Ofisi za AG na DPP kuna nini?

Figisu za maslahi, ofisi ya DPP (polisi) siku hizi hawaendeshi kesi mahakamani na kwa hiyo kukosa machikicho yatokanayo na urasimu na hila kama hizo ulizosikia yule mjane akiziainisha kwa JPM jana!

Kazi ya kuendesha kesi mahakamani inasimamiwa na wanasheria wa serikali kutoka ofisi ya AG ambao kwa maana hiyo ndio wanaonufaika na kansa hiyo!

Chuki ni kwamba ofisi ya AG wananufaika visivyo halali; na kwa kuwa hiyo yote ni kazi haramu hakuna jinsi ya kuweka uwiano wa mgao wa mafao!

Polisi wanachukua risk zote za kukamata wahalifu, wakishakamata issue kwisha kazi wanakabidhi faili kwa AG, wanachapa mwendo! Vijana wa AG wanakula kwa ulaini ndani ya designer suits zao! kisa cha uhasama! Yaani vijana wa AG wanavuna kwenye shamba ambalo hawakulima, wanakula jasho la wenzao!?

Nionavyo, kazi ya kusaka, kukamata na kuendesha mashitaka irejee kwa DPP kikamilifu kwa sababu wao ndio wapelelezi wa kesi kuanzia shina, ofisi ya AG wakikosa ushirikiano wa DPP kwa sababu yoyote ile AG hatakaa ashinde kesi maisha yake hata wakiweka pale magenious wote wa dunia!

Ofisi ya AG wabaki na kazi ya kuandika miswada ya sheria na kuitetea serikali mahakamani au ofisi ya DPP ihamishiwe kwa AG or vice versa, ni mgongano wa maslahi kaka!

Principle of natural justice wont be there,inawezekana kweli polisi akukamate,akuhoji ,akupeleke mahakamani alafu akubali kushindwa?
Hii haikubaliki hata siku moja.

Najua wewe ni layman (mbulula)ila kisheria huo ndio msimamo.
 
Kipindi cha DPP FELESHI AG alikuwa Werema na sio Masaju. Masaju alishika kwa kipindi kifupi baada ya Werema kujiuzuru kwa ESCROW. Hivyo kipindi kitefu cha mgogoro AG alikuwa Werema na DPP Feleshi
Mwajiri wa DPP ni Deputy Attorney General ambaye kipindi hicho alikuwa Masaju na ndio walipambana sana. Deputy ndiye mwajiri wa hao mawakili wote wa serikali unaowaona, na kipindi hicho alikuwa masaju. alishawahi kuwa mwajiri wangu, hivyo siongei toka sokoni, i know everything going on there. feleshi na masaju walishawahi kuwa mabos wangu, na Mganga huyo wa sasa nilishawahi kufanya naye kazi.....alikuwa kijana mdogo tu kwa wale wanaokumbuka alipokuwa Tabora kama wakili wa serikali. ni mchapa kazi sana na hanaga masihara ila kwa ubabe wa pale kwa AG, hadi namuonea huruma. bora wenzie tulishakimbia hiyo ofisi.
 
Pole dogo, umetumia maneno na mitusi mingi kuelezea kile kile nilichopost mwanzo kwamba hawa tatizo lao maslahi dogo! Unatetea wale rushwa kwa kuwa ofisi haiwajali, si ndio mgongano wa maslahi huo au una hangover ya st Kayumba dogo? Anyway umezunguka sana duara nafikiri ni shauri ya kuzoea kula rushwa, lakini bora umefika salama, tatizo ni maslahi dogo, sio madaraka, AG anavuna shamba asilolima! Watenganishiwe majukumu au mmoja wao afutwe!
sijajua umri wako, lakini jua kuwa nimeshafanya kazi kwenye iyo ofisi. ni kweli nilisoma st.kayumba hukoo vijijini, ila ninyi vijana wa sasa tuliowapeleka shule, mnaishia tu kujidai mmesoma shule bora lakini akili hamna. sitabishana na wewe.

unachotakiwa kujua ni kwamba, sio kwamba AG anavuna shamba asilolima. wewe unaongea hivyo ukimaanisha kuwa AG ndiye anaendesha kesi walizopeleleza polisi ambao zamani walikuwa waendesha mashitaka(pp). kwa kifupi ni kwamba, ofisi ya DPP ipo pale Sukari house, wakati ofisi ya AG ipo jengo moja na ofisi ya mambo ya nje kule kivukoni. hakuna hata mtu mmoja anayeendesha kesi kule kwa AG, na kikatiba mwenye mamlaka kusimamia kesi zote za jinai ni DPP sio AG wakati huohuo AG ndiye boss wa DPP (deputy attorney general ambaye pia yupo chini ya AG ni mwajiri wa DPP na mawakili woote wa serikali...dpp pia ni wakili wa serikali...nilishawahi kuwa wakili wa serikali).

mgogoro uliopo ni AG kutaka madaraka yoote, ya kimaslahi na hata kiutendaji wakati mtendaji mkuu kwenye mambo mengi ya ofisi (prosecution) ni mtu mwingine, dpp. ofisi hizi zisipotenganishwa, hakuna ufanisi utafanyika, na hiki ndicho kilikuwa kilio cha feleshi hadi wakamuundia zengwe aondoke kwasababu waliona ana nguvu ya kuweza kunyang'anya madaraka toka kwa AG kwa maslahi ya watz.
 
Do you have an ear to the ground au unaongea Nguini kutoka kwenye vitabu na makabrasha?! Sizungumzii nani anaripoti kwa nani bali tasks and functions per ce! Unaona kuwa ofisi moja hakujawasaidia kufanya kazi smoothly na hujasema tatizo liko wapi sasa kati yako na mimi nani mburula kuliko mwenzie? Angalau mimi nimesogeza mjadala kwa kuainisha ninachoona ni tatizo wewe unapanga majalada ya vyeo nani yuko juu ya nani?!

Kama una kaakili kidogo kalikobaki hebu funguka nini ni sababu ya kusigana baina ya idara hizi nyeti za taifa?! Twambie is it out of sheer incompetence; kama wewe? Au ni overlapping and duplication of functions au mgongano wa maslahi nk nk! Acha kuwa kilaza!
dogo, Task and functions unazotaka tukujibu ni kwamba, mwenye shughuli nyingi zaidi ni DPP kuliko hata AG. Tanzania kuna ofisi za mwanasheria mkuu wa serikali (kwaajili ya kuendesha mashitaka) zaidi ya mikoa 20, na huko kote immediate boss wao alitakiwa kuwa DPP, sio AG kwasababu AG au deputy wake (ambaye ni mwajiri wa dpp) hawahusiki wala hawapo accountable kwa kesi yeyote ya jinai. huyu anahitaji fungu liwe mikononi mwake, sio kwaajili ya kula, bali kuendesha ofisi ikiwepo kuendeshea magari kupeleka mawakili mahakamani, kulipa nauli mawakili kwenda kuendesha kesi mikoa mbalimbali na mambo mengine mengi. sisi wenzio tunaongea tulishafanya kazi huko, wewe ni mwanafunzi sijui wa chuo gani haujui hata unachoongea.
 
Principle of natural justice wont be there,inawezekana kweli polisi akukamate,akuhoji ,akupeleke mahakamani alafu akubali kushindwa?
Hii haikubaliki hata siku moja.

Najua wewe ni layman (mbulula)ila kisheria huo ndio msimamo.
Ok Mr know it all, the self righteous, mbona umesahau kwamba kuna mahakama, mhimili tofauti!
 
N
...Very well said. Sasa mkuu ikiwa katiba inawatambua kama watu 2 tofauti why mmoja akamtia kwapani mwenzake? Kwa nini AG alivyojinasua toka wizara ya katiba na sheria hawakufikiria kuwa na two separate offices? (ya AG na DPP i mean).
Nyerere alisema dhambi ya kujitenga haishi. Baada ya DPP kujitenga atakuja division ya assets recovery ndani ya DPP kutaka kujitenga
 
wewe ni sifuri, hujui unachoongea kama wanavyokuambia. DPP ni mwajiriwa kabisa wa ofisi ya AG na ni wakili wa serikali Mkuu (principal state attorney) ndiye anateuliwa kuwa DPP. sio polisi, umechanganya DPP na DCI. DCI ni Director of Criminal Investigation ambaye anasimamia masuala yote ya upelelezi wa kesi. ila mwenye mamlaka ya kufungua mashitaka ya jinai, kuyaendesha au kuyafuta ni DPP aliyepo ofisi ya AG. Zamani kwasababu mawakili wa serikali walikuwa wachache, DPP kwa mamlaka yake alikuwa ana delegate polisi (pp) kuwa public prosecutors, lakini siku hizi mawakili ni wengi, pamoja na kwamba delegation hiyo bado inaendelea, ni kwa wilayani tu ambako ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali haijafika. kwa taarifa yako, mawakili wa serikali woote mikoani immediate boss wao ni DPP, AG hajihusishi na masuala yeyote ya criminal prosecution na hana power hiyo, mwenye power hiyo ni DPP ambaye ni mwajiriwa wake....

mgongano uliopo pale, bila kuficha ni kugombania madaraka, na hilo ndilo alilisema rais jana,...DPP ni appointee wa Rais, the same applies to AG na deputy wake. lakini anayefanya kazi nyingi zaidi ni DPP kwasababu ofisi hiyo pamoja na kwamba kuna mambo mengi sana, shughuli kubwa ni kuendesha kesi za jinai ambazo zote mamlaka yake hayapo chini ya AG bali DPP. sasa kuna mtifuano hapo, wakati huyu anayesimamia keso zote za jinai anahitaji labda pesa au chochote kuwezesha mawakili wa serikali kushinda kesi, mwingine anabada kwasababu tu yeye ni boss wa DPP, hapo ndipo wanaanza kutunishiana misuli na ndio ugomvi. AG offisi inamwangusha sana DPP kiutendaji na hawatoi sapoti ya kutosha. ninasema hivyo kwasababu nilishafanya kazi kama wakili wa serikali nikaacha. mawakili wana maisha magumu sana wanapelekeshwa ile mbaya kuendesha kesi za mamilioni, lakini vitendea kazi na motisha hamna, hayo yote yanatakiwa kuamuliwa kule kwa MASAJU, ninasikia hapa juzi hata mamlaka ya kuwa signatory DPP wamemnyang'anya, hivyo chochote atakachotaka kufanya, hata kama anataka kutuma vijana wake wakaendeshe kesi mkoani harakaharaka haiwezekani hadi aombe ruhusa ya pesa kwa AG na deputy wake. kuna mengi naomba nisifichue sana, ila solution ni hiii:

RAIS, TENGANISHA OFISI YA AG NA OFISI YA DPP, ziwe ofisi mbili kama ilivyo nchi zingine. DPP anashindwa kufanya kazi chini ya AG kwasababu yeye ana mamlaka makubwa sana pengine kiutendaji yanamzidi hata boss wake AG, sasa hapo boss hataki kuonekana kazidiwa ndio maana anamkwamisha mwezake. i am speaking from experience na hii ndio solution. ukifanya hivyo, kesi zitakuwa zinenda haraka, watashinda kesi na mawakili hawatakuwa wanaacha kazi na kula rushwa kila siku au kushirikiana na upande wa washitakiwa kuharibu kesi. ni sawa na kumweka mbwa alinde nyama wakati haujampa chakula cha kula. unafikiri ataacha, ni mtu punguani tu ataacha kula rushwa wakati maisha yake magumu ofisi haimjali. ndio maana kila mwezi kuna watu wanahama hiyo ofisi kwasababu haina motisha, ni ngumu san akufanya iyo ofisi.
Nimekupata uwakili kazi ngumu
 
N

Nyerere alisema dhambi ya kujitenga haishi. Baada ya DPP kujitenga atakuja division ya assets recovery ndani ya DPP kutaka kujitenga
nyerere hakuwa Mungu aisee, sio kila alichosema ni sahihi. pia jua kipindi hicho aliongea kukiwa na "zidumu fikra za mwenyekiti wa chama"..watu wanasema zidumuuuu? yaani kile anachofikiria watu akiamini na kukibeba ivyohivyo. nijuavyo mimi, na nilivyotafiti, asset recovery ipo chini ya DPP na wanaendesha kesi, hivyo ni waendesha mashitaka. lakini, hata wakijitenga, kama ufanisi kuhudumia raia upo kuna shida gani?
 
hao wawili wana matitizo yao personal wala hayana uhusiano na kazi,
... Kupitia Michango mingi hapa tumeona kuna tatizo kuu la kimuundo kwenye hii ofisi, sasa hebu tujuze if it is personal wanagombea nini? You really think JPM akiwatoa wote na kuleta new faces itakuwa problem solved?
 
Wakuu leo nimemsikia mhe rais akisema ofisi hizi mbili hakuna maelewano, na akaenda mbali kusema kwamba pamoja na AG na DPP kutoka mkoa mmoja and possibly wilaya moja, anashangaa kwanini hawaelewani. Nani anayejua chanzo cha mgogoro wao?
Kama Rais nae anashangaa nasi inabidi tumshangae, amesahau tumbuatumbua yake au kilikuwa kimbunga? Kwanini hawa anawashangaa badala ya kuwatumbua?
 
Figisu za maslahi, ofisi ya DPP (polisi) siku hizi hawaendeshi kesi mahakamani na kwa hiyo kukosa machikicho yatokanayo na urasimu na hila kama hizo ulizosikia yule mjane akiziainisha kwa JPM jana!

Kazi ya kuendesha kesi mahakamani inasimamiwa na wanasheria wa serikali kutoka ofisi ya AG ambao kwa maana hiyo ndio wanaonufaika na kansa hiyo!

Chuki ni kwamba ofisi ya AG wananufaika visivyo halali; na kwa kuwa hiyo yote ni kazi haramu hakuna jinsi ya kuweka uwiano wa mgao wa mafao!

Polisi wanachukua risk zote za kukamata wahalifu, wakishakamata issue kwisha kazi wanakabidhi faili kwa AG, wanachapa mwendo! Vijana wa AG wanakula kwa ulaini ndani ya designer suits zao! kisa cha uhasama! Yaani vijana wa AG wanavuna kwenye shamba ambalo hawakulima, wanakula jasho la wenzao!?

Nionavyo, kazi ya kusaka, kukamata na kuendesha mashitaka irejee kwa DPP kikamilifu kwa sababu wao ndio wapelelezi wa kesi kuanzia shina, ofisi ya AG wakikosa ushirikiano wa DPP kwa sababu yoyote ile AG hatakaa ashinde kesi maisha yake hata wakiweka pale magenious wote wa dunia!

Ofisi ya AG wabaki na kazi ya kuandika miswada ya sheria na kuitetea serikali mahakamani au ofisi ya DPP ihamishiwe kwa AG or vice versa, ni mgongano wa maslahi kaka!
Ongea unayoyajua
 
Ok Mr know it all, the self righteous, mbona umesahau kwamba kuna mahakama, mhimili tofauti!
uzoefu dunia nzima umeonyesha kwamba, ukikamata, kupeleleza na kupeleka mahakamani wewe mwenyewe kuna ubambikizaji kesi mwingi. wewe ni mwanafunzi tu haujaanza kufanya kazi unavyoonyesha. sisi ambao tumekuwepo kwenye field miaka mingi, serikalini na private, tumeshaona kuna ubambikizaji kesi mwingi sana ulikuwa unafanywa na polisi, na unafanywa hata leo hii. kama hakitakuwepo kitengo kingine cha kuwaweka accountable hawa watu, haki haitatendeka kwa watu wengi sana. wanachofanya polisi kwa sasa ni kukamata na kukusanya upelelezi afu jalada wanapeleka kwa DPP, akiona mmekusanya ushahidi wa kumsaidia mtuhumiwa, ushahidi hafifu etc, anarudisha jalada mpeleleza vizuri kwa maelekezo. kuna mengi yanaendelea ambayo nahisi hauyajui na ni vigumu sana kukutolea lecture hapa, ni kupoteza muda, labda ufanye utafiti.
 
hahaha, hicho kitu ukiongea mbele ya AG kama siku hiyo hajaamka vizuri anaweza kukurushia makonde (kidding). Kati ya sababu kubwa ya ugomvi ni DPP kuweka mapendekezo kuwa ajitenge iwe ofisi inayojitegemea, na ndilo bifu lililomsumbua sana Feleshi. AG anataka dpp awe chini yake na kwa vile ni mwajiriwa wake ndio anataka aendelee kuwa chini yake. kwa uzoefu ninavyoangalia nchi zingine, ofisi ya DPP inajitegemea. Pamoja maneno yoote waliyomsema Feleshi, wakitaka tatizo hili litatuliwe once and for all, wamwite Feleshi awape ushauri kwasababu yeye ndiye alipata shida sana na hiyo ofisi ya boss wake AG, na Feleshi alijitahidi sana kupambana ijitenge iwe kama ilivyo nchi zingine ili ufanisi uwepo, lakini alipoondoka tu, yote aliyokuwa ameimarisha feleshi yamenyang'anywa kwa Mganga na yamerudishwa kwa AG. ofisi hiyo kufanya bila kuwa independent ni ngumu sana. ndugu zetu wanafanya kazi hapo, tangu Feleshi aondoke hapo kwa dpp, kila kitu kimelala na yamebaki mapambano tu ya mamlaka, na anayeonewa ni DPP. AG awe na ofisi yake na DPP awe na ofisi yake kama kitengo ndio ataweza kutoa maamuzi kwa uhuru na ufanisi, kama sivyo hivyo, tutaendelea kuona yanayoendelea.
... Dah kweli kazi ipo. So this was the source, na kwa kweli sitashangaa kusikia serikali iliendelea kushindwa kesi kama alivyosema JPM, maana muda wote wako bize na vita ya mamlaka. Now that it's obvious AG kamwe hatakubali kumwachia DPP it is only president who can resolve this. Sasa najiuliza why since Mkapa, JK and JPM wanasita kumuua nyoka kichwani once and for all??
 
Kama Rais nae anashangaa nasi inabidi tumshangae, amesahau tumbuatumbua yake au kilikuwa kimbunga? Kwanini hawa anawashangaa badala ya kuwatumbua?
kama ulimsikiliza rais vizuri, alisema..." kwani wote si appointee wa rais"?....hapo anaongea kati ya watu wawili, mmoja boss mwingine subordinate. kwa akili ya kawaida unafikiri amemhukumu nani hapo? ni kwamba anamtuhumu attorney general kwamba ampe DPP heshima yake na amwache afanye majukumu yake, kuwa kwake boss kusizuie kazi zake na asimbane sana kwani hata dpp ni appointee wa rais...maana yake pia ni kama amewaweka wote kuwa wapo sawa tu mbele yake hakuna boss wa mwenzake. kwani nyie wote si appointee wangu?hahaha. kati ya mdogo na mkubwa unafikiri nani alikuwa anasutwa apo?
 
Mwajiri wa DPP ni Deputy Attorney General ambaye kipindi hicho alikuwa Masaju na ndio walipambana sana. Deputy ndiye mwajiri wa hao mawakili wote wa serikali unaowaona, na kipindi hicho alikuwa masaju. alishawahi kuwa mwajiri wangu, hivyo siongei toka sokoni, i know everything going on there. feleshi na masaju walishawahi kuwa mabos wangu, na Mganga huyo wa sasa nilishawahi kufanya naye kazi.....alikuwa kijana mdogo tu kwa wale wanaokumbuka alipokuwa Tabora kama wakili wa serikali. ni mchapa kazi sana na hanaga masihara ila kwa ubabe wa pale kwa AG, hadi namuonea huruma. bora wenzie tulishakimbia hiyo ofisi.
... Mkuu nimekukubali kwa madini unayomwaga hapa, umetufungua macho.
 
... Dah kweli kazi ipo. So this was the source, na kwa kweli sitashangaa kusikia serikali iliendelea kushindwa kesi kama alivyosema JPM, maana muda wote wako bize na vita ya mamlaka. Now that it's obvious AG kamwe hatakubali kumwachia DPP it is only president who can resolve this. Sasa najiuliza why since Mkapa, JK and JPM wanasita kumuua nyoka kichwani once and for all??
kaka, ukiwatenganisha kama jamaa anavyosema, AG Hatabaki na kitu kabisa, kwasababu mtendaji mkuu wa ofisi ya mwanasheria mkuu ni DPP kwasababu shughuli zilizo nyingi hapo ni kuendesha mashitaka. ukimwondoa DPP, attorney general atabaki na division ya katiba na sheria, division ya mikataba, division ya mashauri ya madai...hapo division ya mashauri ya jinai anayoshikilia DPP itakuwa imenyofoka. hizo division zingine ukiondoa ya kuendesha mashitaka(dpp) ni watu wachache sana hata 500 sidhani kama wanafika ukijumuisha na makatibu muhtasi na wafagiaji. ofisi zote mikoani zinazoendesha mashauri ya madai ni kesi chache sana hivyo wanajikuta wote wanafanya kazi za DPP tu,...

hata hivyo, haitakuwa shida kwasababu kama kuna kesi ya madai, attorney general anacho kitengo cha madai na mikataba pale chenye mawakili wa serikali wanaozunguka nchi nzima kuendesha kesi za madai....nashauri watenganisha haraka ili kuwe na ufanisi, na wakitenganisha, arudishwe Feleshi ndiye alikuwa anaiweza hiyo ofisi na ndiye alikuwa amekubalika dunia nzima. alipoondoka nasikia aliondoka na kila kitu...wafadhili wakakimbia, misaada kwenye iyo ofisi ikakauka kwasababu watu waliona jembe limeondoka....hata kikwete alikuja kujilaumu baadaye kwa kuona amepotoshwa akatamani kumrudisha lakini ikawa ngumu.
 
Nimesubiri kidogo nikidhani kuna atakayeonyesha ''ugonjwa'', hakuna
Wote tunapiga 'ramli' kwanini AG na DPP hawaelewani

Kwanza, kusema kuwa wanatoka Mkoa mmoja au Wilaya haikuwa na ladha
Ina 'invoke' fikra za ukabila. Wapo watakaohoji kwanini watatu hao hawakai kumaliza tofauti?

Mahusiano ya AG na DPP yanaongozwa na sheria za kazi na miiko na mipaka yao
Hayongozwi kwa kuangalia majina, ukabila, ukanda au udini. Hili ninaliona kama tatizo linalozidi kumea

Pili, AG na DPP ni wateuliwa wa Rais wanawajibika kwake. Wanaweza kumuona wakati wowote

Tofauti zao ziwe za kimkoa Wilaya, kikazi au vinginevyo zinasikilizwa na Mh Rais

Iweje basi Rais aliyewateua arudi kulalamika kwetu tusiojua watu hawao wanapatikana kwa vigezo gani?

Iweje basi kama kuna mgongano wa kikazi, kimasilahi n.k. Rais asitafute ufumbuzi huko ofisini?

Kutueleza wananchi matatizo ya ofisini ni kututwisha mzigo wa bure

Hata tukibaini AG au DPP mmoja wao ni tatizo, kwa mujibu wa katiba tutafanya nini cha ziada?

Hili linaeleza vema hoja ya mfumo mbaya na haja ya katiba
 
Kama Rais nae anashangaa nasi inabidi tumshangae, amesahau tumbuatumbua yake au kilikuwa kimbunga? Kwanini hawa anawashangaa badala ya kuwatumbua?
... Hili ni moja ya swali ambalo nami nasubiri majibu hapa. Hakuna mashaka kabisa kwamba suala hili ni rais pekee anayesubiriwa ku intervene, nimeshangaa pia naye jana hakulihitimisha.
 
Figisu za maslahi, ofisi ya DPP (polisi) siku hizi hawaendeshi kesi mahakamani na kwa hiyo kukosa machikicho yatokanayo na urasimu na hila kama hizo ulizosikia yule mjane akiziainisha kwa JPM jana!

Kazi ya kuendesha kesi mahakamani inasimamiwa na wanasheria wa serikali kutoka ofisi ya AG ambao kwa maana hiyo ndio wanaonufaika na kansa hiyo!

Chuki ni kwamba ofisi ya AG wananufaika visivyo halali; na kwa kuwa hiyo yote ni kazi haramu hakuna jinsi ya kuweka uwiano wa mgao wa mafao!

Polisi wanachukua risk zote za kukamata wahalifu, wakishakamata issue kwisha kazi wanakabidhi faili kwa AG, wanachapa mwendo! Vijana wa AG wanakula kwa ulaini ndani ya designer suits zao! kisa cha uhasama! Yaani vijana wa AG wanavuna kwenye shamba ambalo hawakulima, wanakula jasho la wenzao!?

Nionavyo, kazi ya kusaka, kukamata na kuendesha mashitaka irejee kwa DPP kikamilifu kwa sababu wao ndio wapelelezi wa kesi kuanzia shina, ofisi ya AG wakikosa ushirikiano wa DPP kwa sababu yoyote ile AG hatakaa ashinde kesi maisha yake hata wakiweka pale magenious wote wa dunia!

Ofisi ya AG wabaki na kazi ya kuandika miswada ya sheria na kuitetea serikali mahakamani au ofisi ya DPP ihamishiwe kwa AG or vice versa, ni mgongano wa maslahi kaka!
Umeandika mengi lakini hujui unachokieleza
 
Back
Top Bottom