Old school days - Mko wapi?

Yeah, head wao alikuwa mkali sana yule mama, tuliwahi kutoa upepo basi lao one day ilipofika saa 4 walipotaka kuondoka, ilikuwa issue kubwa tukawa burnned kucheza nao disko kwa muda, yeah walicheza na uniform na mitaa kibao - wale mastaa zaidi walicheza kwenye taa karibu na DJ, wezangu mie walijifisha kwenye giza giza kwa nyuma.
Kiongozi! Kiongozi! Kiongozi!
Umenikumbusha mbali sana! Inawezekana tulisoma darasa moja.
Kampeni ya kulitoa upepo lile gari nami nilihusika.
Mwalimu Mpande nusura atukamate. Ingekuwa soo nakwambia.

Nakumbuka Sakata la kuingizwa pale uwanja wa tenis kwenye foleni ya waalimu wataalam wa kutandika bakora.....
Hapa Bob Kasenge, Hapa the killer Munuo........ Acha kabisa!
 
Aah bwana eeh, mwataka kujipendelea nyie wa Moshi tu? Mie nakumbuka hapo Mazengo technical siku ya disko tulikuwa tunavaa nguo saa tatu asubuhi ambapo safari ya kuelekea kwa vimwana wa Msalato ni saa tisa. Uniform ilikuwa ni suruali nyeusi kwa shati nyupe na kwa siku hiyo ya disko hupuliziwa upupu(perfume) zaidi ya mara kumi. Nakumbuka second master wakati huo alikuwa akiitwa Msasa alijaribu kunishusha kwenye isuzu ya shule nisiende disco bila mafanikio japokuwa alikuwa mkali kama pili pili. Kwenye. J/tatu yake akanitoa mbele kwenye morning assembly na kuwatangazia wanafunzi wenzangu 'when i call this thing to get out of the school track he refused categorically, so now i send him home' nakumbuka alinigeukia akaniambia 'you have to run, run till to your parents house where you run no more'. Alieniokoa na suspicion ni Silvester Mkoba ambae ndie aliyekuwa heademaster wakati huo, kwa kunilamba mboko 4. Disco likiwa linaendelea mie nilijihusisha zaidi na ujasiria mali. Nilikuwa nauza Big G kwa kwenda mbele. Ole wao msalato wawaagize Bihawana sec kwenye disco lao, kufanya hivyo wangekuwa wametangaza vita na Mazengo. Kweli mleta tread umenikumbusha mbali sana. Na wakati huo maisha yalikuwa matamu mno.
Naamini ni ile SUSPENSION
 
Upo sahihi kamanda, mwalimu Pande na Super Six zake ilikuwa hatari - Bob Kasenge nakumbuka aliingia Disko anamwambia DJ - Funga mziki kwa muda akaaza kutoka hotuba
" Mimi ndiyo Second Master wa shule hii - Karibuni wageni wetu - DJ hebu wawekee YESU MKOMBOZI....vijana wacheze" hapo kicheko kikubwa toka kwetu na wageni wetu. Yaani anamaanisha atuweke wimbo wa Umkomboti - wa Yvonne Chaka Chaka
 
Ngoja niendelee kuvuta memory kidogo.
Will be back shortly
Ochard..... Mama Hawa na vimbuzi vyake... Mzee Lekey na Nyuka.....
 
Na ule mpango mzima wa kuazima Viatu na Viwalo... Jamaa mmoja alikosa Sox... akakata Mikono ya Sweta ya njuka akaivaa... Duh tumetoka mbali...
 
Crispin na Elnino, naona nyie kweli mwafahamiana. Nilikuwa na mpango wa siku moja kuja hapo Moshi Tech kwani kuna bwana mdogo wangu mmoja kutoka Sikonge na babu yake ndiye alikuwa mwalimu wangu wa kwanza shule ya msingi alikuwa akisoma miaka hiyo hapo Moshi Tech Sec. Alikuwa akiitwa Peter M. Nimepotezana naye siku nyingi sana. Pana wakati mdogo wake aliniambia yuko Iringa ila mdogo wake pia kapotea. Alikuwa kijana mfupi, mtanashati na anavaa miwani. Mara nyingi akija kututembelea pale Technical College Arusha. Kama kuna mtu ana mawasiliano na huyu kijana Peter Mal. basi anipitishie kwenye PM.

Kuna kijana mmoja sijui kama Ciprian alikuacha pale Moshi. Alikuwa akiitwa Cathbert Busumano (mhangaza). Nilikuja kupata habari amefariki. Ila baadaye mdogo wake atakuwa alisoma na nyie maana nilimuona siku moja na walikuwa wamefanana si kawaida ila tabia sifahamu maana kilikuwa kioga sana siku hiyo.
 
Nyani Ngabu na Elnino,
Yaani nyie wote Ngosha mnapeana maneno yenu utafikiri nyie ni mtu na mtani wake? Si nyie wote chapa ya ng'ombe?
Wala MANUMBU utawafahamu tu, maneno mengi?
 
daaah maisha ya boarding school , weeh acha tu.nakumbuka mwaka 1983 natoka Dar naenda kujiunga sekondari moja huko Morogoro, aisee wacha tu.
 
Aah bwana eeh, mwataka kujipendelea nyie wa Moshi tu? Mie nakumbuka hapo Mazengo technical siku ya disko tulikuwa tunavaa nguo saa tatu asubuhi ambapo safari ya kuelekea kwa vimwana wa Msalato ni saa tisa. Uniform ilikuwa ni suruali nyeusi kwa shati nyupe na kwa siku hiyo ya disko hupuliziwa upupu(perfume) zaidi ya mara kumi. Nakumbuka second master wakati huo alikuwa akiitwa Msasa alijaribu kunishusha kwenye isuzu ya shule nisiende disco bila mafanikio japokuwa alikuwa mkali kama pili pili. Kwenye. J/tatu yake akanitoa mbele kwenye morning assembly na kuwatangazia wanafunzi wenzangu 'when i call this thing to get out of the school track he refused categorically, so now i send him home' nakumbuka alinigeukia akaniambia 'you have to run, run till to your parents house where you run no more'. Alieniokoa na suspicion ni Silvester Mkoba ambae ndie aliyekuwa heademaster wakati huo, kwa kunilamba mboko 4. Disco likiwa linaendelea mie nilijihusisha zaidi na ujasiria mali. Nilikuwa nauza Big G kwa kwenda mbele. Ole wao msalato wawaagize Bihawana sec kwenye disco lao, kufanya hivyo wangekuwa wametangaza vita na Mazengo. Kweli mleta tread umenikumbusha mbali sana. Na wakati huo maisha yalikuwa matamu mno.
Hahaaaa, Mkuu. Mazengo bweni gani? Mie nilikuwa pale Mwongozo, bweni karibu na choo ahhh, uwanja wa basketball.
Kumbe ulifaidi joto la Msasa. Mgogo yule alikuwa hawezi kumpiga mdogo wake Pro. Kabudi tu. Alikuwa akimuona anaongea naye kwa heshima kwelikweli na anaongea naye Kigogo tu.
Mkoba mara ya mwisho nilimuona Arusha. Walikuwa wamekuja kwenye mkutano gani sijui. Basi wanafunzi wa Mazengo tukamvamia. Jamaa alikuwa mwalimu mmoja safi sana. Nakumbuka kesi moja ambayo rafiki zangu walikamatwa na mali za shule wakitaka kwenda kuuza mjini. Kila mtu alifahamu kuwa wanafukuzwa shule. Kiliwaokoa kwamba kati yao, hakuna aliyewahi kushika nafasi chini ya sita darasani kwao. Ila zaidi naamini Mkoba alitumia busara zake. Walirudishwa nyumbani na wakarudi wiki mbili kabla ya mitihani kuanza. Wote walipata Div. 1. Mkoba alikuwa anatumia zaidi Busara kuliko sheria.

Kuna siku niliitwa kwake, nikamkuta bila shati na ugali wake mezani. Akaniuliza kama namfahamu mama mwenye jina la Janet Sikonge, nikasema naam ni dada yangu. Akaniambia amekuja na yuko kwa rafiki yake Area C, unafahamu ni wapi na ninakupa ruhusa uende ila uvae uniform (shati jeupe na suruali nyeusi) na urudi kabla ya saa 18. Nilienda na nikarudi sijui saa 21?? Siku hiyo ugali wa Chonya wala sikugusa. Sijui Sister alimpiga kashkash gani au ni busara zake kama kawaida. All in all, Mzee Mkoba alikuwa ni zaidi ya Mwalimu Mkuu. Alikuwa ni kama Baba yetu Mlezi.
Maneno yake milele ntayakumbuka ni ile sauti kubwa na kusema "You come here alone and you will go home alone...." Huyu mzee badi yupo hai??
Msasa yeye ni kuchongesha fimbo kwa ajili ya kupiga watu na maneno yake ni " Magesa Lukundija, see me in my Office after this dismisal......." Hapo ujuwe unaenda kukiona cha moto. Ila kuna kijana alikula Zabibu za Mwalimu Lubeleje (mgogo mwingine aliyeleta mradi wa shule ambao kila mwaka ulikuwa unaleta hasara ila kila mwana unaendelea kuwepi) basi alipigwa fimbo sita na kijana kamtolea macho makali Msasa. Hakushika makalio waka kutikisiza zaidi ya kumkodolea macho. Kiboko cha kwanza watu wakaanza kusikitika, cha pili wakazidsha sauti, cha tatu ikaanza miluzi na Msasa likafoka "who is doing pyoo pyoo there...", cha nne wakabaki form 4 peke yake basi Msasa likawageukia "form 4, acheni UNYAMA.........", watu hahaaaaaaaaa :) Huyu jamaa alikuwa SADIST.
Kuna siku tulikutana dry Cliner pale Dar, yeye na suti zake na mie za kwangu. Nilijikausha kama vile simfahamu. Ila kama sikosei wakati ule alikuwa HM Mtwara sijui shule gani.
 
Hahaaaa, Mkuu. Mazengo bweni gani? Mie nilikuwa pale Mwongozo, bweni karibu na choo ahhh, uwanja wa basketball.
Kumbe ulifaidi joto la Msasa. Mgogo yule alikuwa hawezi kumpiga mdogo wake Pro. Kabudi tu. Alikuwa akimuona anaongea naye kwa heshima kwelikweli na anaongea naye Kigogo tu.

aaah shemeji huyo kwenye red usingemtaja umenitonesha (alikuwa mkufunzi wangu)

afu kumbe nilichelewa kidogo tu we shem ningecheza 'disko' la welcome fomu wani na wewe.....
 
Crispin na Elnino, naona nyie kweli mwafahamiana. Nilikuwa na mpango wa siku moja kuja hapo Moshi Tech kwani kuna bwana mdogo wangu mmoja kutoka Sikonge na babu yake ndiye alikuwa mwalimu wangu wa kwanza shule ya msingi alikuwa akisoma miaka hiyo hapo Moshi Tech Sec. Alikuwa akiitwa Peter M. Nimepotezana naye siku nyingi sana. Pana wakati mdogo wake aliniambia yuko Iringa ila mdogo wake pia kapotea. Alikuwa kijana mfupi, mtanashati na anavaa miwani. Mara nyingi akija kututembelea pale Technical College Arusha. Kama kuna mtu ana mawasiliano na huyu kijana Peter Mal. basi anipitishie kwenye PM.

Kuna kijana mmoja sijui kama Ciprian alikuacha pale Moshi. Alikuwa akiitwa Cathbert Busumano (mhangaza). Nilikuja kupata habari amefariki. Ila baadaye mdogo wake atakuwa alisoma na nyie maana nilimuona siku moja na walikuwa wamefanana si kawaida ila tabia sifahamu maana kilikuwa kioga sana siku hiyo.
Jamaa alikuwa anaitwa Peter Malembeka -namfahamu sana wao walitangulia kumaliza shule wakatuacha sisi nyuma - duh sina contact naye. - Sikonge kweli umenirudisha mbali mno enzi za bondo na Top -Layer!
 
Halafu tulikuwa tunaanzia "spika kubwa" kupata boora la mbege ilituweze kutoa nishai!
Watoto wa-Kibosho Girls walikuwa "vyuma" bana!

Perfume ingeweza kuwa-shared kuanzia Azimio mpaka Karume!

Siku ya Graduu disco linapigwa "Kwadrengo"!
 
Naongelea maisha ya Boarding school hasa - O'level kati ya mwaka 1985 - 1995. Nitajikita zaidi Kilimanjaro hasa katika shule zifuatazo
Moshi Technical, Kibosho Girls, Weruweru, Masama Girls, Eliboru (Arusha), Umbwe Sec, Kiraeni Girls, Marangu Sec, Old Moshi, Kibohehe Sec, Kolila Sec

Sisi Mafundi wa Moshi Tech tuliambiwa mikono yetu imekomaa, watoto wa weruweru walipenda kucheza na eliboru secondary. Wakati huo madisko yalikuwa ya kishule shule bila kuvaa kisawasawa huwezi ibua mtoto kucheza naye mziki.

Nakumbuka mavazi ya wakati ule yalikuwa na kitanashati kweli kweli Mokasini shoes, Suruali ya mchelemchele na mkanda wake, Shati( Single color) ya mikono mirefu na neck tai au wengine walipiga Suluari za Jeans mawingu-mawingu mashati ya bahama bahama na Raba mtoni- mimi na marafiki zangu tulipenda kuvaa hivi - Nilipenda kupiga Punk glasses kujiweka swa -dakta.

Kama mzazi wako hana ma-peni ilikuwa shughuli- maana hutakuwa na upenyo wa kujihusisha kwenye social activies kama hizi maana kivazi kinakuwa tatizo kwako na kwenye kundi la machekibobu unakuwa humo sababu madisko yalikuwa yanatakiwa michango kwanza then mnakodi Bus linakuja kuwachukua na kuwarudisha.

Kwa wadada walikuwa wanapiga gauni smart ndefu na viatu mokasini za kike hasa rangi Nyeusi au nyeupe.

Kuna shule zilikuwa matawi ya juu kama Kibosho girls - wasichana wanakuja disko wote walikuwa na uwezo wa kupiga mokasini nyeusi gauni zilizoenda shule kisawa sawa, sasa kasheshe kuwaibua kucheza nao disko lazima uthamaminswe kutoka juu hadi chini - kama unalipa hapo ndiyo mtoto anaibuka anacheza na wewe. miziki ya slow (blues kama wengi wanapenda kuiita) ndo ilikuwa utata kupata mtoto wa kucheza naye.

Kulikuwa na wazamiaji wakuu hasa kutoka Kolila sec na Old moshi - hii mijemba ilikuwa inanusa disko hata likiwa wapi then inazamia - walinichekesha tu pale walipopitia maliwato ya kike kuzamia disko kule Kibosho ambalo moshi Tech tulikuwa tumealikwa. - disco likafungwa mlinzi alipigwa kwa sababu ya unoko wake.

Visting days bwana hazikukosa katika haya mashule, tulijitosa siku za weekend kutafuta watu wa kubadilishana nao mawazo wakati huo hakuna simu za kikononi (mobile phones)ilikuwa barua tena kupitia posta hadi mwenzako aipate ajibu then uconfirm visting day ilikuwa shughuli - Sisi wa Moshi Tech tulikuwa na mazoea kwenda Weruweru pale utawakuta watoto wamekaa kusuburi wageni - unafika mzee mkanda nje unajitambulisha kwa dada anayepokea wageni - mgeni anaitwa unalongaa then saa 12 kamili nje ya geti bye shuleni kwenu mwenda kuwatambia wenzako.

Ukiringanisha na sasa watoto wa o'level wanajichangaya sana kwenye madisko ya watu wazima - Sidhani kama wanapata fleva yetu - unajua mtoto wenzio ana nafasi yake. pale ilikuwa kitoto toto lakini hatukeshi.

Pamoja na hayo yote watu walifumua mitihani vilivyo, wakati huo kichwa chako ndiyo tuition - Naona ma Engineer kibao, wanahabari, Wahadhiri, Wanasheria wametoka shule hizi.
Aisee wewe tupo products za pale maengineer kibao umenikumbusha mbali mambo ya moshi tech na kwa sembeke pale, kusunday face weruweru, akina mzee makabila jikoni , Mpande na mchakamchaka, wakina Malisa, na mambo ya kiwese!!! aaaa bwanaeeh acha tu.............................. lakini wale wa Kibosho girls hivi nafirkiri walikuwa wanatuma picha kabisa before admission manake eish.... walikuwa warembo na zile uniform zao basitu.... zilituchengua!!!
 
Hivi hawa walimu bado wapo pale:

1. Munuo
2. Kasenge
3. Mpande
4. Malale (HeadMaster)
5. Lyimo
6. Kashimbili
7. Boxer
8. Koba
9. Mzee wa Electronics
10. Mutanda
11. Idaffa

Nawa-miss sana!

1. Mapease
2. Mikate
3. Uji wa Sukari
4. Special diet
5. Bisi
6. Vimbuzi
7. Top-layer

Navi-miss pia!
 
Hivi hawa walimu bado wapo pale:

1. Munuo
2. Kasenge
3. Mpande
4. Malale (HeadMaster)
5. Lyimo
6. Kashimbili
7. Boxer
8. Koba
9. Mzee wa Electronics
10. Mutanda
11. Idaffa

Nawa-miss sana!

1. Mapease
2. Mikate
3. Uji wa Sukari
4. Special diet
5. Bisi
6. Vimbuzi
7. Top-layer

Navi-miss pia!

hahahahaaaaaaa! Hivi mwalimu Mutanda na siasa zake alipotelea wapi jamani!!!! Mie nilikuwa kwenye timu ya mpira wakati fulani but eeh nikitegea starehe lakini mazoezi bwana ya kina Mpande na mwalimu mmoja nimemsahau alitoka ifunda anavaa miwani yalikuwa kiboko!!! Basi sie wakaaji wa Lumumba na azimio tulifaidi bisi usiku wa manane!!! pamoja na kuwa mbali huku huku bondeni mamabo yalikuwa supa enzi zile!!!
 
Aisee wewe tupo products za pale maengineer kibao umenikumbusha mbali mambo ya moshi tech na kwa sembeke pale, kusunday face weruweru, akina mzee makabila jikoni , Mpande na mchakamchaka, wakina Malisa, na mambo ya kiwese!!! aaaa bwanaeeh acha tu.............................. lakini wale wa Kibosho girls hivi nafirkiri walikuwa wanatuma picha kabisa before admission manake eish.... walikuwa warembo na zile uniform zao basitu.... zilituchengua!!!

Mwaka Juzi nilikuwa naenda Arusha nikapita pale moja kwa moja hadi bwenini kwangu - nikaingia pale Dom II Azimio house- kwenye engle ya kushoto ndo kitanda changu kilikuwapo, nikakuta dogo kalala nikamwamsha nikaongea naye kidogo nikatoka nikaangalia mazingira yanasikitisha. Nilivyotoka tu bwenini nikakutana na mwalimu wa zamu nikaongea na yeye nikaenda moja kwa moja Azimio Jikoni nikamkuta mzee makabila alifurahi sana nikamuungisha kidogo - imagine bado anapika bondo as of now.

Nikapandisha maeneo ya pale uwanjani kulikuwa na wanafunzi wanafanya evenning activities - Mpande alikuwepo kama kawaida yake akaitisha press confrence ya fasta nikaongea kidogo na madenti - jamaa anatiaje "mnaonaa somenii kila siku mnacheza mnawaona wenzenu kila mmoja akija ana drive...." madenti wakacheka nikaacha kidogo dogo nikasepa.

Nikatoka pale nikamtafuta mama Mwunuo - alinifundisha kingereza sikulipenda somo lake lakini alinifanya nipate B. nikampa zawadi yake na yeye ingawa alinikumbuka kwa shida sana. wote yeye na mumewe wameshastaafu

Ukweli mazingira ya shule yetu si mazuri - si kama tulivyoyaacha.
 
Mkuu ELNINO,

Nakushukuru kwa hii "flashback"!

Vipi, yule teacher wa Biology (Mrs Fute) bado yupo? Alinifanya nikafurahia sana somo la "Biology"!
 
Hivi hawa walimu bado wapo pale:

1. Munuo
2. Kasenge
3. Mpande
4. Malale (HeadMaster)
5. Lyimo
6. Kashimbili
7. Boxer
8. Koba
9. Mzee wa Electronics
10. Mutanda
11. Idaffa

Nawa-miss sana!

1. Mapease
2. Mikate
3. Uji wa Sukari
4. Special diet
5. Bisi
6. Vimbuzi
7. Top-layer

Navi-miss pia!

Malale alishastaafu kitambo mwanae nilisoma nae Primary,Munuo, Daffa walihama Boxer unamaanisha Malisa? Now ndio Headmaster KOBA-Mtaaalamu wa (Engineering Science) analewa hadi anashindwa kutembea then wanafunzi wanakuja kumbeba alikuwepo hadi 2007 sijui kama hadi leo yupo Hivyo vimbuzi/mapisi hadi leo vinatumika
 
hivi hawa walimu bado wapo pale:

1. Munuo - kastaafu
2. Kasenge - huyu sina taarifa naye kama anaishi
3. Mpande - yupo vile vile kijamaa hakizeeki
4. Malale (headmaster) - alifariki
5. Lyimo -
6. Kashimbili - duh mzee unanikumbusha bali sana
7. Boxer - mama alikuwa kweli amekaa kichanga si mchezo sina taarifa zake
8. Koba - jamaa alimpiga mtama ule mguu wake mbovu baada ya kumwekea unoko asiende disko kibosho girls
9. Mzee wa electronics - mzee nyanza - sidhani kama yuko hai -wakati tunaondoka alikuwa anaanzisha shule yake
10. Mutanda
11. Idaffa - mwalimu wa vijana by the time nilipoenda

nawa-miss sana!

1. Mapease - duh pale outgate kwa sambeke kwenda kunua mapease
2. Mikate - siku ya jummanne kama hujakimbia mchakamchaka basi lazima upate mkate kwa fimbo
3. Uji wa sukari - ulikuwepo saa 5 duh ulikuwa unalewesha ule lazima vipindi vya mchana upige mboji class
4. Special diet - utapenda uwe mgojwa upigwe diet kwa mwezi
5. Bisi - duh mzee unanikumbusha jangos laws 1. No material no paff ( yaani kama huna mahindi huonji na unafukuzwa) 2. The material that is present is proportional to the members only ( yaani mahindi, kuni na kila kilichopo ni kwa ajili ya members tu)
6. Vimbuzi - kuna jamaa vilimtajilisha - akatoka na four lakini hela kibao, siku moja alitaka kukamatwa na 2nd master akakimbia akachumbuka magoti yote tulikuwa tunamita comandoo
7. Top-layer - hii ilifeliisha ma mess mover wengi sana - wakila wanashiba hawaendi hata prep.

Navi-miss pia!
PHP:
[php]
[/php]

mzee soma maandishi kwenye blue.
 
MPANDE nahisi huenda akawa miongoni mwa Mwalimu maarufu hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom