Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
aaah shemeji huyo kwenye red usingemtaja umenitonesha (alikuwa mkufunzi wangu)
afu kumbe nilichelewa kidogo tu we shem ningecheza 'disko' la welcome fomu wani na wewe.....
Shem, mie nilikuwa siku nyingi sana hapo Mazengo. Mkoba wakati anakuja Mazengo amenikuta. Enzi hizo ilikuwa shule ya WANAUME tu. Baadaye nikaja sikia imekuwa mchanganyiko. Pia siyo siri kuwa enzi hizo nilikuwa MSHAMBA wa kutupwa. Nilikulia Dar hadi nilipoanza kuzidisha utundu. Nikarushwa kijijini na sikuona wala Tabora mjini hadi nilipofika darasa la saba. Effect yake ilikuwa kubwa sana. Nilipofika Disco nilikuwa nashangaa tu. Enzi hizo pale Mazengo Disco linapigwa na wale watoto wa yule Mzee Wa Kinyamwezi mwenye kituo kinaitwa KAGUNILA Radio Service wale uwanja ya Jamhuri. Mzee alikuwa na Spika yule si kawaida. Mara ya kwanza niliona Spika ikitoa BASS peke yake. Ni baada ya miaka mingi sana nikaja kufahamu kuwa inaitwa SUBWOOFER. Hii ilikuwa mwanzo wa miaka ya 80. Baadaye akaja Mwalimu mmoja wa Kihaya na yeye akawa anatupigia Disco pale alikuwa akiitwa MGANYIZI. Mganyizi alitumika hata kwenye kukariri Periodic Table yaani "Lile Beda bovu Chonya Nipe Orange Fanya Nende, Na Mganyizi alivuta Sigara Paketi Sita Arusha..." Ahh Na-Sodium, Mganyizi-Magnesium......
Kuna mwalimu mmoja wa Kigogo alikuwa akifundisha Kiwahili, yeye alikuwa akiongelea ngono tu. Alinifanya nianze tabia ya kuangalia miguu ya wanawake. Unakuta linasema "Look her, from behind, her leg ........ hahahahaaa siyo chenzo bwana!!!!" Alikuwa akijisifu jinsi anavyofaulisha wanafunzi kwenye mitihani. Imekaribia mitihani tukagundua hatuelewi kitu. Ikabidi watu tukimbilie Mama mmoja wa Kipare akiishi Kikuyu Flats akiitwa Mwalimy Kasira kama sikosei. Tukamuomba notes zake na tukasoma tukitumia na yale aliyotufundisha zamani. Wagogo kweli ni WASANII.
Sasa Shem, kama ulifundishwa na Paramagamba sijui, na wewe alikuweka Ile alama ya 50 cent usoni? Maana Wagogo hawachelewi. Nilivyoona mara ya kwanza nikafikiri labda walipoona Train locomotive ila taa yake, wakaionea wivu na wao wakaamua WAWEKE ZAO usoni. Wagogo BANA!!!!