Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,676
- 40,555
Tangu kuteuliwa kwake nilikataa kusema lolote juu ya Pinda na nakumbuka niliandika kuwa nampa benefit of the doubt ili aniconvince yeye si mmoja wao. Niliamini kwamba kila mtu ahukumiwe kwa vitendo vyake na maamuzi yake; niliamini kuwa kila mtu apewe nafasi ya kuonesha uongozi ili ijulikane anaongoza.
Ni kwa sababu hiyo tangu kuteuliwa kwa Pinda sijasema lolote dhidi yake, kauli zake, maamuzi yake n.k Nikimpa nafasi ya kufanya makosa mwanzoni na kujisahihisha kwani ndio anaanza. Miezi zaidi ya minne baadaye, uendelezo wa sera za kizugaji, na maamuzi ya kubabaisha unanilazimu nikiwa nadhamira safi kujikuta natumwa kuwapinga tena, na kuwapinga vikali.
Ni jukumu la raia kuikatalia serikali yake pake inapofanya jambo ambalo halina msingi, manufaa au uwazi kwa wananchi. Niliandika huko nyuma kuwa "lazima tuwakatalie" nikiamini kuwa msingi wa utawala wa demokrasia na unaofuata sheria umejengwa katika nguzo za wananchi kuihoji serikali yao na kutaka maelezo ya kuridhisha na serikali hiyo inaposhindwa kufanya hivyo basi inatakiwa kujiuzulu.
Kwa vile Waziri Mkuu Pinda ameamua kutokuwa mkweli kwa wananchi, na kwa makusudi kutoa taarifa za kupotosha umma, kulipigisha magoti Bunge, natoa ushauri wa bure asahihishe kauli yake Bungeni, na kutoa maelezo mara moja kuhusu kampuni ya Meremeta na ushiriki wa Jeshi letu kwenye biashara ya madini. Afafanue ni sheria gani, maamuzi gani, na kipengele gani cha Katiba yetu kimelipa JWTZ jukumu la kufanya biashara ya madini bila Bunge au wawakilishi wa wananchi kujulishwa. Zaidi ya yote, awaeleze wananchi ni kikao gani cha Baraza la Mawaziri ambacho kiliamuru kuanzishwa kwa kampuni ya Meremeta na kilibariki makampuni ya Mwananchi Gold, Deep Green, Tangold n.k ambayo yote kwa namna moja au nyingine yamehusishwa na uchotaji wa mabilioni ya fedha zetu toka benki kuu.
Kwa vile suala la usalama linahusu usalama wa Taifa letu na wanaoohoji ni wabunge wa Taifa hilo ambao ni wawakilishi wetu, basi hata kama suala la Meremeta haliwezi kuwekwa hadharani (kwa kurushwa kwenye Luninga) basi Bunge lifunge macho na masikio ya nje na Wabunge wote wawe briefed wazi na moja kwa moja kuhusu Meremeta, umiliki wake na uhusiano wake na JWTZ na usalama wa TAifa. Na endapo wabunge wataridhika basi tutapenda kusikia kuwa wameridhika na maelezo hayo na kama wabunge wapige kura kama wasimamizi wa serikali kuamua kama habari hizo kweli zinatishia usalama wa Taifa na kama wananchi wanapaswa kuziona.
Endapo wabunge wataona kuwa suala la Meremeta halitishii Usalama wa Taifa na hakuna jambo lolote ambalo linahatarisha usalama huo isipokuwa linaweza kuaibisha na kuumbua watu wachache basi habari hizo ziwekwe hadharani kwa kila mwananchi kuona.
Kama Bw. Pinda hayuko tayari kufanya hivyo, basi na yeye aamue kujiuzulu maramoja kwani ameamua kwa makusudi kabisa kuwaficha wananchi habari kuhusu Taifa lao na mojawapo ya chombo chao muhimu na kwa maneno yake mwenyewe ameamua kuwazuga Watanzania. Hili halikubaliki.
Tumedanganywa kiasi cha kutosha,
Tumezugwa kiasi cha kutosha,
Tumeburuzwa kiasi cha kutosha!
Na sasa tunadai haki yetu ya kuheshimiwa na kuthaminiwa kama raia!
Tunataka kutambuliwa kama ndiyo chanzo cha madaraka yote ya serikali.
Tunataka kuheshimiwa kama ndio waajiri halali wa serikali iliyoko madarakani na ya kuwa wao wanafanya kazi kwa niaba yetu na hakuna jambo lolote wanaloweza kufanya ambalo ni "siri yao" na sisi wananchi au wawakilishi wetu wasijulishwe.
Kama kuna kanuni ya Bunge ambayo inazuia kujadiliwa kwa masuala ya Usalama basi Bunge litengue kanuni hiyo kwani liko ndani ya uwezo wake. Hatukubali tena kuburuzwa kama mkokoteni uliovunjika, na hatuko tayari tena kubebwa mzoba mzomba kama lumbesa!
Kuweni wa kweli sasa kwani saa ya mjaribu inakuja na imefika, siku ya Jumatano ijayo kama nilivyofanya mwaka jana nitaongoza sala ya "baraka na laana" na Mungu aliye mbinguni mwenye kutawala nyakati na nyakati, mmiliki wa nyota na sayari na muumbaji wa muda, kina, umbali na mwendo! na Mfadhili wa uhai wote atasikia. Kwa yeye peke yake najisalimisha na uhai wangu uko mikononi mwake! Kwake yeye peke hofu yangu ipo na kwa mwanadamu awaye yote sitomhofia na simhofu yeyote mwenye kuudhuru mwili na asiiguse roho yangu! Jumatano, mbingu zitafunguka na sauti itasikika ya kwamba "mafisadi mmekwisha"! Mna siku tano kujisahihisha kuhusu uzugaji huu!
Kila jambo lina wakati wake, muda wao kutuzuga umepita na haurudi tena... huu ni muda wetu! Ni muda wetu kutaka serikali yenye uwazi, ni muda wetu kutaka serikali inayowajibika, na kwa hakika ni muda wetu kutaka viongozi wa kweli siyo wanafurahia kupigiwa saluti na kumulikwa na vimuli muli! Huu ni muda wa Watanzania, na watanzania hatimaye watashinda! Si kwa nguvu, si kwa jeshi, si umwagaji damu, si kwa ngumi.. bali kwa hoja zenye nguvu zibadilishazo fikira za wana na wana wa wana!
Huu ni wakati wetu, wa kwenu umefikia 11:59PM