DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 8,591
- 17,711
Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Imetangaza Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini inayowezesha nguvu kazi ya Taifa kupata ujuzi na stadi za kazi stahiki ili kumudu ushindani katika soko la ajira.
Ofisi imeingia makubaliano vyuo mbalimbali kutoa mafunzo mafunzo ya ufundi stadi kukuza ujuzi na stadi za kazi kwa vijana. Miongoni mwa mafunzo yatakayotolewa ni Ubunifu wa Mitindo na Ushonaji Nguo, Ufundi Bomba, Uashi, Useremala, Uchomeleaji na Uungaji vyuma, Upakaji rangi na maandishi ya alama, Utengenezaji wa vipuri vya mitambo, Ufundi Magari na Mitambo, Umeme wa Majumbani na Viwandani, TEHAMA, Umeme wa Magari, Huduma za Hoteli na Utalii, Ukataji Madini ya Vito na Kilimo.
Mafunzo hayo yatatolewa Bure kabisa kwa vijana wote
Hivyo, tunapenda kuwatangazia vijana wa Kitanzania wenye umri kati ya miaka 15 hadi 35 wanaopenda kujiunga na mafunzo katika mojawapo ya fani zilizoorodheshwa hapo juu wafike katika vyuo vilivyoainishwa na Tangazo hili hapa chini ili kuchukua fomu ya kuomba kujiunga na mafunzo. Serikali itafadhili ada ya mafunzo kwa asilimia 100.
Mwanafunzi / mzazi / mlezi atagharamia gharama nyingine zikijumuisha nauli ya kwenda chuoni na kurudi nyumbani bhasi..
Maombi yawasilishwe kuanzia tarehe 01/11/2023 hadi tarehe 14/11/2023 yakiambatana na nyaraka zilizoorodheshwa...
HUENDA HAWA WAKAWA NDO WALIMU WA MAFUNZO YA AMALI KWA MTAALA WETU MPYA TUCHANGAMKIE VIJANA
Pitia hapa:
Nafasi za masomo fani mbalimbali kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu