Ok Pinda... here is the deal..

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Tangu kuteuliwa kwake nilikataa kusema lolote juu ya Pinda na nakumbuka niliandika kuwa nampa benefit of the doubt ili aniconvince yeye si mmoja wao. Niliamini kwamba kila mtu ahukumiwe kwa vitendo vyake na maamuzi yake; niliamini kuwa kila mtu apewe nafasi ya kuonesha uongozi ili ijulikane anaongoza.

Ni kwa sababu hiyo tangu kuteuliwa kwa Pinda sijasema lolote dhidi yake, kauli zake, maamuzi yake n.k Nikimpa nafasi ya kufanya makosa mwanzoni na kujisahihisha kwani ndio anaanza. Miezi zaidi ya minne baadaye, uendelezo wa sera za kizugaji, na maamuzi ya kubabaisha unanilazimu nikiwa nadhamira safi kujikuta natumwa kuwapinga tena, na kuwapinga vikali.

Ni jukumu la raia kuikatalia serikali yake pake inapofanya jambo ambalo halina msingi, manufaa au uwazi kwa wananchi. Niliandika huko nyuma kuwa "lazima tuwakatalie" nikiamini kuwa msingi wa utawala wa demokrasia na unaofuata sheria umejengwa katika nguzo za wananchi kuihoji serikali yao na kutaka maelezo ya kuridhisha na serikali hiyo inaposhindwa kufanya hivyo basi inatakiwa kujiuzulu.

Kwa vile Waziri Mkuu Pinda ameamua kutokuwa mkweli kwa wananchi, na kwa makusudi kutoa taarifa za kupotosha umma, kulipigisha magoti Bunge, natoa ushauri wa bure asahihishe kauli yake Bungeni, na kutoa maelezo mara moja kuhusu kampuni ya Meremeta na ushiriki wa Jeshi letu kwenye biashara ya madini. Afafanue ni sheria gani, maamuzi gani, na kipengele gani cha Katiba yetu kimelipa JWTZ jukumu la kufanya biashara ya madini bila Bunge au wawakilishi wa wananchi kujulishwa. Zaidi ya yote, awaeleze wananchi ni kikao gani cha Baraza la Mawaziri ambacho kiliamuru kuanzishwa kwa kampuni ya Meremeta na kilibariki makampuni ya Mwananchi Gold, Deep Green, Tangold n.k ambayo yote kwa namna moja au nyingine yamehusishwa na uchotaji wa mabilioni ya fedha zetu toka benki kuu.

Kwa vile suala la usalama linahusu usalama wa Taifa letu na wanaoohoji ni wabunge wa Taifa hilo ambao ni wawakilishi wetu, basi hata kama suala la Meremeta haliwezi kuwekwa hadharani (kwa kurushwa kwenye Luninga) basi Bunge lifunge macho na masikio ya nje na Wabunge wote wawe briefed wazi na moja kwa moja kuhusu Meremeta, umiliki wake na uhusiano wake na JWTZ na usalama wa TAifa. Na endapo wabunge wataridhika basi tutapenda kusikia kuwa wameridhika na maelezo hayo na kama wabunge wapige kura kama wasimamizi wa serikali kuamua kama habari hizo kweli zinatishia usalama wa Taifa na kama wananchi wanapaswa kuziona.

Endapo wabunge wataona kuwa suala la Meremeta halitishii Usalama wa Taifa na hakuna jambo lolote ambalo linahatarisha usalama huo isipokuwa linaweza kuaibisha na kuumbua watu wachache basi habari hizo ziwekwe hadharani kwa kila mwananchi kuona.

Kama Bw. Pinda hayuko tayari kufanya hivyo, basi na yeye aamue kujiuzulu maramoja kwani ameamua kwa makusudi kabisa kuwaficha wananchi habari kuhusu Taifa lao na mojawapo ya chombo chao muhimu na kwa maneno yake mwenyewe ameamua kuwazuga Watanzania. Hili halikubaliki.

Tumedanganywa kiasi cha kutosha,
Tumezugwa kiasi cha kutosha,
Tumeburuzwa kiasi cha kutosha!

Na sasa tunadai haki yetu ya kuheshimiwa na kuthaminiwa kama raia!

Tunataka kutambuliwa kama ndiyo chanzo cha madaraka yote ya serikali.

Tunataka kuheshimiwa kama ndio waajiri halali wa serikali iliyoko madarakani na ya kuwa wao wanafanya kazi kwa niaba yetu na hakuna jambo lolote wanaloweza kufanya ambalo ni "siri yao" na sisi wananchi au wawakilishi wetu wasijulishwe.

Kama kuna kanuni ya Bunge ambayo inazuia kujadiliwa kwa masuala ya Usalama basi Bunge litengue kanuni hiyo kwani liko ndani ya uwezo wake. Hatukubali tena kuburuzwa kama mkokoteni uliovunjika, na hatuko tayari tena kubebwa mzoba mzomba kama lumbesa!

Kuweni wa kweli sasa kwani saa ya mjaribu inakuja na imefika, siku ya Jumatano ijayo kama nilivyofanya mwaka jana nitaongoza sala ya "baraka na laana" na Mungu aliye mbinguni mwenye kutawala nyakati na nyakati, mmiliki wa nyota na sayari na muumbaji wa muda, kina, umbali na mwendo! na Mfadhili wa uhai wote atasikia. Kwa yeye peke yake najisalimisha na uhai wangu uko mikononi mwake! Kwake yeye peke hofu yangu ipo na kwa mwanadamu awaye yote sitomhofia na simhofu yeyote mwenye kuudhuru mwili na asiiguse roho yangu! Jumatano, mbingu zitafunguka na sauti itasikika ya kwamba "mafisadi mmekwisha"! Mna siku tano kujisahihisha kuhusu uzugaji huu!

Kila jambo lina wakati wake, muda wao kutuzuga umepita na haurudi tena... huu ni muda wetu! Ni muda wetu kutaka serikali yenye uwazi, ni muda wetu kutaka serikali inayowajibika, na kwa hakika ni muda wetu kutaka viongozi wa kweli siyo wanafurahia kupigiwa saluti na kumulikwa na vimuli muli! Huu ni muda wa Watanzania, na watanzania hatimaye watashinda! Si kwa nguvu, si kwa jeshi, si umwagaji damu, si kwa ngumi.. bali kwa hoja zenye nguvu zibadilishazo fikira za wana na wana wa wana!

Huu ni wakati wetu, wa kwenu umefikia 11:59PM
 
... Na Yeye Aamue Kujiuzulu Maramoja Kwani Ameamua Kwa Makusudi Kabisa Kuwaficha Wananchi Habari Kuhusu Taifa Lao Na Mojawapo Ya Chombo Chao Muhimu Na Kwa Maneno Yake Mwenyewe Ameamua Kuwazuga Watanzania. hili Halikubaliki.

Pinda Masti Go!
 
Mzee Mwanakijiji nitakuwa na wewe katika sala hii ya kuwapa laana,
Mungu naomba uwe upande wetu ili hawa mafisadi wahukumiwe hapa hapa duniani
Eeh Mungu,angalia Pinda anvyopindisha mambo na kutufanya siye wapuuzi na wajinga
Eeh baba sikia maombi yetu na naomba uyajibu kwa siku hizi mbili tu.

Na kwa kuwa wameamua kutufanya wapuuzi na mazezeta tusiyo na msikio na akili
Na kwa kuwa wanatamani watukamate ili watuue kabisa na kutoa macho
Na kwa kuwa Nasimamia katika haki na sina namba 666 kwenye paji la suo wangu
Nina Imani ya kuwa Pesa za Meremeta Zitarudishwa na tutashinda.

Enyi vingozi mlio na roho ya udanganyifu na waongo wa kutupwa msio na aibu,
Nawaandikieni nikiwaomba tutumie siku hizi mbili kwa ajili ya haya tu yafuatyo
Kwanza Muachie Ngazi kwa kosa la kupitisha Bajeti ya kutuning'iniza siye makini
Pili Naomba mjiunge nasi na kuanza kudai haki yetu kama Wanajamii makini

Najua wanaona Tunawakera,ila Naamini nyie mtakekerekaa zaidi wakati si mwingi
Ninajua wiki inaio kuja itakuwa ni wiki mbaya sana kwenu na familia zenu zakifisadi
Nimepata Ujumbe wenu na niko tayari tena na nasisitiza niko tayari kwa lolote
Ila La msingi mjue Siko tayari kukubali kumezeshwa matapishi kwa kuogopa kufa.

Najua Mnasifika kwa uchawi na mambo mabaya,ila Mungu ninaye muamini hawapendi
Mmejipalia makaa,Mmelewa Mvinyo wa madaraka,Mmekuwa wahuni,mmekuwa wa ovyo
siwapendi kamwe,na sitawapenda milele kwa kuwa nyie si wana wa Mungu
Hatma ya Tanzania kwa uongozi huu,nawaonea huruma wajukuu zangu huko mbeleni

kwi kwi kwi kwi

Do we really Need Pinda?
 
Last edited:
I will repeat what I posted in one of the threads about Kikwete and some members were not happy with it.
He is a damn freak and coward.
He is a loser and just like all other corrupt people surrounding him.He is no better than any of them.
 
Pinda Masti Go!

kuna wakati ambapo mistari tuliyoichora isikubali kuvukwa. Si na Kikwete, si na Pinda wala si na mtu yeyote yule. Kuheshimu wananchi unaowatawala ni mstari ambao hauvukwi na mtu yeyote yule. Kitendo cha Pinda na serikali kutuzungusha kuhusu Meremeta ni dharau ya hali ya juu kwa taifa letu, na hili hatuwezi kuwakubalia.
 
We need a new government with a new Mandate.. turudi kwa wapiga kura. Let me look at the constitution...
 
Kikwete Yeye Hana Muda Na Tanzania, Keshokutwa Anaondoka Kwenda Zake Japan, Taarifa Za Ndani Zinasema Atapitia Na Dubai Kufanya Shopping Kidogo.
 
huyu Pinda anakilinda CCM kwani hapa ni kuwatesa watanzania kila kukicha.

Inatia uchungu na hasira sana sana kuwasikiliza wengine wakizungumzia mambo ya kiajabu ajabu........

Pinda must be delt with accordinglly......
 
ummh Mkuu mwanakijiji ulituambia wiki ijayo, au ndo imekuja mapema, maana kama ni mstari wameshavuka tayari. uwiiiii! nchi yetu jamani..
 
Tena ni afadhali umemwahi mapema mapema hawa wanataka kuliangamiza TAIFA kwa maslahi yao BINAFSI!
 
We need a new government with a new Mandate.. turudi kwa wapiga kura. Let me look at the constitution...

Nakubaliana na wewe kabsaa. The issue is how do we get rid of JK? It is my belief that we dont have a strong party to win against him, how do we do it then?
 
Nataka alinde masilahi ya nchi tuu.
Ila ibara ya 13 ya CCM...inasemaje?Hapo ndipo pagumu panapowashinda wengi..Mgombea Binafsi ndiyo jibu.
Ibara hiyoo ndiyo ulikuwa mstari mkuu wa Kikao kilichopita cha NEC pale DODOMA,wanachama walionekana wamekuwa siyo wa kiCCM hivyo iabidi atafutwe muhubiri mahili na wa siku nyingi,akatafutwa Mkapa na Mkalimani wake akawa Lowassa ,

wakanena maneno ya kusifiana na kujazana miioyo yao na leo hii penda anashuhudia yaliyomtokea,wako wengi wameshashuhudia hayo.

Ila kizuri watanzania ni wenye akili na wanajua ni jambo lipi la kuchukua na lipi la kuacha.Hii dini walioamua kuanzisha miye naona kama ni kama ya kishetani hivi..
 
Hii Nchi Si Ya Jeshi...Ni ya utawala wa kisheria zenye kutulinda sisi wadau wa nchi...ila Inaonekana Wataamua Kuikabidhi Kwa Jeshi Kama Wapinzani Wataelekea Kushinda.
Tatizo Ni Jeshi Lenyewe Lishagawanyika Kimtizamo Kwani Si Wote Wenye Hisa Na Mafisadi Kama Hao Wa Meremeta.
 
Pinda is nothing but a big joke ambaye hata wenzake kina Mkapa,JK,Lowassa they dont even respect him nina uhakika kina Rostam na Mgonja wana nguvu kuliko this lazy a$$....huyu mtu anafanya office ya katibu kata ionekane ina nguvu kuliko ya Waziri mkuu....tuandike maumivu tuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom