OilCom inahusika kuchakachua mafuta?

Shukrani sana kwa follwback Dadake. Hii process ya kuchakachua mafuta nadhani inaanzia kwa kampuni mama na siyo mfanyabiashara anayemiliki Filling Station. Kama ni kweli basi kuna kila sababu ya kushtukia Filling Station za wala ngamia. Bora BP, Engen, Oryx, Total etc ambazo kampuni mama ni za Kizungu/South African.
 
Maeneo yanaotumika kuchakachua mafuta yapo na yanajulikana ila EWURA wana kamradi ndani yake.Si vizuri kulaumu wala ngamia bila kuangalia uzembe wa EWURA.
Kwa taarifa ni kwamba hata makampuni ya Kizungu nayo hayako nyuma katika suala hili.Kinachotakiwa ni EWURA kufanya kazi yao au ushuru uongezwe kwenye mafuta ya taa.
 
Inasikitisha sana kuona serikali na EWURA yake hawako tayari kulishughulkia tatizo hili. Tatizo kama hili liliwahi kunipata muda si mrefu na ni wakati mjadala wa wabunge ukiendelea kuhusu uchakachuaji wa mafuta. Ilikuwa ni usiku na nilivyotafuta na kufuatilia sana mwenye kituo cha mafuta alionyesha wazi kuwa kuna kampuni mama inahusika na uchakachuaji huo. Offcourse alinilipa gharama za uharibifu. Wananchi wanaogopa kuingia kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwa sababu biashara ya mafuta inaonekana ina wenyewe ambao wanawalinda.

Wakati wa matatizo hayo nilijaribu kuwatafuta Ewura kama wana Hotline, Lakini ni wakala wa serikali ambaye hawezi kupatikana kirahisi mpaka iwe saa za kazi. Kuripoti swala hilo polisi kwa mwendo tunaokwenda ni kupoteza wakati kwa upelelezi usioisha, ushahidi hautapatikana. Kumbuka kuchukua risiti kila unapojaza mafuta kwenye gari yako.
 
Wachakachuaji wa hayo mafuta ni wamiliki wa vituo ili wapate profit kubwa, si madereva wala nani, mabosi wa vituo wanajua wese gani zuri na lipi baya, seal inayotumika kufunga matank ya malori si kitu kwani ni mpano wao.Tanzania zaidi ya uijuavyo bwana.:sick:
 
Hii habari inahitaji umuhimu zaidi kuliko ambayo imeipata hadi hivi sasa. Dadake asante.. kwa habari hii..
 
Dadake huu ufafanuzi wako na ufuatiliaji unahitaji pongezi!
Binafsi nakupa pongezi za dhati!

Tungekuwa na waandishi wa habari wa kutosha wa namna hii ambao hawaziki (Hawaui) story za msingi kama hizi kwa kufuatilia hatua kwa hatua, Naamini tungekuwa tumesonga mbele hata hatua moja toka hapa tulipo! Ila waandishi wetu wengi wakisharipoti habari, ndo inakuwa imefika mwisho.

Hongera sana kwa mara nyingine tena!

Oilcom nadhani ni mtandao mkubwa kuliko tunavyodhani, sijui kama JK ataweza kuwagusa. I believe he is too weak for them! Kwanza sasa hiv anafikiria uchaguzi, sidhani hili kama lipo kwenye ajenda zake. maana kama gari yake mwenyewe ili wekewa mafuta machafu na hajasema kitu, unategemea anaweza kutufanyia sisi kitu? Sidhani!
 
Wana JF nashukuru kwa kunipongeza kwa kazi ninayofanya, inanipa faraja kwa baadhi kuniongoza pa kuelekea katika suala hili. mmoja wetu alitamani kujua zaidi kuhusu Oil com ingawa maelezo yake yanaashiria kuwa anataarifa zake kwa kiasi fualani. alihoji kuhusu tetesi zilizokuwepo kwamba kampuni hiyo iliomba tenda ya kusafirisha mafuta ya ndege.
Hiyo ni kweli na kwa taarifa nilizopata ni kwamba kampuni hiyo ilipata tenda hiyo na hata leo gari moja la kampuni hiyo limeondoka jijini Dar es Salaam kupeleka mafuta hayo ya ndege.

Mmoja wa madereva wa kampuni hiyo ambaye ameiburuza kampuni hiyo kwa kumpunja malipo yake ya mshahara kwa miaka miaka tisa na kutomlipia michango NSSF ambaye amejulikana kwa jina moja la George, kumbukumbu zinaonyesha kuwa amewahi kusafirisha nishati hiyo mikoa mbalimbali nchini.
Kwa ufupi kampuni hiyo ni mali za urithi wa familia ya kiarabu. mzee aliyerithi mali hiyo anaishi jijini Dar es Salaam Kariakoo, anao watoto wake wa kiume wanne, mmoja anasimamia Oil Com Tanzania, mwingine Kenya na mwingine Malawi. Mmoja hana idara maalumu kutokana na kuwa mtumiaji zaidi ya uwajibikaji. kama tujuavyo mtu wa aina hiyo katika familia hakosekani. Nawafahamu wote kwa majina.
Namuunga mkono Kabwege kwamba huu ni mtandao mkubwa ambao ili JK aukabili ni lazima abwage manyanga ya kuthamini uswahiba.
kumbukumbu zinaonyesha pia kuwa "wakubwa" wengi wanakunywa mafuta kwenye vituo vya kunywea mafuta vinavyomilikiwa na kampuni hii-siyo mafuta ya kwenye magari tu bali hata ya mifukoni. Hata hivyo hilo halitatuzuia kuanika tunayofanikiwa kuyafahamu kwa sababu hata tone la maji likidondokea mwamba kwa miaka mingi hatimaye ufa hutokea na mwishowe mwamba kuvunjia. ipo siku atatokea mwenye kuthubutu, atakamilisha ndoto za watanzania kuwa huru.
 
......uuuuwiiii.......
 
Asante sana Dadake.
Hee, sasa sijui tushitaki wapi? Maana hata EWURA naona ni joka la kibisa tu.

Halina hata jino moja!!! Kuna kitu tu........
 
Hakiyanani, wenye magari tunapata shida kweli. Wiki ilopita nililinunua mafuta ya Petroli pale Bomang'ombe Hai Oryx. Kufika Arusha gari inamisi na kupoteza nfguvu kabisa. Nikatafuta Ofisi za EWURA huku Arusha bila mafanikio! Ilibidi niingie gharama ya kushusha tanki na kulisafisha.

Hapa Arusha vituo vya Mount Meru viko vingi na nadhani vyote vina tabia hiyo. Nimeamua kuachana na mafuta ya Mount Meru na sasa natumia Total na Gapco. Orxy na BP huku Arusha hata vyenyewe vimewahi kupatwa na kashfa ya uchanganyaji mafuta, ni taabu tupu.

Nahisi EWURA , Wizara ya Nishati na Madini navyo VIMECHAKACHULIWA!
 
Kuchakachua mafuta .....ndio kuyafanyeje?.............naomba kuelimishwa hiyo sayansi...........
 
Naona kitufe che "senksi" hakitoshi kutoa pongezi zangu kwa Dadake kufuatilia hii issue. HONGERA SANA. Ni mfani mzuru kwa kuigwa. Ogah, kama hujui kuchakachua mafuta ni nini, basi unaishi ughaibuni na una gari, au unaishi bongo lakini hauna gari (just joking!!):smiling:
 
Wana JF nashukuru kwa kunipongeza kwa kazi ninayofanya, inanipa faraja kwa baadhi kuniongoza pa kuelekea katika suala hili. mmoja wetu alitamani kujua zaidi kuhusu Oil com ingawa maelezo yake yanaashiria kuwa anataarifa zake kwa kiasi fualani. alihoji kuhusu tetesi zilizokuwepo kwamba kampuni hiyo iliomba tenda ya kusafirisha mafuta ya ndege.
Hiyo ni kweli na kwa taarifa nilizopata ni kwamba kampuni hiyo ilipata tenda hiyo na hata leo gari moja la kampuni hiyo limeondoka jijini Dar es Salaam kupeleka mafuta hayo ya ndege.

Mmoja wa madereva wa kampuni hiyo ambaye ameiburuza kampuni hiyo kwa kumpunja malipo yake ya mshahara kwa miaka miaka tisa na kutomlipia michango NSSF ambaye amejulikana kwa jina moja la George, kumbukumbu zinaonyesha kuwa amewahi kusafirisha nishati hiyo mikoa mbalimbali nchini.
Kwa ufupi kampuni hiyo ni mali za urithi wa familia ya kiarabu. mzee aliyerithi mali hiyo anaishi jijini Dar es Salaam Kariakoo, anao watoto wake wa kiume wanne, mmoja anasimamia Oil Com Tanzania, mwingine Kenya na mwingine Malawi. Mmoja hana idara maalumu kutokana na kuwa mtumiaji zaidi ya uwajibikaji. kama tujuavyo mtu wa aina hiyo katika familia hakosekani. Nawafahamu wote kwa majina.
Namuunga mkono Kabwege kwamba huu ni mtandao mkubwa ambao ili JK aukabili ni lazima abwage manyanga ya kuthamini uswahiba.
kumbukumbu zinaonyesha pia kuwa "wakubwa" wengi wanakunywa mafuta kwenye vituo vya kunywea mafuta vinavyomilikiwa na kampuni hii-siyo mafuta ya kwenye magari tu bali hata ya mifukoni. Hata hivyo hilo halitatuzuia kuanika tunayofanikiwa kuyafahamu kwa sababu hata tone la maji likidondokea mwamba kwa miaka mingi hatimaye ufa hutokea na mwishowe mwamba kuvunjia. ipo siku atatokea mwenye kuthubutu, atakamilisha ndoto za watanzania kuwa huru.

Asante mkuu kwa kutuhabarisha....
Du mi mpaka natishika,kumbe nchi hii inaubovu kila mahali...Tutaponea wapi?Nini hatima ya nchi hii km si kuelekea kule tulikotoka...yaani katika ukoloni,tena wa kutawaliwa na ndugu zetu.Tunahitaji ukombozi kwa kufanya tafikti km hizi,na kuzifanyia kazi...
 
Asante sana Dadake.
Hee, sasa sijui tushitaki wapi? Maana hata EWURA naona ni joka la kibisa tu.

Halina hata jino moja!!! Kuna kitu tu........

Ukweli ni kwambaaa akina Makamba na CCM yao ndio inawafuga watu hawa kwani kutwa hawaishi kwenda kuomba fedha za kuimarisha chama kwa matajiri hawa kumbe wanatayarisha pesa za watoto wao kugombea ubunge, kununulia mgari ya kifahari, kumalizia vibanda vyao kule Bumbuli kaya...etc, ukifuatilia kwa ukaribu sana utagundua kuwa kila tajiri wa biashara ya mafuta yupo na mlinzi wake serikalini hana wasiwasi sie twaishhia piga doomoo tu
 
huo ndio ukweli halafu adhabu utasikia eti ukikamatwa faini milioni 100. wakati hizo kwao ni cha mtoto. ingekuwa wanawekea adhabu anglau kama hizi labda wangeshika adabu
1. kosa liwe la kuhujumu uchumi wa nchi.
2. kifungo cha maisha jela au miaka isiyopungu sitini na hiyo faini ya m.100
3. kupingwa ban permanent na kunyang'anywa lesseni
3. kama ni raia wa kujiandikisha kunyang'anywa uraia na kufukuzwa nchini baada ya kutumikia kifungo chake kama sio cha misha
4. kama ni mwekezaji kufungiwa na kufukuzwa nchini. labda ingesaidia.
 
Wana JF nashukuru kwa kunipongeza kwa kazi ninayofanya, inanipa faraja kwa baadhi kuniongoza pa kuelekea katika suala hili. mmoja wetu alitamani kujua zaidi kuhusu Oil com ingawa maelezo yake yanaashiria kuwa anataarifa zake kwa kiasi fualani. alihoji kuhusu tetesi zilizokuwepo kwamba kampuni hiyo iliomba tenda ya kusafirisha mafuta ya ndege.
Hiyo ni kweli na kwa taarifa nilizopata ni kwamba kampuni hiyo ilipata tenda hiyo na hata leo gari moja la kampuni hiyo limeondoka jijini Dar es Salaam kupeleka mafuta hayo ya ndege.

Mmoja wa madereva wa kampuni hiyo ambaye ameiburuza kampuni hiyo kwa kumpunja malipo yake ya mshahara kwa miaka miaka tisa na kutomlipia michango NSSF ambaye amejulikana kwa jina moja la George, kumbukumbu zinaonyesha kuwa amewahi kusafirisha nishati hiyo mikoa mbalimbali nchini.
Kwa ufupi kampuni hiyo ni mali za urithi wa familia ya kiarabu. mzee aliyerithi mali hiyo anaishi jijini Dar es Salaam Kariakoo, anao watoto wake wa kiume wanne, mmoja anasimamia Oil Com Tanzania, mwingine Kenya na mwingine Malawi. Mmoja hana idara maalumu kutokana na kuwa mtumiaji zaidi ya uwajibikaji. kama tujuavyo mtu wa aina hiyo katika familia hakosekani. Nawafahamu wote kwa majina.
Namuunga mkono Kabwege kwamba huu ni mtandao mkubwa ambao ili JK aukabili ni lazima abwage manyanga ya kuthamini uswahiba.
kumbukumbu zinaonyesha pia kuwa "wakubwa" wengi wanakunywa mafuta kwenye vituo vya kunywea mafuta vinavyomilikiwa na kampuni hii-siyo mafuta ya kwenye magari tu bali hata ya mifukoni. Hata hivyo hilo halitatuzuia kuanika tunayofanikiwa kuyafahamu kwa sababu hata tone la maji likidondokea mwamba kwa miaka mingi hatimaye ufa hutokea na mwishowe mwamba kuvunjia. ipo siku atatokea mwenye kuthubutu, atakamilisha ndoto za watanzania kuwa huru.

Thanks Dadake kwa habari hii,

Nafikiri vyombo vyetu vy usalama vimeshindwa kazi au vinagawio katika uovu unaotendeka katika mambo mengi ikiwemo ujambazi, kuchakachua mafuta na kukata mapanga ma-albino.

Ujumbe kwa vyombo vinavyohusika na usalama wa nchi, rai na mali zo nikwamba wananchi hawajasindwa kujitafutia suluhu juu ya hilo, ni muda muda tu! Ukitimu mtaona suluhu yake na mtajutia gawio mnalolipata toka kwa watenda maovu hayo. Si mmeona vibaka wanavyochomwa moto. Ni sehemu tu ya suluhu baada ya kuona tafsiri ya usalama wa taifa kwenu ni kulindsa viongozi na nyaraka za posho za safari mnazoenda kila uchao.

Hivi vyombo vya dola hamuoni aibu kama mpaka magari ya rais yanapata mchakachuo huo wa mafuta? eeee tata wane mwe titantambuaje mtu anaechakachua mafuta,eeeee tata wane mwe titantambuaje, titantambuaje mtu anaelijali taifa hili?
 
wandugu,hili tatizo la uchakachuaji wa mafuta ni zaidi ya tunavyolifikilia,mimi nafanya kazi katika moja ya makampuni ya mafuta kurasini,hakua depot hata moja inayochanganya mafuta,anayechanganya mafuta ni dereve...matajiri wote wenye vituo vya mafuta wanategema uchanganyaji wa mafuta kupata faida kwahiyo hakuna tajiri atayenunua mafuta ukishayachangaya depot maana yeye akinunua hata pata faida..na hakuna kituo cha mafuta hata kioja hapa tanzania ambacho hawachanganyi mafuta sema wanatofautiana kiwango cha uchangayaji.tatizo la hayamafuta ya density range kwamfano diesel inaanzia 0.8-0.85 kwaiyo wachanganayji wanachenza na hiyo range tu..kenya wenzetu mafuta yote yanatozwa ushuru sawa kwahiyo hakuna uchanganyaji,hapa tanzania kuna matajiri wanaishi kwa uchakachuaji tu kwahiyo hata ukisema umwambie raisi au waziri apandishe ushuru wa mafuta ya taa hataweza maana hawa matajiri wanatoa mshiko si mchezo,hii point ya kwamba eti tunawajali maskini ndio maana hawapandihsi mafuta ya taa si kweli,pandisha bei mafuta ya taa punguza bei ya gas,zahai za kutosha barabara nzuri huko ndokumjali maskini tena itasaidia watu wasikate miti hovyo..
 
Back
Top Bottom