Ogopa sana kifaa kinachoitwa “Wireless Speaker”

Ogopa sana kifaa kinachoitwa “Wireless Speaker”

Habalini Wanajanvi.

Zamani zile kabla Tekinolojia haijakua sana hakukua na hizi Wireless Spika zenu za sasa, yaani ili mziki usikike basi Mitambo ilikua ni lazima iunganishwe na Spika kwa kutumia Nyaya.

Sasa siku hizi Spika za kisasa Haziunganishwi kwa Nyaya tena, zinaunganishwa kwa mifumo ya Wireless kama vile mfumo wa Blutooth, au Wi-Fi n.k.

Tatizo la hizi Wireless Spika ni kua zinaweza kuingiliwa na Mitambo tofauti na hivyo Msikilizaji akajikuta anasikiliza mziki usio wa Mitambo yake. Kwa mfano, Spika inaweza kua Dodoma lakini ikaingiliwa ki Blutooth au Ki Wi-Fi na Mitambo iliyopo Dar na hivyo Msikilizaji akajikuta anacheza Mziki wa Dj wa Dar.
Zamani haikua hivyo yaani kama Spika ipo Dodoma basi Msikilizaji atausikia Mziki wa Mitambo ya Dodoma, maana hakukua na njia ya ki Wireless kuunga Mitambo ya Mbali kama ilivyo Leo.

Zamani ilikua Spika ya Dodoma, Mitambo ya Dodoma na Mziki wa Dodoma.

Leo hii ni Spika ya Dodoma, Mitambo ya Dar na Mziki wa Dar.

Kweli Tekinolojia inakuja na Mambo Mapya.
Hakuna technology ya wireless communication kutoka Dar mpaka Dodoma kwa speaker. Kwanza speakers za hivyo au WiFi au Bluetooth yenye nguvu namna huyo havipo.
 
Hakuna technology ya wireless communication kutoka Dar mpaka Dodoma kwa speaker. Kwanza speakers za hivyo au WiFi au Bluetooth yenye nguvu namna huyo havipo.
Wewe ni mgumu kuelewa.... Angalia mada ipo jukwaa gani

😀ont folo folo me wizout ene bikoz:
 
Saboofer au loudspeaker ni kiwakilishi cha ayanenayo mc
 
You can't connect one device in two connections. Hasa wireless speakers or headphones, but inaweza kuwa destructionnetwork nyengine, ikiwa itakuwa so close.
Yaani wewe ndo umetoka kapa kabisa kwenye mada. Hii ni mada fikirishi... unganisha nukta. Hili ni jukwaa la siasa
 
Nimekuelewa lakini lazima nijifanye sijakuelewa nisijeitwa mbele ya kamati ya harusi yenye spika za buluutuusi nikajikuta nacheza singeli badala ya ngoma za wagogo wakwetu Dodoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna technology ya wireless communication kutoka Dar mpaka Dodoma kwa speaker. Kwanza speakers za hivyo au WiFi au Bluetooth yenye nguvu namna huyo havipo.
Usipende kuchangia mada ambayo hujaielewa. Utaonekana zuzu.
 
Back
Top Bottom