Ofisi za AG na DPP kuna nini?

Ofisi za AG na DPP kuna nini?

Mkuu kila nikikumbuka ule mgongano uliokuwepo kati ya DPP Feleshi na Mkurugenzi wa Takukuru Hosea wakati ule, aisee NAKUELEWA sana usemacho.
Imagine watu wameshasahau hata sakata hilo la Feleshi na Edward Hosea la majuzi tuu?! Anaibuka kizuka hapa anasema sijui ninachoongea! Ajabu na kweli!
 
...Mkuu with all due respect hebu tema huyo ubuyu ulioko moyoni mwako, ili nasi tumsaidie Mh JPM. Unajua jana kile kitendo cha yule mjane mjasiri kumuibukia Mhe Rais ni fedheha sana kwa wasaidizi wa rais ambao yule mama aliwataja? Hatuwezi fanikiwa kwa show ya mtu mmoja aisee.
Yeees! Mwambie huyo jeff kapita asipite afunguke tumsaudie Rais, ya jana yalikuwa aibu kubwa kwa taifa!
 
Wakuu leo nimemsikia mhe rais akisema ofisi hizi mbili hakuna maelewano, na akaenda mbali kusema kwamba pamoja na AG na DPP kutoka mkoa mmoja and possibly wilaya moja, anashangaa kwanini hawaelewani. Nani anayejua chanzo cha mgogoro wao?
Afukuze kazi hakuna namna yaani mpaka leo bado wapo?
 
jamaa kusema hajui anachoongea ni kweli kabisa. DPP ni department ndani ya ofisi ya AG. DPP sio polisi, and it strikes me when president says ofisi ya DPP. hakuna ofisi ya DPP kuna cheo cha DPP ambacho ndio top wa idara ya mashtaka. top wa ofisi ni AG. kwa AG kuna presidential appointee wengine sio AG, DAG na DPP, CPD pia ni presidential appointee. Mkuu wa nchi awaite watu wake atoe maelekezo na sio kubwabwaja mbele za watu kutaka political mileage kwenye mambo ya kiutendaji.

...Now you are talking mkuu, lakini pamoja na hayo mapungufu uliyotujuza why hawa watu wawili wateule wa rais hawaivi? Maslahi kama alivyosema MTK au ni nini hasa? Hata Waziri ameshindwa ku intervene?
 
Rais wangu ana kazi sana katika kuinyoosha hii nchi yani kuna watu wameamua kuishi kama vile Mungu hayupo ila kilio cha yule mama nina hakika kimefika mwisho machozi ya mnyonge hulipwa na Mungu naamini mama atakuwa na Amani ndani ya Moyo wake kwa sasa na atakuwa ameutua mzigo mzito uliokuwa ukimwelemea baada ya kupata faraja kutoka kwa Rais naamini haki ipo juu yake Mwenyezi Mungu amwinue mjane huyu.
 
Figisu za maslahi, ofisi ya DPP (polisi) siku hizi hawaendeshi kesi mahakamani na kwa hiyo kukosa machikicho yatokanayo na urasimu na hila kama hizo ulizosikia yule mjane akiziainisha kwa JPM jana!

Kazi ya kuendesha kesi mahakamani inasimamiwa na wanasheria wa serikali kutoka ofisi ya AG ambao kwa maana hiyo ndio wanaonufaika na kansa hiyo!

Chuki ni kwamba ofisi ya AG wananufaika visivyo halali; na kwa kuwa hiyo yote ni kazi haramu hakuna jinsi ya kuweka uwiano wa mgao wa mafao!

Polisi wanachukua risk zote za kukamata wahalifu, wakishakamata issue kwisha kazi wanakabidhi faili kwa AG, wanachapa mwendo! Vijana wa AG wanakula kwa ulaini ndani ya designer suits zao! kisa cha uhasama! Yaani vijana wa AG wanavuna kwenye shamba ambalo hawakulima, wanakula jasho la wenzao!?

Nionavyo, kazi ya kusaka, kukamata na kuendesha mashitaka irejee kwa DPP kikamilifu kwa sababu wao ndio wapelelezi wa kesi kuanzia shina, ofisi ya AG wakikosa ushirikiano wa DPP kwa sababu yoyote ile AG hatakaa ashinde kesi maisha yake hata wakiweka pale magenious wote wa dunia!

Ofisi ya AG wabaki na kazi ya kuandika miswada ya sheria na kuitetea serikali mahakamani au ofisi ya DPP ihamishiwe kwa AG or vice versa, ni mgongano wa maslahi kaka!
yaani kati ya watu walioanika ujinga wao leo wewe ni wa kwanza. angalia kwenye red, hivi unajua kuwa DPP ni ofisi iliyo chini ya AG?..usichanganye ofisi ya DPP na ofisi ya DCI.

kwa kifupi ni kwamba, ofisi ya AG ina section kadhaa, mojawapo ni ofisi ya DPP...ambaye ni mwajiriwa wa AG. DPP sio polisi na hapelelezi kesi, hao mawakili wa serikali wooote wanaoendesha kesi za jinai wapo chini ya DPP na DPP mwenyewe ni wakili wa serikali aliyeajiriwa na kulipwa mshahara na AG.

ama kweli kutokuwa informed kunaweza kumfanya mtu aropoke chochote. pole sana.
 
Mkuu kila nikikumbuka ule mgongano uliokuwepo kati ya DPP Feleshi na Mkurugenzi wa Takukuru Hosea wakati ule, aisee NAKUELEWA sana usemacho.
kati ya feleshi na hosea nani unafikiri alikuwa tatizo? mmoja ni jaji sasaivi, mwingine alitumbuliwa na hana kazi yeyote sasaivi, sijui analima au anachunga ng'ombe.
 
Kuna vitu vitatu vya kuangalia hapa

1.Mgongano wa maslahi namaanisha uwepo wa mmoja wao unamnyima ugali mwenzake
2.Muingiliano wa majukumu hapa namaanisha serikali imeshindwa kutenganisha majukumu ya AG na DPP hivo kupelekea wote kuwa na majukumu yanayofanana nhali inayoweza kusababisha mgongano wa maslahi kama nilivyoeleza hapo juu
3. Kutotambua malengo,madhumunu ya uanzishwaji,kazi wanazowajibika kuzifanya na mipaka ya uwajibikaji wa ofisi husika,Inawezekana pia ikatokea hilo hivo kupelekea mmoja wao kufanya kazi za mwenzake.

Uchunguzi uanzie kwa AG maana hiyo ofisi toka kipindi imeunganishwa na wizara ya katiba na sheria walikuwa na migongano mikubwa sana mpaka kipindi wanatenganishwa ndipo hali ikawa shwari sasa uko uwezakano hayo mambo machache niliyoyataja hapo juu yote yamefall kwa AG
ajabu yake, mmoja wa wale waliokuwa wanagongana na ofisi ya DPP tangu enzi za FELESHI ni huyo AG wa sasa, sasa kusemwa mbele za watu vile jana ina maana anafaa au hafai, amesolve vipi mgogoro huo? DPP wa sasa ni mtoto mdogo hajui kitu watamuonea tu maugomvi hayo ameyakuta. wamuulize MASAJU huo ugomvi kwanini hauishi? na yeye alikuwepo tangu miaka ya nyuma na kutuhumiwa kuwa ndiye anayegombana na ofisi ya DPP? tumbua mbali huko.
 
Figisu za maslahi, ofisi ya DPP (polisi) siku hizi hawaendeshi kesi mahakamani na kwa hiyo kukosa machikicho yatokanayo na urasimu na hila kama hizo ulizosikia yule mjane akiziainisha kwa JPM jana!......
Aisee kumbe safari ni ndefu sana kuliko nilivyokuwa nafikili. Kuna haja somo la Katika likawa linarushwa clouds media labda watu wataelewa. DPP ni sehemu ya AG, ukisema ni sehemu ya polisi hueleweki labda Kenya ndiyo ipo hivyo.
 
jamaa kusema hajui anachoongea ni kweli kabisa. DPP ni department ndani ya ofisi ya AG. DPP sio polisi, and it strikes me when president says ofisi ya DPP. hakuna ofisi ya DPP kuna cheo cha DPP ambacho ndio top wa idara ya mashtaka. top wa ofisi ni AG. kwa AG kuna presidential appointee wengine sio AG, DAG na DPP, CPD pia ni presidential appointee. Mkuu wa nchi awaite watu wake atoe maelekezo na sio kubwabwaja mbele za watu kutaka political mileage kwenye mambo ya kiutendaji.
lakini ana washauri wengine waliotoka palepale kwa AG wanafanya kazi kwake, hawasikilizi au hawaulizi vitu kabla ya kuja kuongea? ila kusema ukweli, ugomvi huo upo na umeathiri sana wafanyakazi walio chini ya DPP na wale waliochini ya AG moja kwa moja. AG ni boss wa wote, hata dpp yupo chini ya AG lakini hao mawakili wa serikali na ofisi zote za mkoani anayewajibika sana ni DPP. katika ofisi ya Attorney general, anayewajibika sana na mwenye majukumu mengi ni DPP kuliko AG.
 
Imagine watu wameshasahau hata sakata hilo la Feleshi na Edward Hosea la majuzi tuu?! Anaibuka kizuka hapa anasema sijui ninachoongea! Ajabu na kweli!
Mkuu Jf ya sasa imejaa kizazi kipya!Turudi madani mi naona kitendo cha kumweka DPP " mtu kati" yaani huku kuna DCI huku kuna AG na kule kuna Boss Takukuru kinaleta ukakasi na hivyo kuzaa utengamano Ofisi ya DPP inatakiwa iwe "independent" ikiwa na nguvu zake zote, na hili litawezekana tu pale siasa zitakapowekwa pembeni.
 
Aaaargh! Wewe ndio umeharibu kabisa!
wewe ni sifuri, hujui unachoongea kama wanavyokuambia. DPP ni mwajiriwa kabisa wa ofisi ya AG na ni wakili wa serikali Mkuu (principal state attorney) ndiye anateuliwa kuwa DPP. sio polisi, umechanganya DPP na DCI. DCI ni Director of Criminal Investigation ambaye anasimamia masuala yote ya upelelezi wa kesi. ila mwenye mamlaka ya kufungua mashitaka ya jinai, kuyaendesha au kuyafuta ni DPP aliyepo ofisi ya AG. Zamani kwasababu mawakili wa serikali walikuwa wachache, DPP kwa mamlaka yake alikuwa ana delegate polisi (pp) kuwa public prosecutors, lakini siku hizi mawakili ni wengi, pamoja na kwamba delegation hiyo bado inaendelea, ni kwa wilayani tu ambako ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali haijafika. kwa taarifa yako, mawakili wa serikali woote mikoani immediate boss wao ni DPP, AG hajihusishi na masuala yeyote ya criminal prosecution na hana power hiyo, mwenye power hiyo ni DPP ambaye ni mwajiriwa wake....

mgongano uliopo pale, bila kuficha ni kugombania madaraka, na hilo ndilo alilisema rais jana,...DPP ni appointee wa Rais, the same applies to AG na deputy wake. lakini anayefanya kazi nyingi zaidi ni DPP kwasababu ofisi hiyo pamoja na kwamba kuna mambo mengi sana, shughuli kubwa ni kuendesha kesi za jinai ambazo zote mamlaka yake hayapo chini ya AG bali DPP. sasa kuna mtifuano hapo, wakati huyu anayesimamia keso zote za jinai anahitaji labda pesa au chochote kuwezesha mawakili wa serikali kushinda kesi, mwingine anabada kwasababu tu yeye ni boss wa DPP, hapo ndipo wanaanza kutunishiana misuli na ndio ugomvi. AG offisi inamwangusha sana DPP kiutendaji na hawatoi sapoti ya kutosha. ninasema hivyo kwasababu nilishafanya kazi kama wakili wa serikali nikaacha. mawakili wana maisha magumu sana wanapelekeshwa ile mbaya kuendesha kesi za mamilioni, lakini vitendea kazi na motisha hamna, hayo yote yanatakiwa kuamuliwa kule kwa MASAJU, ninasikia hapa juzi hata mamlaka ya kuwa signatory DPP wamemnyang'anya, hivyo chochote atakachotaka kufanya, hata kama anataka kutuma vijana wake wakaendeshe kesi mkoani harakaharaka haiwezekani hadi aombe ruhusa ya pesa kwa AG na deputy wake. kuna mengi naomba nisifichue sana, ila solution ni hiii:

RAIS, TENGANISHA OFISI YA AG NA OFISI YA DPP, ziwe ofisi mbili kama ilivyo nchi zingine. DPP anashindwa kufanya kazi chini ya AG kwasababu yeye ana mamlaka makubwa sana pengine kiutendaji yanamzidi hata boss wake AG, sasa hapo boss hataki kuonekana kazidiwa ndio maana anamkwamisha mwezake. i am speaking from experience na hii ndio solution. ukifanya hivyo, kesi zitakuwa zinenda haraka, watashinda kesi na mawakili hawatakuwa wanaacha kazi na kula rushwa kila siku au kushirikiana na upande wa washitakiwa kuharibu kesi. ni sawa na kumweka mbwa alinde nyama wakati haujampa chakula cha kula. unafikiri ataacha, ni mtu punguani tu ataacha kula rushwa wakati maisha yake magumu ofisi haimjali. ndio maana kila mwezi kuna watu wanahama hiyo ofisi kwasababu haina motisha, ni ngumu san akufanya iyo ofisi.
 
Aiseee kichwa kinauma
 
Mkuu Jf ya sasa imejaa kizazi kipya!Turudi madani mi naona kitendo cha kumweka DPP mtu kati yaani huku kuna DCI huku kuna AG na kule kuna Boss Takukuru kinaleta ukakasi na hivyo kuzaa utengamano Ofisi ya DPP inatakiwa iwe "independent" ikiwa na nguvu zake zote, na hili litawezekana tu pale siasa zitakapowekwa pembeni.
wewe ndio umeongea kitu. hiyo ofisi inaishi kishujaa sana, kwasababu huku kuna AG boss wake/mwajiri, huku kuna DCI wapelelezi, huku kuna PCCB walio chini ya ofisi ya rais (Wapelelezi), anawekwa mtu kati, masimango kila kona. hapohapo mawakili wa serikali nchi nzima wapo chini yake (immediate boss wao kesi za jinao)...inatakiwa iwe independent kabisa, hata rais hatakiwi kuiamrisha hivyo.
 
Mkuu Jf ya sasa imejaa kizazi kipya!Turudi madani mi naona kitendo cha kumweka DPP " mtu kati" yaani huku kuna DCI huku kuna AG na kule kuna Boss Takukuru kinaleta ukakasi na hivyo kuzaa utengamano Ofisi ya DPP inatakiwa iwe "independent" ikiwa na nguvu zake zote, na hili litawezekana tu pale siasa zitakapowekwa pembeni.
...Huu mtazamo na mimi nauunga mkono.
 
yaani kati ya watu walioanika ujinga wao leo wewe ni wa kwanza. angalia kwenye red, hivi unajua kuwa DPP ni ofisi iliyo chini ya AG?..usichanganye ofisi ya DPP na ofisi ya DCI.

kwa kifupi ni kwamba, ofisi ya AG ina section kadhaa, mojawapo ni ofisi ya DPP...ambaye ni mwajiriwa wa AG. DPP sio polisi na hapelelezi kesi, hao mawakili wa serikali wooote wanaoendesha kesi za jinai wapo chini ya DPP na DPP mwenyewe ni wakili wa serikali aliyeajiriwa na kulipwa mshahara na AG.

ama kweli kutokuwa informed kunaweza kumfanya mtu aropoke chochote. pole sana.
Do you have an ear to the ground au unaongea Nguini kutoka kwenye vitabu na makabrasha?! Sizungumzii nani anaripoti kwa nani bali tasks and functions per ce! Unaona kuwa ofisi moja hakujawasaidia kufanya kazi smoothly na hujasema tatizo liko wapi sasa kati yako na mimi nani mburula kuliko mwenzie? Angalau mimi nimesogeza mjadala kwa kuainisha ninachoona ni tatizo wewe unapanga majalada ya vyeo nani yuko juu ya nani?!

Kama una kaakili kidogo kalikobaki hebu funguka nini ni sababu ya kusigana baina ya idara hizi nyeti za taifa?! Twambie is it out of sheer incompetence; kama wewe? Au ni overlapping and duplication of functions au mgongano wa maslahi nk nk! Acha kuwa kilaza!
 
Back
Top Bottom