwa mwalimu kipindi hicho Elnino heshima yangu tafadhari ...
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Yeah, head wao alikuwa mkali sana yule mama, tuliwahi kutoa upepo basi lao one day ilipofika saa 4 walipotaka kuondoka, ilikuwa issue kubwa tukawa burnned kucheza nao disko kwa muda, yeah walicheza na uniform na mitaa kibao - wale mastaa zaidi walicheza kwenye taa karibu na DJ, wezangu mie walijifisha kwenye giza giza kwa nyuma.
   
 6. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #6
  Apr 29, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Aaaah nyi wote washamba wa mikoani kumbe.....
   
 7. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  teh teh teh, kama sikosei ukikuwa darasa la nne
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  teh teh teh, kijana unaweza kuzaliwa town wakaja watu wakakuzidi kwa kwenda mbele .... si wa kuja muzeee
   
 9. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Hapana nilikuwa skuli teacher wenu serious
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Apr 29, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Bush people can't tell me nothing...
   
 11. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #11
  Apr 29, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  sisi shuleni kwetu disco ilikuwa mwisho saa 12, then mnaenda kula mkumaliza mnaenda Prep. na mwalimu alikuwa anakuja kukagua mabwenini kama hakuna watu. hapo prep muda wote ni kusimuliana tu jinsi manjemba yalivyokuwa yanachemsha kwa kumwaga sera
   
 12. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,026
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Wao superb. Mnanikumbusha DABANGA CAMP -Minaki kwa O'Level na Old Moshi na Mzumbe kwa A'Level. Miye kazi yangu ilikuwa ni kuuza sigara ndani ya ukumbi hakuna kucheza wala mama yake kucheza, ni ujasiriamali kwa kwenda mbele. Blues unajikumbatia pekeyako hakuna cha mtoto. Aaaaaaaaaaaaaah! ni long time and funny
   
 13. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,026
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mshamba wa wapi ambaye hutoki ktk mkoa mmojawapo wa Tanzania?
   
 14. Bazazi

  Bazazi JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 18, 2008
  Messages: 2,026
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Mwalimu wa nini, wapi. Vp darasani hukuwa ukiona aibu kuwafundisha NYAMAUME zilizokuwa zimejaa madarasani. Si unakumbuka enzi zetu hizo umri wetu ulikuwaje na wewe ulukuwa mbado Ndito/Desii. Naamini wakati huo ulikuwa mzima kabisa; kitu na boksi
   
 15. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #15
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,202
  Likes Received: 1,007
  Trophy Points: 280
  Aah bwana eeh, mwataka kujipendelea nyie wa Moshi tu? Mie nakumbuka hapo Mazengo technical siku ya disko tulikuwa tunavaa nguo saa tatu asubuhi ambapo safari ya kuelekea kwa vimwana wa Msalato ni saa tisa. Uniform ilikuwa ni suruali nyeusi kwa shati nyupe na kwa siku hiyo ya disko hupuliziwa upupu(perfume) zaidi ya mara kumi. Nakumbuka second master wakati huo alikuwa akiitwa Msasa alijaribu kunishusha kwenye isuzu ya shule nisiende disco bila mafanikio japokuwa alikuwa mkali kama pili pili. Kwenye. J/tatu yake akanitoa mbele kwenye morning assembly na kuwatangazia wanafunzi wenzangu 'when i call this thing to get out of the school track he refused categorically, so now i send him home' nakumbuka alinigeukia akaniambia 'you have to run, run till to your parents house where you run no more'. Alieniokoa na suspicion ni Silvester Mkoba ambae ndie aliyekuwa heademaster wakati huo, kwa kunilamba mboko 4. Disco likiwa linaendelea mie nilijihusisha zaidi na ujasiria mali. Nilikuwa nauza Big G kwa kwenda mbele. Ole wao msalato wawaagize Bihawana sec kwenye disco lao, kufanya hivyo wangekuwa wametangaza vita na Mazengo. Kweli mleta tread umenikumbusha mbali sana. Na wakati huo maisha yalikuwa matamu mno.
   
 16. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #16
  Apr 29, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  ha haaaaaaaaaa, disko kwenda na isuzu. nakumbuka siku moja wakaka wa shuleni kwetu walialikwa disko shule ya wadada. sijui ilikuwaje lori likawa bovu, walienda na trekta. wenyewe wanasema walimwomba dereva awashushe mbali na shule ili wadada wasiwaone wamekuja na trekta. ila wanasema walifika hoii, si unajua mitikisiko ya trekta! halafu haliendi mnabaki kutikisika tu
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  aaaa we wa mujini hebu tuambie mafanikio yako tujustify kama unavyodaI umezaliwa mujini

  Wenzako wanjanja wa mjini huwa hawasemi, ila wanagundulika tu - sasa wewe unayebwabwaja tunamashaka may be umezaliwa Tuangoma au Kimbiji kule kwenye mashamba yetu then unadai we mtoto wa city.
   
 18. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #18
  Apr 30, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Yawezekana jamaa ni mkongomani - kazamia trein then anajifanya dogo wa town - teh teh teh
   
 19. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #19
  May 2, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mkono wa mara sec school pale kilosa haha niko unyoya(Form 1()hapo niliwakuta mapacha flani wakijiita dr no na dr yes na ndugu yao msela nondo, jamaa walipenda sana kusimulia mambo ya home kwao mpaka wakaonywa na mwalim asembly. mimi nta base kwenye mpira, kuna jamaa walikuwa wanapiga futbol balaa noma tupu. kuna jamaa alikuwa kazi yake kugonga kengele pale skuli wenyewe wakimwita mtaalam kitabazi, huyo jamaa nilikuwa simpendi coz alikuwa hasahau kugonga kengele hata siku moja kumi na moja na nusu mwana kengele inaita mchakamchaka hahaa mambo ya shule. kuna kina power same, jamaa alikuwa ananyanyua vyuma na mwana riadha lkn kila mashindano ya umiseta jamaa wa mwisho.
   
 20. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 218
  Trophy Points: 160
  Kiby,

  Siku ya disko maandalizi yalianza mapema - viatu vilipigwa kiwi na kuanikwa juani mapema - nguo kunyooshwa saa tatu asubuhi - kuoga mara mbili mbili teh teh.
  Wakati huo shule nyingi zilikuwa na malori - nakumbuka tulishapanda katala telu ( Lori la shule) kwenda disko pia
  Mzee ujasiliamani ulianza zamani, nakumbuka kuna jamaa pia kwetu alikuwa anauza maandazi toka form 1 hadi four - aliondoka na div four lakini pesa alipata nyingi.
  Shule za wavulana zilikuwa mahasimu - mfano Moshi Tech na Ilboru hatukupendana sababu ya weruweru.

  Ushirikiano

  Wakati huo sisi wanafunzi tulikuwa na ushirikiano mzuri sana, kwa wale wa mkoani tulikuwa tunasafirishwa na train tunalipiwa nauli na serikali, sasa utakuta mabehewa Mazengo Sec, Kirakara Sec, Msalato sec, Mzumbe, Tabora Boys, Old Moshi, Moshi Tech na zinginezo sasa we mzee zamia behewa lolote ili mradi una kitambulisho cha shule yako upo salama. Kasheshe mtu Raia azamie - duh tulikuwa na ushirikiano wa kutosha - lazima ashushwe apelekwe kituo cha police.

  Sasa bahati ukazamia behewa la Kirakala au Tabora Girls - duh humo inakuwa full mastory na kujiachia utapenda train lisifike kwenu maana ni story za masomo kwa kwenda mbele- wakati huo kupewa jina na anuani aisee ilikuwa dili kubwa sana.
   
Loading...