OilCom inahusika kuchakachua mafuta? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

OilCom inahusika kuchakachua mafuta?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Dadake, Jul 1, 2010.

 1. D

  Dadake Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Serikali na mamlaka zake inadai inaendelea kupambana na vitendo vya kuchakachua mafuta ya dizeli na petroli, lakini ufuatiliaji niliofanya unaashiria kuwa baadhi ya watendaji ndani ya serikali na mamlaka zinazotarajiwa kudhibiti vitendo hivyo wanafahamu wanaofanya uovu huo na pengine kuwasaidia kwa namna mbalimbali.

  Kampuni ya kusafirisha na kuuza aina mbalimbali za mafuta, yaani dizeli, petroli, mafuta ya taa na mafuta ya ndege, Oil Com inasadikiwa kufanya uchakachuaji mafuta kabla haijayaingiza sokoni.

  Mei 20, mwaka huu gari la kampuni hiyo Scania Na.T517AJM lenye tela Na. 687ACP lililoendeshwa na S. A. Mkude lilipakiwa lita 35,000 za dizeli katika depot ya kampuni hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam.

  Gari hilo likaegeshwa ndani ya Yadi ya kampuni hiyo iliyopo Tabata Relini. Safari ya kupeleka mafuta hayo Ushirombo wilayani Bukombe ilianza Mei 21 mwaka huu, siku ya Ijumaa ambapo yalitakiwa kuwasilishwa kwa Kampuni inayojenga barabara ya Ushirombo mpaka Lunzewe, ambayo imeingia mkataba wa kuuziwa mafuta na Oil Com.

  Afisa wa kampuni ya ujenzi, Gasper Msuya, alipelekewa mafuta na nyaraka zinazohusika na mzigo huo na Mkude Jumatatu asubuhi. Baada ya kuchukua sampuli ya mafuta kutoka ndani ya gari hilo na kuondoka nayo, alirejea mchana na kumueleza Mkude kuwa hawezi kupokea mafuta hayo, yamechakachuliwa.

  Dereva na gari vikatakiwa kupelekwa polisi Ushirombo. Dereva akaomba polisi ishirikiane na EWURA wachukue sampuli ya mafuta hayo ikafananishwe na yaliyo kwenye matanki ya mafuta yanayomilikiwa na Oil Com yaliyopo Kurasini Dar es Salaam ambapo mafuta hayo yalichukuliwa kwa maelezo kuwa, wakati yakipakiwa hata yeye aliingiwa na shaka kutokana na wepesi wake.

  Tofauti na matarajio, wakati dereva huyo akiwa rumande, ofisi ya Oil Com Kahama iliagiza dereva akachukua gari hilo siku hiyo hiyo ya Jumatatu. Inasadikiwa ilipelekwa Kahama. Dereva alishikiliwa na polisi tokea Jumatatu hadi Ijumaa ambapo aliambiwa ajidhamini kwa leseni yake, akae eneo hilo la Ushirombo kwa siku chache, waliomshitaki wasipofika ili apelekwe mahakamani angeachiwa huru arudi Dar. Hakupelekwa mahakamani kwani walompeleka waliingia mitini.

  Ufuatiliaji ukafanikisha kupatikana namba ya simu ya kiganjani ya afande aliyeshughulikia sakata hilo na jina lake kwa sasa linahifadhiwa, akaitwa na kuhojiwa:

  Swali: Tunazo taarifa kwamba mmekamata mafuta yaliyochakachuliwa na dereva anayetuhumiwa kufanya kosa hilo, suala hilo limefikia wapi?

  Jibu: Ni kweli suala hilo lilitokea, lakini siwezi kulizungumzia kwa kina, waulize wakubwa

  Swali:
  Wakubwa wakina nani? Si ulilishughulikia wewe?

  Jibu: Nakushauri umuulize mkuu wa upelelezi.

  Ufuatiliaji ukafanikiwa kupata namba ya mkuu wa upelelezi wa wilaya ya Bukombe, Leonard Paul, alipoulizwa baada ya kuelezwa sakata lote lilivyokuwa tokea gari lilivyopakia mzigo hadi lilivyofika mikononi mwa polisi Ushirombo alisema hivi:

  "Kwakweli sina taarifa za uhakika za kukueleza kuhusu suala hilo. Kwanza tokea Mei 20 mpaka Mei 30 mwaka huu, sikuwepo wilayani nilikuwa mafunzoni mjini Morogoro. Hata sasa tunavyozungumza nipo vijijini kikazi, nikirudi wilayani nitafuatilia na kutoa ufafanuzi."

  Kwa mwendo huu, mchezo huu mchafu utakwisha? Kwa vyovyote hizo lita 35,000 zilisambazwa sokoni baada ya kushtukiwa na kampuni ya ujenzi na kutolewa nje, yalipelekwa wapi? Hilo ni swali linalohitaji kufanyiwa kazi...
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 235
  Trophy Points: 160
  Mh, inafikirisha!
   
 3. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Haki katika taifa letu, safari bado ni ndefu. Rushwa hupofusha macho ya wenye madaraka wanapokubali kuikumbatia.
   
 4. K

  Katabazi JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 18, 2007
  Messages: 355
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Haya mambo nadhani kama JK hataki kufuta ushuru wa mafuta ya taa ambayo sasa vijini yanalanguliwa kwa bei kubwa hata kuliko yangekuwa na ushuru basi panahitajika utaalamu wa kina, wapo madereva ambao kweli wamenemeeka na sakata hili, lakini kama amepewa mafuta ambayo tayari jamaa wameishayashughulikia-yeye ana vipimo gani vya kugundua?

  Sijajua kwanini JK hataki kutoka ushuru wa mafuta ya taa? Angalau akaokoa hasara ya vifaa vyetu,hasara ya bandari na kampuni zinasomba mafuta kwa ukweli na heshima ya nchi kwa majirani.

  Iko kazi!:sick:
   
 5. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2010
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  nenda bp mafuta yao safi, BP wamewanyang'a vituo kibao franchise yao kwa ajili ya kuchanganya mafuta
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Utaanza kugusa maslahi ya watu. Kama mngelijua jinsi gani oil industry inavyotumiwa kuharibu mambo wala tusingelisema. Na kiboko kinakuja baada ya mnunuzi wa BP ambaye inaaminika ni ....kuingia sokoni
   
 7. K

  Katibu Tarafa JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 16, 2007
  Messages: 980
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  wanaochanganya mafuta si madereva wa malori, ila ni wafanyabiashara wanaoagiza hayo mafuta au wanaonunua kutoka depot za mafuta. hawa wanashirikiana na watu wa depot kufanya huu uhalifu. dereva yeye ni kibaru tu na hausiki kwa lolote lile.
   
 8. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  sure....
   
 9. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,163
  Likes Received: 1,122
  Trophy Points: 280
  ..........na yale malori ya mafuta yaliyochachuliwa toka Tanzania yaliyokamatwa Rwanda yameishia wapi?
   
 10. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  tutafika tu kwa kuwa tayari tumeshakuwa damping place na shamba la bibi. Uozo Uozo tu.
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Tamaa itaharibu kila kitu si ajabu hayo mapolisi yamepewa vihela yanaanza kuzungusha mambo...
  Wakati dhahama itawakumba na wao...

  Afu ma-viongozi yetu nayo hivi hawaskii...hawaoni..au kwakua sisi walipa kodi ndo tunaendesha maisha yao..ndo maana hawajali..

  Nyie wenye maamuzi fikieni mahali muone hizo benki na nchi mnazopenda kuweka fedha..na kuishi huko..
  Hao jamaa walipenda Nchi zao kuzijenga hazikushushwa.....

  Ni upuuzi kama huu wa mafuta waliukataa ndo maana leo mnakimbilia huko..
   
 12. M

  MJM JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Poor Tanzania. Ukitoa ushuru kwenye mafuta ya taa ndiyo kwanza unawaua Watanzania wenzetu wanyonge. Tunahitaji utawala wa sheria usioangalia personality. Wanasheria wenyewe wako wapi kina Mkono et al? Safari bado ni ndefu kuliko ya kutafuta uhuru. Tunachotakiwa kusema ni ENOUGH IS ENOUGH. YES WE CAN
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Watu wazito wanahusika humo!
   
 14. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Walaaniwe!
   
 15. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Wana JF,

  Haya Yote mie nayapeleka EWURA

  Kwa any Administration iliyo vyema katika utendaji wake wa kazi ilipaswa itoe haki bin haki kwa tukio lililotokea Moshi baada ya kituo kimoja kuwa na mafuta yachakachua kwanini naseam hivi.

  1: Vituo vyote vya mafuta huwa vyakaguriwa na EWURA huko mikoani na wilayani sasa napenda kujua EWURA wao huwa wamejipanga vipi kwa utaratibu upi wa kukagua vituo vya mafuta??

  Iweje hili kosa liende kuwaangukia walio na kituo cha mafuta pale Moshi kwanini hii ni dhahili kuwa EWURA hawawezi kazi yao na wao wachukuliwe hatua especially viongozi wao wa Moshi; hili ni uzembe mkubwa sana nchi nzima.

  Kwanini nasema hivyo; inaonekana hizi sheria zitungwazo ni za kufanyika Dar tu basi na sio applicable sehemu nyingine ndani ya nchi hii, jamani viongozi angalieni haya m-yafanyayo katika jamii inayowazunguka na kuwapa dhamana ya kuwaongoza nyie mfanye madudu muhukumu mnaowasimamia; hii si haki mmeivuruga sheria hapo.

  2: EWURA inapo toa sheria zake kwa watu wanao husika na taasisi hii je huwa inapewa mamlaka gani katika kujisimamia sheria na utekelezaji wake wa sheria ilizo zitunga??

  eg: Kulitolewa tamko kuwa dereva akutwapo akiendesha gari huku anaongea na simu atashikiliwa. Hili sijaliona likitekerezwa kwanini? Ni kuwa mlilirukia hili swala pasipo kulitizama kiundani na kulipangia mikakati makini kwa ajili ya utekelezaji wake na likawashinda. Kwanini mbwatuke kwa kutunga sheria mzisemazo na kushindwa tekeleza?

  3: Kwanini kila siku twaimbia serikali yetu haiko makini kila kukicha bla bla zimekuwa nyingi sana? Imefika mahali tuache uzembe na tufuatilie utekelezaji.

  4: Hivi wana JF niwaulize kwanini kila kukicha wananchi hasa wafanyabiashara wanakuja na mbinu mpya za ujanja ili kujipatia kipato zaidi na kuwakandamiza watumiaji wakubwa ambao ni watanzania maskini wenye kipato kidogo?

  Je hii ni serikali yetu inashindwa kukaa na kudadisi kujua kunani huko na ni mbinu gani zitumike kuepusha hili balaa la watu kuwa creative kwa kuwanyongea kati raia wasio kuwa na uwezo kuumia katika maisha haya? Na wizara zipi husika zahusika Wizara ya UCHUMI, ULINZI (Mambo ya ndani), TRA?

  Sielewi kuna mzimu gani katika serikali hii!
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Jul 3, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,955
  Trophy Points: 280
  ..kuna mtandao wa matajiri unaojihusisha na biashara ya mafuta machafu nchini.

  ..hawa naona wamekuwa kama poachers wa miaka ile ya 80.
   
 17. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dereva ametoa wito kwa EWURA kwamba waende kupima mafuta ya kwenye tanks za oilcom, Ewura hawakuende wala polisi hawakujali. kilicho fuata ni gari kutoweka. mchawi gani tena tunamtafuta? wachawi ni EWURA na OILCOM (Waigizaji). wengine wapo mjini hawajui umuhimu wa mafuta ya taa kwa 80% ya watanzania. Lets call a spade a spade.Ewura na waigizaji wa mafuta wanahusika basi.
   
 18. D

  Dadake Member

  #18
  Jul 3, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wapendwa wanaJF nawashukuru kwa michango yenu kuhusu taarifa za hujuma katika uchumi wa nchi yetu, zinazofanywa na watu wasiyo na uchungu kwa jamii ya Watanzania. Leo nawahabarisha yaliyompata dereva wa Scania lililosafirisha mafuta hayo.

  Ufuatiliaji wangu umefanikiwa kumpata dereva huyo na amezungumza kwa kinywa chake mwenyewe, amethibitisha kuwa yote niliyoeleza ni kweli tupu, zaidi ya yote ameongeza baadhi ya taarifa zilizokuwa zimekosekana na ameeleza maswahiba yaliyompata baada ya kurejea kwenye kampuni ya Oil Com ambayo inamiliki kampuni ya usafirishaji mafuta ya Al-hushoom.:crying:
   
 19. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Again, we should take interest to know much more about Haruna Masebu, person in charge of EWURA. Naona kama kuna watu hata ndani ya Ewura wananeemeka na hii biashara inayoendelea.

  Na tujue pia kampuni kama oil com inamilikiwa kwa asilimia miamoja na wawekezaji wa ndani ambao wananeemeka sana na political cconnection zilizopo. Hawa Oilcom kuna kipindi kulikuwa na tetesi wangelipewa biashara ya kupeleka mafuta ya ndege kwenye viwanja vyetu, ila hizi big airlines zikagoma. Kama sikosei wakaishia kujenga depot yao Mwanza.

  Sasa kampuni ambayo mambo ya Safety na environment siyo part ya biashara yao watawezaje kuwa players wa kweli kwenye soko?Tukumbuke pia wanaoperate kwenye nchi kama Malawi as Petroda..that tells alot about how big they are.

  Ifike sehemu sasa kila player achunguzwe na watu tujue hili tatizo ni la nani. Tukiacha haya yaendelee, tutakuja jaza maji kwenye ndege maana uovu hauna kiasi.
   
 20. D

  Dadake Member

  #20
  Jul 3, 2010
  Joined: Jul 1, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Salaam wanaJF,

  Kama umesoma taarifa yenye kichea cha habari "Oil Com inahusika kuchakachua mafuta", tutaelewana vizuri katika taarifa hii ambayo ni muendelezo wake.

  Dereva aliyejitambulisha kwa jina la Sulusi Alex Mkude amekiri kuendesha Scania la Oil Com lililopeleka lita 35,000 za dizeli zilizosadikiwa kuwa zilikuwa zimechakachuliwa, na amekiri kuziwasilisha kwa Gasper Msuya, aliyeajiriwa na kampuni inayotengeneza barabara Ushirombo wilayani Bukombe. Amekuwa dereva wa Oil Com kwa miaka 12 na miezi 6.

  Amemtaja kwa jina moja askari polisi wa kituo cha Ushirombo, afande Luso, kuwa ndiye aliyekuwa mpelelezi wa shauri hilo. Anamtaja bosi wa Oil Com ofisi ya Kahama kwa jina moja la Ladwa kuwa ndiye aliita dereva ambaye yeye (Mkude) hamfahamu, akaondoa gari kwenye kituo cha polisi Ushirombo na kuipeleka wanakojua.

  Alirejea Dar es Salaamaam Juni 5, mwaka huu. Akaugua kwa wiki moja na siku tatu kisha akajirejesha ofisini-yadi ya Oil Com iliyo Tabata relini ambapo alikutana uso kwa uso na Scania lililomwacha kituo cha polisi Ushirombo.

  Anasema akamueleza Abdallah Bushilingi ambaye anawajibika kwake, kila kilichompata safarini. Abdallah akamwambia akazungumze na work shop manager anayetajwa kwa jina la Mbaraka. Naye akamwambia akazungumze na Islam ambaye ni meneja wa depot iliyo Kurasini. Hapo anasema hakuonana naye bali sekretari wake baada ya kumweleza uwepo wa Mkude kupitia simu, Islam alitoa maelekezo kwamba akaonane na Norshad ambaye ni msimamizi wa ofisi za Oil Com Tabata relini.

  Akaambiwa, "hamna tatizo, rudi kazini lakini gari lako (scania alilosafirishia mafuta likamwacha kituoni Ushirombo) limerudi likiwa bovu, linatengenezwa hivyo lisimamie litengenezwa vizuri." anawataja mafundi waliyolitengeneza kuwa ni Omari na Rama. lilikuwa na ubovu mbalimbali ikiwemo kupasuka busta.

  Akaambiwa kwa kuwa gari lake bovu, atakuwa anaendesha tiper linalofanya kazi za ndani ya kampuni hiyo kwa sababu dereva wa gari hilo alifiwa akaenda kwenye msiba Morogoro. aliendesha gari hilo kwa siku tatu. siku mbili alisomba kifusi kutoka kwenye eneo la kusaga mawe linalomilikiwa na kampuni hiyo lililopo Boko kukipeleka kwenye yadi mpya iliyopo Tabata relini jirani na AMI.

  Siku ya tatu anasema alisomba udongo uliyochimbwa ndani ya yadi mpya-AMI kuupeleka kwenye yadi mpya nyingine iliyo Malawi cargo, kufukia mashimo. Dereva wa lori hilo aliporudi, akabaki na bila kazi, Juni 28 mwaka huu akapewa Scania T653 ABG aisimamie itengenezwe, ilipokamilika akaambiwa apakie matenki ayapeleke mkoani Mtwara.

  Anasema alipoingia ofisini kwa Norshad kuomba nyaraka za kusafirisha mzigo huo, akaambiwa na Norshad, "Wewe sitaki kukuona ofisini kwangu wala ushike gari langu lolote, toka leo kazi basi, njoo kesho uchukue kiinua mgongo chako."

  Anasema alipokwenda Ijumaa (juzi) akaambiwa aende kesho yake (leo) alipofika leo amepewa sh. 150,000/- kuwa ndicho kiinua mgongo chake kwa miaka 12 na nusu aliyofanyia kazi kampuni hiyo.

  Anasema kwa muda wote huo hakuwahi kuwa na mkataba wa ajira wala kulipiwa mchango wowote katika mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) hivyo alichovuna pekee ni hiyo laki moja na nusu.

  Zaidi anasema ameambiwa, asithubutu kushitaki mahala popote kwa sababu hana atakachopata bali atakuwa amejifungia milango ya ajira ya udereva kwa waarabu wote wanaomiliki magari ya kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi.

  Pia anasema ameambiwa hivi, akae atulie, ikibidi atafute shughuli nyingine na kwamba ikipita muda kama mwaka mmoja hivi akihitaji kazi kwenye kampuni yao wanaweza kumchukua awafanyie kazi tena.

  HAPA inaibuka hoja nyingine ya maslahi ya wafanyakazi katika mashirika ya usafirishaji wa mizigo masafa marefu kwa sababu kumbukumbu zinaonyesha kuwa mfanyakazi mwingine wa kampuni hii anayeitwa George amefungua shitaka kwenye Baraza la Usuluhishi na Upatanishi, kudai malimbikizo ya mapunjo ya mishahara yake na malipo ya kila siku alizokuwa akisafirisha mizigo ya Oil Com, nje ya Nchi.

  Shauri hilo litatajwa tena kwenye baraza hilo la Taifa Julai 5, mwaka huu. Mkude anasema wapo madereva wengi, zaidi ya 300 wanaofanya kazi za kampuni hiyo hawana mikataba ya ajira wala hawalipiwi NSSF. Hoja ni kwamba, ina maana hata NSSF wamewekwa 'viganjani' na Oil Com?

  Binafsi inanikera sana, nayaandika haya ili mnao husika najua mnayasoma. mtambue kuwa nchi ikiingia kwenye machafuko jeuri yenu haitasaidia na hao mnaodhani ni wenzenu hamtawaona bali mtashuhudia raia wasiyo na hatia wakiangamia.

  Hata kama nyinyi mtafanikiwa kuepuka madhara lakini mtaweza kupoteza ndugu, wapendwa na au wana ukoo wenu na hizo mali mnazokumbatia hamtapata raha ya kuwa nazo kwa sababu zitawasuta kila mtakapoziangalia. Jamani, rudisheni moyo wa uzalendo kwa kuacha kukumbatia watu wenye uraia na asili ya Nchi zaidi ya moja ambao wamegeuza Tanzania kuwa sawa na Ubungo Terminal.

  Yaani wapo Tanzania kama wasafiri vile, usafiri wao ukifika (vurugu), kila mmoja wao anachukua kilicho chake na kutokomea. siyo wajinga hawa watu wanajua wanalofanya. hawana hasara ya jina la Tanzania kuchafuka kwa sababu si lao, aibu kwenu vibaraka wao.

  Kwa sasa niwaache, tukutane wakati mwingine nitakapowaletea yatakayozungumzwa na Haruna Masebu wa EWURA, Waziri/Naibu waziri au Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira na maendeleo ya Vijana, uongozi wa NSSF - Taifa kuhusu suala zima la makato ya wafanyakazi hususani madereva wa Oil Com
   
Loading...